Eneo alilopatia ajali Mh. Hayati Edward Moringe Sokoine hapo Wami Dakawa Halijapewa Hadhi inayostahiki

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,036
3,479
Wakuu,

Yapata takribani miaka 36 tangu waziri mkuu Edward Moringe Sokoine afariki kwa ajali ya gari huko Wami-Dakawa akitokea Dodoma baada ya kuahirisha bunge tarehe 12/4/1984 akielekea Jijini Dar Es Salaam. Eneo linalodaidaiwa ndipo ajali ilitokea baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na gari lililokuwa likitokea Morogoro kuelekea Dodoma lililokuwa likiendeshwa na raia wa afrika kusini aitwaye Dube; kimsingi mnara na shule iliyojengwa eneo hilo haiwakilishi hadhi ya kiongozi huyo ambaye ambaye alisimamia ipasavyo vita dhidi ya ulanguzi, ubadhirifu wa mali za umma,, uhujumu uchumi na uzembe kazini. Pia alihimiza ipasavyo shughuli za kilimo cha kufa na kupona baada ya majanga kadhaa na kukataliwa misaada na mikopo kutoka kwenye mashirika makubwa ya fedha ya kimataifa yaliyotoa masharti yaliyokuwa yanaingilia uhuru wa nchi, tamaduni na desturi za Mtanzania.

Eneo hilo bado limezungukwa na misitu mikubwa karibu na makao makuu ya wilaya ya Mvomero

Mapendekezo kwa uboreshaji

1. Uoto wa asili udumishwe na kuhifadhiwa vema;
2. yale magari yaliyohusika kwenye ajali eneo hilo yapelekwe eneo hilo na kujengewa ili kuvutia utalii
3. Barabara kati ya Makunganya na Wami Dakawa ipanuliwe njia nne ili kupunguza ajali kwa kuwa bado tatizo hilo linaendelea sana maeneo hayo na kukatili uhai wa wananchi na mifugo
4. Ujenzi wa mnara na shule hautoshi badala yake kianzishwe chuo cha ufundi na ujasiriamali kwa vijana ukijumuisha kilimo biashara, ufugaji bora, ufundi ujenzi, ufundi seremala, ufugaji nyuki na samaki kwenye bwawa ambalo linatakiwa kuchimbwa

Hayo na baadhi ya nyongeza yanaweza kuongeza kipato kwa taifa kwa njia ya utalii na kuwezesha vijana kujitegemea kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi hivyo kuchochea maendeleo na kupunguza umaskini katika jamii husika
 
Wakuu,

Yapata takribani 26 tangu waziri mkuu Edward Moringe Sokoine afariki kwa ajali ya gari huko Wami-Dakawa akitokea Dodoma baada ya kuahirisha bunge tarehe 12/4/1984 akielekea Jijini Dar Es Salaam. Eneo linalodaidaiwa ndipo ajali ilitokea baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na gari lililokuwa likitokea Morogoro kuelekea Dodoma lililokuwa likiendeshwa na raia wa afrika kusini aitwaye Dube; kimsingi mnara na shule iliyojengwa eneo hilo haiwakilishi hadhi ya kiongozi huyo ambaye ambaye alisimamia ipasavyo vita dhidi ya ulanguzi, ubadhirifu wa mali za umma,, uhujumu uchumi na uzembe kazini. Pia alihimiza ipasavyo shughuli za kilimo cha kufa na kupona baada ya majanga kadhaa na kukataliwa misaada na mikopo kutoka kwenye mashirika makubwa ya fedha ya kimataifa yaliyotoa masharti yaliyokuwa yanaingilia uhuru wa nchi, tamaduni na desturi za Mtanzania.

Eneo hilo bado limezungukwa na misitu mikubwa karibu na makao makuu ya wilaya ya Mvomero

Mapendekezo kwa uboreshaji

1. Uoto wa asili udumishwe na kuhifadhiwa vema;
2. yale magari yaliyohusika kwenye ajali eneo hilo yapelekwe eneo hilo na kujengewa ili kuvutia utalii
3. Barabara kati ya Makunganya na Wami Dakawa ipanuliwe njia nne ili kupunguza ajali kwa kuwa bado tatizo hilo linaendelea sana maeneo hayo na kukatili uhai wa wananchi na mifugo
4. Ujenzi wa mnara na shule hautoshi badala yake kianzishwe chuo cha ufundi na ujasiriamali kwa vijana ukijumuisha kilimo biashara, ufugaji bora, ufundi ujenzi, ufundi seremala, ufugaji nyuki na samaki kwenye bwawa ambalo linatakiwa kuchimbwa

Hayo na baadhi ya nyongeza yanaweza kuongeza kipato kwa taifa kwa njia ya utalii na kuwezesha vijana kujitegemea kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi hivyo kuchochea maendeleo na kupunguza umaskini katika jamii husika
Ni Miaka 36 mkuu Intelligence Justice
 
Namshukuru Mzee Mwanakijiji kwa kuniwezesha kusikia na kuona clip ya Hayati Edward Moringe Sokoine. Baada ya kuhangaika sana Mtandaoni kuitafuta huku GENTAMYCINE akinitishia kuwa nitakamatwa na kutupwa sero kwa kutaka kufuatilia masuala ya Hayati Sokoine. Hii ni baada ya kuanzisha uzi hapa jukwaani kwa ajili hiyo.
 
Kumbe GENTAMYCINE ana mambo ya KIFALA?
 
Endelea Kunitafuta Mkuu utanipata. Siku hizi huwa ninaanza na Kuwaonyeni Kwanza na mkiendelea nawaonyesheni tu Mapigo ya Haki ya Kiyahudi.
Acha mambo ya KIFALA kujifanya una mikwala mbuzi nyuma ya keyboard.

Sio kila mtu unaparamia, utakuja kusokomezwa kisu cha makalio.
 
Back
Top Bottom