BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,365
- 8,097
Siku moja baada ya kifo cha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Igunga, Fatma Omary na watu wengine wawili kwa ajali ya gari, tayari eneo la Inyala mkoani Mbeya sehemu hiyo imeanza kutafutiwa ufumbuzi.
Leo Alhamis, Septemba 15, 2022, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (RC), Juma Homera amezindua barabara ya mchepuko eneo hilo yenye urefu wa kilometa 2.8.
Jana Septemba 14,2022 eneo hilo lilisababisha kifo cha Mkurugenzi wa Igunga, Fatma Omary dereva wake, Alex Mtabika (48) pamoja na Shafih Said.
Homera amesema eneo hilo limekuwa na changamoto kubwa na kusababisha ajali kila wakati jambo ambalo kwa sasa limepatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Matari Masige amesema kwa sasa barabara hiyo itatumika kwaajili ya magari madogo pamoja na yale ya abiria.
"Tutaendelea kuboresha zaidi eneo hili kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kuhakikisha sehemu hii inakuwa salama zaidi kwa wananchi hasa waendesha vyombo vya moto," amesema Masige.
Mwananchi