Endapo Serikali itaacha kutumia mabavu kukusanya kodi, wafanyabiashara wapo tayari kulipa kodi bila kudanganya na kofoji "documents"?

Hakuna mfanyabiashara anaependa kulipa kodi popote pale ata iwe America! Kama wakina Ronaldo na Messi walikutwa na hatia ya ukwepaji kodi kwa kuto wasilisha taarifa sahihi sembuse huku kwetu?
Hakuna duniani mtu anayeweza kulipa kodi HALALI bila shurti,ikiwa trump bilionaire anashindwa kuwa mkweli kwenye kodi nani yuko tayari. Hata nchi zilizoendelea watu hulipa kodi kwa kubanwa tu . Short of that serikali icheze na nyani shamani ivune mabua.
 
Hakuna mfanyabiashara huyo. Tax rates zetu ziko juu sana bila ya kujali kipato cha lazima cha kujikidhi. Mwenye mtaji wa 10,000,000 , milioni 10 anakatwa rate sawa na mwenye mtaji wa 1,000,000,000,000, trillioni 1. Wakati huyu wa Milioni 10 anapata hela ya kula tu.

Kwa rates za sasa invoice halali ya container ya nguo itakubidi ulipe milioni 100+.
 
Mimi Nimeuliza swali Kwamba, Ikiwa kina Mbowe wenye mitaji mikubwa na wazoefu wa biashara kipindi cha JK hawakuwa wawazi kwenye kwenye biashara zao na wakawa wakwepa Kodi wakubwa Hadi kufikia madeni ya B2, Nani ataweza kulipa Kwa hiari?
 
Hivi sasa wafanyabiashara hawataki kutoa risiti za kielektroniki sasa wapi serikali itapata kodi za kufanya maendeleo naona kunasintofahamu kubwa sana , sijui hii serikali itaendeshwa vipi.
kuna kamsemo maarufu wanatumia ukiwabana kuhusu risti " nikupe ya kutembelea"
 
We umesikia wapi mfanyabiashara anapenda kulipa kodi!!?
Punda haendi bila fimbo bhana
 
Hizi kodi za Awamu ya tano zilikuwa za kihasidi sana zilikuwa za kukomoa Watanzania wapenda Amani

Kodi ziangaliwe upya na jopo la Wataalamu tena watoke nje ya Nchi wakishirikiana na Wafanyabiashara wa Tanzania

Halafu Mzee Bakhresa asimamie huo mchakato

Maha kwenye Kodi tatu nne hadi sita zinapunguzwa inabaki kodi moja ambayo ni rahisi kuielewa na inalipika
 
Pakiwepo mazingira rafiki na yenye kumjali mfanyabiashara kwa asilimia kubwa sana watu watakuwa wazalendo na hata kile wanachobaki nacho kitaisaidia nchi kwa namna moja ama nyingine.
Sio kwa m'bongo.
Tabia ya kudanganyadanganya ni inborn.
 
Duniani kote watu wote wanapenda kukwepa kodi , fikiria na mahela yote ya akina Messi walikwepa kodi , waziri Mkuu wa Italia alikwerpa kodi sasa serikali ijiingize kwenye kucheka na wafanya biashara itavuna mabua ,eti serikali itegemee mishahara ya wafanyakazi tutaona.,
 
Wote ni mashahidi kwa namna ambavyo watanzania wengi ni wagumu kufuata utaratibu pamoja na sharia halali zilizowekwa. Wengi wetu tunapenda sana kupata mali kirahisi na kwa njia ya udanganyifu ama rushwa.

Sasa je, serikali ikaamua kutumia upole na njia laini kukusanya kodi Watanzania wangapi watasema wamepata faida kwa halali kabisa bila kudanganya hasara hewa na za uongo?

Hili la kukwepa kulipa kodi linawagusa kuanzia mawaziri waliopo madarakani mpaka mama ntilie, ni nadra sana kumkuta mfanya biashara ameweka vitabu vyake safi na kwa ukweli mtupu bila kudangaya hapa nilipata hasara hapa, imekuwa hivi ilimradi akwepe kutoa ya kaisari.

Tunailaumu sana serikali kwakua ndio inayowajibika kuweka mambo sawa, lakini na sisi wananchi tujiuleze kweli tupo tayari kuwa nchi ambayo wote tutakuwa mstari wa mbele katika kufuata na kuwajibika mbele ya taratibu na sharia halali zilizowekwa.

Tujiulize nasisi: Je tupo tayari kumsaidia Mama Samia Suluhu Hassani kuitibu Tanzania ugonjwa wa

Wote ni mashahidi kwa namna ambavyo watanzania wengi ni wagumu kufuata utaratibu pamoja na sharia halali zilizowekwa. Wengi wetu tunapenda sana kupata mali kirahisi na kwa njia ya udanganyifu ama rushwa.

Sasa je, serikali ikaamua kutumia upole na njia laini kukusanya kodi Watanzania wangapi watasema wamepata faida kwa halali kabisa bila kudanganya hasara hewa na za uongo?

Hili la kukwepa kulipa kodi linawagusa kuanzia mawaziri waliopo madarakani mpaka mama ntilie, ni nadra sana kumkuta mfanya biashara ameweka vitabu vyake safi na kwa ukweli mtupu bila kudangaya hapa nilipata hasara hapa, imekuwa hivi ilimradi akwepe kutoa ya kaisari.

Tunailaumu sana serikali kwakua ndio inayowajibika kuweka mambo sawa, lakini na sisi wananchi tujiuleze kweli tupo tayari kuwa nchi ambayo wote tutakuwa mstari wa mbele katika kufuata na kuwajibika mbele ya taratibu na sharia halali zilizowekwa.

Tujiulize nasisi: Je tupo tayari kumsaidia Mama Samia Suluhu Hassani kuitibu Tanzania ugonjwa wa unafiki na uongo?
Usidanganyike.Dunia nzima kodi haikusanywi kwa mabavu.waingereza wanaita Win Win situation.serikali inafuata sheria na wafanyabiashara nao wanalipa kodi kwa kuwa wanajua sio hiyari ni lazima.Kwanza Ajira zitaongezeka,pili wahasibu watapata ajira mbali mbali,tatu wawekezaji wataongezeka sana katika sekta mbali mbali,tutaanza kuona pesa zipo mifukoni sio ahadi tu kama awamu ya 5.yapo mambo mengi.Mfano Ronaldo alipokuwa anaichezea real madrid alikuwa anadaiwa kodi ya dola milioni 8 lakini baada ya serikali na wawakilishi wake kuketi wakakubaliana alipe dola milioni 6.sababu kuu ya serikali ya hispania kumkubalia ni umaarufu wake uliyosaidia kuiingizia serikali ya huko mamilioni kwa watalii just kwenda kumwona,matangazo ya TV kuongezeka n.k Hawakutumia mabavu.Ndivyo serikali yetu ya awamu ya sita 6 itakavyofanya.Mfano hapa kwetu tunaye Muimbaji Diamond ambaye ni maarufu sana,sasa badala ya kuvifungia vyombo vyake kama wasafi TV n.k unamchaji kodi lakini pia unaangalia analiingizia Taifa kiasi gani.mwishowe mnakubaliana na kila mmoja anafaidika.Hakuna Nguvu wala Mabavu.Kwa taarifa watanzania wengibsana kuogopa kuswekwa ndani kwa kubambikiwa makodi haramu wamewekeza Rwanda,Mozambique,Uganda,Kenya,South Sudan,Malawi,Hata mpaka Afrika ya Kusini.NAWAOMBA WAFANYABIASHARA MRUDI NCHINI NA MSAJILI BIASHARA ZENU TANZANIA.TULIPE KODI KWA UAMINIFU NA TUWASHAWISHI WAGENI WAJE KUWEKEZA AIDHA KWA UBIA AU KWA WAO WENYEWE KUANZISHA BIASHARA ZAO.COME AND INVEST IN A TAX FRIENDLY COUNTRY CALLED TANZANIA.
 
Pakiwepo mazingira rafiki na yenye kumjali mfanyabiashara kwa asilimia kubwa sana watu watakuwa wazalendo na hata kile wanachobaki nacho kitaisaidia nchi kwa namna moja ama nyingine.
Awamu ya 2 na 4 serikali haikuwa ngangari kwenye ukusanyaji wa kodi matokeo yake sote tunayajua, serikali ilifilisika. Tuacheni masihara, hakuna mtu anayependa kulipa kodi. Hata huko marekani, TRA ya huko (IRS) ni wakali kama pilipili kichaa.
 
Wote ni mashahidi kwa namna ambavyo watanzania wengi ni wagumu kufuata utaratibu pamoja na sharia halali zilizowekwa. Wengi wetu tunapenda sana kupata mali kirahisi na kwa njia ya udanganyifu ama rushwa.

Sasa je, serikali ikaamua kutumia upole na njia laini kukusanya kodi Watanzania wangapi watasema wamepata faida kwa halali kabisa bila kudanganya hasara hewa na za uongo?

Hili la kukwepa kulipa kodi linawagusa kuanzia mawaziri waliopo madarakani mpaka mama ntilie, ni nadra sana kumkuta mfanya biashara ameweka vitabu vyake safi na kwa ukweli mtupu bila kudangaya hapa nilipata hasara hapa, imekuwa hivi ilimradi akwepe kutoa ya kaisari.

Tunailaumu sana serikali kwakua ndio inayowajibika kuweka mambo sawa, lakini na sisi wananchi tujiuleze kweli tupo tayari kuwa nchi ambayo wote tutakuwa mstari wa mbele katika kufuata na kuwajibika mbele ya taratibu na sharia halali zilizowekwa.

Tujiulize nasisi: Je tupo tayari kumsaidia Mama Samia Suluhu Hassani kuitibu Tanzania ugonjwa wa unafiki na uongo?
Kenya na Uganda panatosha kuwa mahali pa maafisa wetu kujifunza...
ACHENI KUKARIRI, KODI NI ELIMU...
KODI NI UZALENDO... ikiwa watu wanaporwa kwa nguvu fedha zao ama kubambikizwa kodi zisizostahiki kwanini kusiwe na janjajanja? Watumishi wa TRA wote ni waadilifu sana au wafanyabiashara wote ni walaghai?
 
Awamu ya 2 na 4 serikali haikuwa ngangari kwenye ukusanyaji wa kodi matokeo yake sote tunayajua, serikali ilifilisika. Tuacheni masihara, hakuna mtu anayependa kulipa kodi. Hata huko marekani, TRA ya huko (IRS) ni wakali kama pilipili kichaa.
Je sasa ukiacha fedha zilizoporwa kwenye akaunti za watu kodi ilikuwa bado ikikusanywa vilivyo? Au hukuona kasi ya kufungwa kwa biashara? Kwanini miaka miwili hii ya mwisho hatukutangaziwa mapato ya TRA kama ilivyokuwa awali? Mtu akikuta msingi mzuri ni hiyari yake kujenga nyumba imara ama kuijenga kwa zimamoto ili ionekane kasi ya ujenzi iko juu... ajae atajijua...
Je awamu ya 2 iliikuta nchi iko kwenye hali gani? Je 1978-1984 Revenue ilikuwa ikikusanya kiasi gani kwa mwaka? Ukipata majibu fananisha na 1985-1990...
 
Back
Top Bottom