Endapo Serikali itawapa kipaumbele cha ajira Walimu wanaojitolea, madhara haya yanaweza kutokea

Ikitotanzila

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
1,409
2,263
Waalimu ambao hamjaajiriwa Pole nyingi ziwafikie,mimi kama mdau wenu niliyewahi kuwa mhanga kwa miaka 4 na tangu 2015-2019*tushare mawazo kidogo👇
Endapo serikali itakuwa serious kuweka kigezo cha kujitolea kuwa ndicho kigezo kukuu cha kuajiri waalimu madhara yafuatayo yatajitokeza.

1. vijana wasomi watakuwa masikini sana:
Kwani muda mwingi watakuwa wanafanya kazi za bure isiyo na malipo

2. Ndoa za wasomi wasio na ajira zitakuwa na migogoro(especially jinsia ya me)
Sidhani kama kuna mwanamke atakayekuelewa eti umuache ndani na watoto afu ukajitolee jioni urudi mikono mitupu labda enzi za mwl miaka 1990 kurudi nyuma..labda atakayekuvumilia atachepuka ili kupata mahitaji muhimu.

3. Serikali haitaajiri tena kwa sababu kutakuwa hakuna upungufu wa waalimu
Kwa mfano wahitimu wote wakaamua kuzama mashuleni na kujitolea upungufu wa waalimu utatokea wapi tena?

4. Morali ya wanafunzi kusoma.kwa bidii utashuka
Hii itatokea pale wanafunzi watakapowaona waalimu wao wakiishi maisha ya shida(kumbuka wanafunzi hawataelewa kuwa mwl fulani anajitolea )wakiona unateseka watajua mshahara wa ualimu ni mdogo.kumbe huna hata sh Mia🙇.

5. Heshima ya ualimu utashuka tena kwa wanajamii
Kumbuka wanajamii wanaishi na waalimu na wao Wataona waalimu wa kujitolea wakipata tabu(jamani huwezi kuficha shida)sasa wananchi hawatakuwa ma muda wa kujua mwl wa kujitolea na mwl wa serikali.

Mwisho mimi naona kama ajira imekuwa shida sana na kigezo cha kuajiri kimekosekana "watumie kigezo cha mwaka wa kuhitimu chuo peke yake..asiajiriwe wa mbele wakati kuna aliyemlisha nyuma yake"hii kidogo ina mashiko kwa mbaaali na lawama yake ni ndogo.

Tofauti na hapo kiukweli tutatengenezewa Mussolini uliokwenda shule mpaka waliofeli zamani Wataona kuwa hawakufanya makosa.
 
Back
Top Bottom