Ciprofloxacin.
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 1,583
- 2,697
Hao waliojitokeza kwenda kupima DNA kwa kuwa wana mashaka na watoto walionao kuwa si damu yao nadhani wanaweza kuwa 1% ya watanzania wote,na bado 50% nusu yao wamebainika kuwa watoto wanaowalea si damu yao,kisa hiki kimenikumbusha mwaka juzi wakati nilimsindikiza rafiki yangu na jirani yangu kupeleka vipimo vya DNA,mimi tangu awali nilikuwa najua kuwa mke wa rafiki yangu anachepuka lakini kumwambia haikuwa jambo rahisi,sijui machale yalimcheza vipi akaamua kucheki DNA,alipopata majibu na kurudi nyumbani alichoma nguo zote za mkewe na watoto feki wawili,naposema zote ni zote hadi nguo za ndani pamoja na vitenge na sidiria kisha akampiga karibia ya kumuua,na kumlaza nje na watoto,alikamatwa na kuwekwa mahabusu,mwanamke kwa kujua ni kosa lake akamtetea mumewe kuwa si yeye aliyempiga,tulimstiri mavazi na watoto wake,sasa najiuliza itakuwaje endapo Tanzania nzima itaamua kupima DNA? Nahisi 78% ya ndoa zitakufa kabisa,uaminifu kwenye ndoa ni mgumu sana,ndo maana kuna wanaume wameamua kuishi kibachela hadi kufa.