Eneo la Selander Bridge limekuwa ni makao ya wauaji

kapuchi

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
268
163
Wadau wa JF,

Napenda kuwaletea tahadhari hii,juzi rafiki yangu alikuwa anatoka mjini saa tatu usiku, akirudi nyumbani kwake Sinza akipitia Bagamoyo Road.

alipokuwa anapita daraja la salander, mbele kidogo pale kwenye vichaka vya miti miti mingi opposite na bahari,ghafla gari yake ikazima akampigia simu rafiki yake aje amsaidie. Yule rafiki yake akamwambia usishuke kwenye gari,asubiri kidogo anakuja.

yule rafiki yangu alipoona,yule mtu aliyemwita amsaidie anachelewa akasema ngoja nishuke nifunue boneti inawezekana ni kitu kidogo kinachosumbua.

Akafungua mlango aliposhuka tu,mara likaja kundi la vijana kama kumi wakamzunguka wakampiga sana, wakamyanganya laptop.hand bags,simu,na vitu vingine vilivyokuwa kwenye gari.

moja wa wale wezi akampiga na nyundo mguuni kwenye kisigino,kikaninginia kinatoa damu,baadaye wale jamaa wakakimbia wakamwacha anavuja damu.

ikapita gari moja, kutoka mjini ndio ikambeba kumpeleka Agakhan ambapo amelazwa hadi hii leo. Damu inasemekana ilimwagika sana kama asingewahiwa kuongezewa damu huenda angepoteza maisha.

jamani habari ndiyo hiyo.ya msitu wa salander bridge.
 
Hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, Salender bridge iko karibu kabisa na kituo cha Polisi, sasa majamaa lakini bado yanaweza kujiicha hapo kusubiri mawindo yao. Morogoro road maeneo ya Jangwani nayo ni hatari mno, sasa pale hata kituo cha Polisi hakuna karibu. Lakini maeneo mengi Dar kwa sasa ni hatari sana kupita usiku.
 
moja wa wale wezi akampiga na nyundo mguuni kwenye kisigino,kikaninginia kinatoa damu,baadaye wale jamaa wakakimbia wakamwacha anavuja damu
.
hii habari imebase kwenye ukweli kabisa, imemtokea mtu huyo kweli, na mimi ninajua imetokea.
Poleni sana wandugu.
hili eneo ni ukanda wa hatari sana, na Jeshi la Police linajua, lakini wanasubiri mpaka binamu ya Mwema afe pale.
 
Ni kweli kabisa maeneo ya selander bridge ni hatari
hasa kuanzia mida ya saa moja usiku.
Na sio tu mpaka gari likuharibikie
bali wale majangili huwa wanavamia hata gari ikiwa kwenye foleni hasa ukiacha vioo wazi.
Nawashauri wana JF ikifika mida hiyo, ukiwa kwenye foleni
kwa usalama wako pandisha vioo vyote.
maeneo ya Jagwani ni hatari zaidi hata mida ya mchana kweupe.
 
Very sad. Mpe Pole Rafiki yako na asante kwa ujumbe huu. Something should be done haraka ile sehemu otherwise mambo yatakuwa si mambo muda si mrefu. Kova sijui Mwema sijui nani send your boys pale tafadhali.
 
Ni kweli Salender Bridge ni hatari japo kwa wiki nzima iliyopita naona kama kuan watu wanalinda nadhani wameona ni hatari
 
Du kweli bong tambarare na mita chache tu kuna kituo kikubwa cha polisi.
 
Jamani Salender Bridge mbona kuna visa hivyo., mara jini manyoya mara ujambazi, eneo lile na maeneo mengine kama Ocean Road na Jangwani hata ukipata pancha ni bora utembelee rim hadi sehemu yenye usalama zaidi, maisha yetu watanzania yamekuwa ya wasiwasi sana, hatuna tofauti na watu wa Darfur.
 
Kwani kuna polisi dedicated Tanzania? Wanapanga deal za hela tu. Pale ni tishio.Nilitegemea hadi sasa watakuwa wameweka patrol ya kudumu pale lakini wapi. Eti IGP ainakuja na mpya ya kuwazawadia watakaokataa Rushwa. Hakuna kitu kama hicho. Sema wanaandaa mchezo wa kuwabambikiza watu rushwa za uongo za design ya kina Murro. Kesi za kubambikizwa zitaongezeka sana.
 
Wabunge wakipunguzwa na kubaki 125 tu, tutaweza kuongeza idadi ya polisi kwa zaidi ya askari 10,000. Fikiria ni kwa kiasi gani wangeweza ku-patrol vichochoro vya miji yetu mikuu. Matumizi yetu mabaya ya mali zetu ndio yanayofanya tushindwe kuhudumia jamii.
 
Wadau wa JF,

Napenda kuwaletea tahadhari hii,juzi rafiki yangu alikuwa anatoka mjini saa tatu usiku, akirudi nyumbani kwake Sinza akipitia Bagamoyo Road.

alipokuwa anapita daraja la salander, mbele kidogo pale kwenye vichaka vya miti miti mingi opposite na bahari,ghafla gari yake ikazima akampigia simu rafiki yake aje amsaidie. Yule rafiki yake akamwambia usishuke kwenye gari,asubiri kidogo anakuja.

yule rafiki yangu alipoona,yule mtu aliyemwita amsaidie anachelewa akasema ngoja nishuke nifunue boneti inawezekana ni kitu kidogo kinachosumbua.

Akafungua mlango aliposhuka tu,mara likaja kundi la vijana kama kumi wakamzunguka wakampiga sana, wakamyanganya laptop.hand bags,simu,na vitu vingine vilivyokuwa kwenye gari.

moja wa wale wezi akampiga na nyundo mguuni kwenye kisigino,kikaninginia kinatoa damu,baadaye wale jamaa wakakimbia wakamwacha anavuja damu.

ikapita gari moja, kutoka mjini ndio ikambeba kumpeleka Agakhan ambapo amelazwa hadi hii leo. Damu inasemekana ilimwagika sana kama asingewahiwa kuongezewa damu huenda angepoteza maisha.

jamani habari ndiyo hiyo.ya msitu wa salander bridge.

Kwani ni mgeni Dar??? hajui S.B palivyo??? na kaonywa na rafikye kadharau!!!
btw mpe pole
 
Inabidi mkuu wa kituo cha Polisi Salendar Bridge awajibike kwa matukio ya aina hii. Haiwezekani majambazi wafanye uhalifu eneo jirani ni kituo cha polisi na wao wasiwe na taarifa. Kuna minong'ono kwamba polisi hugawana chochote na hawa majambazi na hata vibaka ili waendelee kuwa-protect. Hatuwezi kuacha hali kama hii iendelee. Heads must roll! Ukipita maeneo yale utawaona traffic wako bize kusimamisha magari, hasa ya foreigners na wahindi, na kuwachomoa pesa kwa vikosa vidogo vidogo. Shame on you police officers!
 
Kapuchi asante sana kwa taarifa yako
Hiyo habari ni ya kweli kabisa, Alopigwa mapanga namjua sana, na kabla hajapigwa nilikuwa naye,Anaitwa Jerry, na nilienda kumuungalia Agakhan, hali yake inasikitisha sana, hawa wauaji wameshamtia matatizo makubwa rafiki yetu,Mungu atamsaidia, Huenda kapuchi mimi na wewe tunajuana, ni pm ili tupeane majina yetu ya kweli
 
huyo Jamaa aliekatwa kisigino , ni mfanyakazi wa pale UNHCR hapa Dar es salaam, jamaa alienda kumuona Juzi, hali yake ni tata, ila bado anaumwa.
 
Polisi wakiitwa kwamba kuna ujambazi sehemu wanasuasua lakini ukiwaita kwamba kuna mzigo wa magendo sehemu wanakuja fasta!!!!
 
Kuna kituo jirani kabisa na hili eneo, ama kweli bongo tambarareeee....

jamani tujulishane maana hili soo linaweza kumpata yeyote - hata pale magomeni bondeni unapoenda faya - saa nne - na kuendelea ukipata tatizo na gari lako ukishuka tu wafwaaa....
 
Du kweli bong tambarare na mita chache tu kuna kituo kikubwa cha polisi.
Hivi kile kituo kina polisi wa kawaida au ni trafic police tu? coz huwa naona tarfic police kama ishirini pale wakati wa mchana, tena wanavizia magari kwenye foleni, wanacheck stickers!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom