Endapo TANU/CCM ingewasikiliza wenye mawazo mbadala, leo taifa letu lingekuwa mbali sana kiuchumi na kwenye hali za maisha za wananchi.

Leo hii ingawa wengi wanamsifu nyerere Ila kwa watu Wenye akili wote wanajua chanzo kikuu cha Tanzania kufeli ni sera mbovu za ujamaa za Mwalimu nyerere zilizopingwa na Kambona hadi kupelekea kukimbia Nchi.
Lord denning hapa umemaliza kila kitu mtu ukiwa makini utagundua Teacher alikuwa mwepesi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyerere mwenyewe alikuja kugundua badae kuwa alikuwa kiongozi mbovu maana alipinga mawazo mazuri kwa mabavu. Ukisikiliza hotuba zake za mwishoni ni kama alikuwa akijutia sana makosa yake.
 
Hii nchi ilianza vizuri sana ila matukio yaliyotokea mpaka tukafika hapa tulipo ni moja ya mambo ya kusikitisha Sana.
Tanzania ni kweli tulikuwa pazuri sana. Endapo mfumo wa kiuchumi ungekuwa uleule tuliorithi kutoka uhuru na labda tungeuboresha kidogo tu tungekuwa taifa la mfano wa kuigwa kiuchumi. Tulikuwa na matajili wengi sana Wakulima ambao walikuwa wameshajijenga tangu kipindi cha mkoloni. Tungewatumia vizuri leo Nchi yetu ingekuwa pazuri sana.
 
Hoja yako ina mashiko,Leo Tanzania ina umaskini wa kutupwa ,Leo hii Tanzania ipo kundi mmoja na nchi kama Somalia kwenye takwimu za umaskini ,ni aibu kupindukia,somalia haijawahi kushudia amani ni vita kila uchao wanayosababu ya kujitetea kwa umaskini walionao
Tanzania hatuna sababu ya kujitetea hata moja ,sababu kuu ni ubovu wa watawala,hawana maono ,hawataki mawazo mbadala،kimsingi ccm ndiyo sababu kubwa ya umaskini wa wananchi,ccm kinaongozwa na watawala wasio na maono na wanaligharimu taifa kwa kiasi kikubwa,wanasera mbovu na za kubahatisha,hawajui maana ya maendeleo,wanafikiri maendeleo ni kuwa na magari mazuri,ndege nzuri,majengo marefu,barabara za fly over,kila kitu wanafanya siasa wanaacha kuweza kwa wananchi wanawekeza kwenye vitu,Leo corona imepiga hodi,wanatokwa na macho,hawajui wafanye nini,kwa sababu hawakuwekeza kwa wananchi, nchi zinazojitambua zina weka sheria za lock down kwa wananchi wao ili kuokoa maisha ya watu wao,sisi tunasema wananchi wetu ni maskini hatuwezi kuweka lock down,nani aliwefanya wananchi wa Tanzania wawe maskini,ni kweli ukiweka watu lock down watakufa njaa sababu nchi haijawekeza kwenye kilimo,kilimo sio kipaumbele chao,chakula cha wananchi sio kipaumbele chao,hawajawekeza kwenye uzalishaji vya kutosha,ukiangalia maisha ya watu utakuta hata debe la unga ndani hakuna wanaishi kwa robo kilo .really we are going to face a heavy disaster, and each of us we will pay for they weakness

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa. Tulikuwa tumeruthi mfumo mzuri sana kutoka kwa wakoloni. Elimu na hata uchumi. Tulitakiwa kuboresha padogo sana na kujijenga vizuri kukua zaidi na zaidi. Makosa ya TANU na baadae CCM kutosikiliza mawazo yenye akili kubwa kwa hofu ya madaraka tu yamelighalimu sana Taifa letu.
 
Uzi wako unataka kunitoa machozi. Watanzania tumefunzwa kuwasifu waovu na kuwadhalilisha wasema kweli.
Labda siku za usoni tutabadilika.

Ila nausubiri kwa hamu uzi utakaomhusu genius wetu wa kizazi hiki Tundu Antipas Mughwai Lisu (TAML).
List ni ndefu sana kwa kweli. Wa kwanza alikuwa huyu Oscar Kambona ambae kwa ujinga wa watu waliaminishwa mabaya juu yake ila leo hii watu tunaona kuwa alikuwa sahihi dhidi ya sera za ujamaa za mwalimu Nyerere.
 
Nyerere mwenyewe alikuja kugundua badae kuwa alikuwa kiongozi mbovu maana alipinga mawazo mazuri kwa mabavu. Ukisikiliza hotuba zake za mwishoni ni kama alikuwa akijutia sana makosa yake.
Muda ni kitu kibaya sana mkuu kwani humfanya mtu kujutia maovu na uzembe wake mf: ni mzee wa riwaya ya mailaif maipapas

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa. Tulikuwa tumeruthi mfumo mzuri sana kutoka kwa wakoloni. Elimu na hata uchumi. Tulitakiwa kuboresha padogo sana na kujijenga vizuri kukua zaidi na zaidi. Makosa ya TANU na baadae CCM kutosikiliza mawazo yenye akili kubwa kwa hofu ya madaraka tu yamelighalimu sana Taifa letu.
Mpaka sasa. Nchi inaangamizwa na wajinga wa CCM. Kila mawazo ya kuinyanyua nchi wanayapinga na kuyazuia kwa nguvu za dola.
 
Back
Top Bottom