winnerian
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 335
- 530
Wote ni mashahidi kwa namna ambavyo watanzania wengi ni wagumu kufuata utaratibu pamoja na sharia halali zilizowekwa. Wengi wetu tunapenda sana kupata mali kirahisi na kwa njia ya udanganyifu ama rushwa.
Sasa je, serikali ikaamua kutumia upole na njia laini kukusanya kodi Watanzania wangapi watasema wamepata faida kwa halali kabisa bila kudanganya hasara hewa na za uongo?
Hili la kukwepa kulipa kodi linawagusa kuanzia mawaziri waliopo madarakani mpaka mama ntilie, ni nadra sana kumkuta mfanya biashara ameweka vitabu vyake safi na kwa ukweli mtupu bila kudangaya hapa nilipata hasara hapa, imekuwa hivi ilimradi akwepe kutoa ya kaisari.
Tunailaumu sana serikali kwakua ndio inayowajibika kuweka mambo sawa, lakini na sisi wananchi tujiuleze kweli tupo tayari kuwa nchi ambayo wote tutakuwa mstari wa mbele katika kufuata na kuwajibika mbele ya taratibu na sharia halali zilizowekwa.
Tujiulize nasisi: Je tupo tayari kumsaidia Mama Samia Suluhu Hassani kuitibu Tanzania ugonjwa wa unafiki na uongo?