Endapo majina ya walioambukizwa Corona yatatangazwa hadharani patakuwa na ubaya gani?

Kwanza lazima ujue hata hao public figures ni wao wenyewe hujitangaza au huwaambia wasaidizi wao wawatangaze na siyo mtu mwingine anakurupuka tu na kutangaza! Kuhusu huyo mtoto, Makonda alifanya kosa kusa kubwa sana na angetakiwa awajibishwe kwa ujinga aliofanya. Familia ya Mbowe ikitaka inaweza kumshtaki ila serikali ilitakiwa kumwajibisha pia.
Nakubaliana na wewe RC Makonda...alifanya kosa kubwa...Hilo la ujinga sikubaliani na wewe...Familia ya Mbowe ikitaka inaweza kumshitaki...it was too bad kwa kweli....
 
Corona ni janga la kimataifa.

Prince Charles katangazwa, PM Boris katangazwa na PM Netanyahu katangazwa.

Sasa, najiuliza hapa Tanzania kuna ubaya gani kuwatangaza wenye dalili na wenye maambukizi?

Anayeweza kunijibu Tafadhali!
Hao unaowasema "hawakutangazwa", bali "wenyewe ndiyo wametangaza", vyombo vya habari wao wanatuhabarisha tu na kunakuja hiyo dhana kuwa wametangaza. Hakuna mtu anayeweza kujua kuwa ameambukizwa bila kupimwa, dalili zake ni nyingi na si kila atakaeambukizwa aonyeshe dalili, na pia kuna atakayekuwa na dalili lakini zikawa ni chanzo cha maradhi mengine. Ni hatari ambayo tumeamua kuifanyia dhihaka, itatugharimu.
 
Corona ni janga la kimataifa.

Prince Charles katangazwa, PM Boris katangazwa na PM Netanyahu katangazwa.

Sasa, najiuliza hapa Tanzania kuna ubaya gani kuwatangaza wenye dalili na wenye maambukizi?

Anayeweza kunijibu Tafadhali!
Ugonjwa wa mtu ni siri ya Daktari na mgonjwa, hata daktari mwenyewe haruhusiwi kutoa siri za mgonjwa specific, isipokuwa takwimu za ugonjwa tu basi. Serikali ndiyo kabisa hawana mamlaka hayo. Mgonjwa mwenyewe ndiyo ana mamlaka ya kutangaza ugonjwa wake, kama akiamua kufanya hivyo, lakini naye pia kwa rdihaa ya madaktari wake na Serikali pia. Kwenye mambo haya watu huwa hawaibuki tu kama vile kwenye swimming pool!
 
Back
Top Bottom