Endapo Kampeni ya kumzuia JK kugombea 2010... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Endapo Kampeni ya kumzuia JK kugombea 2010...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 18, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 18, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Endapo kampeni ya kumzuia JK kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM 2010 itafanikiwa Taifa letu litakuwa matatani kwani itakuwa ni mgawanyiko ambao Taifa haliwezi kustahimili. Kwa ajiili ya amani, umoja, na mshikamano vyovyote vile ni lazima Kikwete awe mgombea wa CCM. Nje ya hapo Nchi yetu itayumba.

  Think you are doing that history paper ambapo uliulizwa "discuss how the British used indirect rule in colonial Africa compared to the system of assimilation used in French colonies".
   
  Last edited by a moderator: Nov 18, 2008
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kila muhula wa miaka mitano unapoisha kwa Rais ni sahihi kwa wananchi wanaoamini kuwa wana uwezo na malengo mazuri ya kuongoza nchi kuwaomba wanachi kupewa fursa hiyo. Hakuna sababu yoyote ya nchi kuyumba kwa sababu ukweli ni kwamba wako watanzania wengi wenye uwezo wa kusimamia utawala wa nchi yetu iwapo watapata fursa hiyo toka wananchi. Kumzui JK kugombea ni mawazo ya wasioelewa maana ya demokrasia, JK ana haki zote za kugombea - sasa kwa nini azuiliwe???na je ni nani mwenye mamlaka hayo??? Sanasana kama mtu ana sababu za msingi anaweza AKAMSHAURI asigombee, lakini sio kumzuia.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kichwa cha habari cha thread kina-syntax error..
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Nov 18, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Yeye sio Mungu na Tanzania sio mali yake! Tanzania ilikuwepo kabla yake na itakuwepo baada yake. Tanzania sio ya mtu mmoja. Tanzania ni ya watu milioni 38-40. Hii dhana ya kumtegemea mtu mmoja na bila yeye hatuwezi ku survive ni dhana ya kichovu. Mimi sijali kama chama chake kitamteua kugombea tena au vipi. Kwanza sijui hata utaratibu wao wa kuchagua wagombea ukoje. Ninachojali mimi ni kupata mgombea mbadala ndani au nje ya CCM mwenye sifa za uongozi na aliye na rekodi ya utendaji wa kazi wenye matokeo mazuri. Hii sio guarantee kwamba mtu huyo atakuwa raisi bora (kuliko Kikwete) lakini angalau tutakuwa na matumaini halisia kuwa anaweza kuja kufanya kazi nzuri.

  Narudia tena. Tanzania sio mali ya mtu mmoja na haitegemei mtu mmoja kuiongoza. Kikwete na CCM ni binadamu kama sisi wengine na wala sio wateule wa Mungu walioletwa kuja kuongoza Tanzania (kuna baadhi ya watu wanaamini hivyo). Waondoke tu na sisi tutakuwa just fine.
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Kipindi cha kwanza (1985 - 1990) cha Mhe. ally Hassan Mwinyi aliongoza nchi vizuri ndiyo maana alipewa kipindi kingine. Hata hivyo aliharibu sana, uchumi wa nchi ulidorora kabisa, migomo ilitapakaa, hali ya kisiasa ilikuwa mbovu kabisa ndani ya CCM. Hali kadhalika Mhe. Ben Mkapa, alifanya vizuri sana katika kipindi cha kwanza. uchumi ulipanda, miundominu ilianza kujengwa hasa barabara. hali ya kisiasa ndani ya CCM ilikuwa tulivu kabisa. Kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, alipewa awamu nyingine ambayo aliboronga sana. Hali ya uchumi ikaanza kuyumba tena, kero zikaongezeka, migomo ikaanza tena kwa kasi, ujambazi ukaongezeka mara dufu. Pia hali ya kisiasa ndani ya CCM ikawa mbaya kabisa huku Wanamtandao wakiwa vinara katika kuendesha propoganda na siasa chafu.

  Mhe. JK ameharibu toka awamu yake ya kwanza; uchumi umekuwa ovyo, migomo, hali ya kisiasa ndani ya CCM ni mbovu than anytime before. Watanzania wamekata tamaa, hakuna falsafa hasa baada ya kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya kuzikwa na richmond. Sasa kunasababu gani ya kumpa Kikwete awamu ya pili?

  Kikwete alipoingia madarakani alisema kuwa watangulizi wake wamejenga msingi imara, kazi yake ni kujenga ukuta tu. Je! huo ukuta uko wapi? misingi anayosimamia ya waliopita iko wapi? aibu kwa Mtawala kushindwa kuficha udhaifu wake.

  Pia historia ya watawala waliotangulia inatuonyesha kwamba kipindi cha pili huwa ni kuharibu na siyo kujenga. Je, huyu Kikwete, aliyeshinda kipindi cha kwanza, cha pili si itakuwa balaa? Somo la Mwinyi na Mkapa linatutosha kwamba Rais anapaswa kuwa wa kipindi kimoja tu.

  namshauri mhe. kikwete asigombee 2010. nchi itakuwa shwari tu. Kunawatu wenye uwezo na moyo wa utumishi na uzalendo, watakaokuwa tayari kuiongoza nchi.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mimi nadhani hiyo itakuwa ni mwanzo wa kukua kwa demokrasia na uwajibikaji ndani ya taifa letu maana hata hao viongozi watakaokuja thereafter they will have that in mind kwamba usipodeliver hata hiyo tano ya mwanzo unaweza usifikishe.

  Cha msingi JK from now should prove to us Tanzanians and not CCM kwamba ni kwa nini tumpe tena the last 5 yrs. Akishindwa hata hao CCM wakimpitisha tumpige chini.

  Can we do it?????????????

  YES WE CAN!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Nov 18, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hii ya yes we can inanikumbusha nguvu mpya, ari mpya, na kasi mpya...(I don't necessarily know the order)......hii mi slogan ni ya kuchota tu akili za watu. Viongozi ambao ni viongozi huwa hawatumii slogan zinazo-chant-iwa na mijitu mingi
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,570
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu mfanyakazi anastahili kupewa tena mkataba mpya kufuatia utendaji wake mzuri wa mkataba uliokwisha ambao umewaridhisha wale waliomuajiri. Kikwete mpaka sasa hivi utendaji wake hauridhishi kabisa na Watanzania wengi tumekatishwa tamaa na utendaji wake.

  Kwa mantiki hiyo basi CCM kama kweli wana demokrasi iliyokomaa ndani ya chama chao basi hawastahili kumpa Kikwete nafasi hiyo bali wamtafute mtu mwingine atakayeweza kukisafisha chama hicho na kuiongoza Tanzania vizuri ili ipate maendeleo yanayostahili na pia kupambana na mafisadi bila woga. Kuna sababu chungu nzima za kuwa na Rais mpya baada ya uchaguzi wa 2010.
   
 9. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2008
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Sorry kama nitawakwaza watu lakini ku generalize hivi mfano "Watanzania wengi tumekatishwa tamaa na utendaji wake binafsi napenda kupingana nao. hivi hatuwezi kufanya surveys tukapata statistics. wengi maana yake ni 50%, or 70% or what? katika 35+million. Inaweza kuwa 10% hawampendi. mnasemaje wakuu? kuna NGO na hata mashirika mbalimbali, wangeweza kuja na numbers. Hatuwezi kujifananisha na USA lakini tungeweza kuelekea huko kwa kuwa na % wanapendelea nini, ingetusaidia kuwa na Directiion nzuri. otherwise tunajadili tukiwa gizani.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,570
  Trophy Points: 280
  Kwani mpaka tutafute statistics!? Utatafuta vipi statistics wakati ambapo Watanzania wengi wnaoishi vijijini hawana mawasiliano yoyote kupitia magazeti, redio au TV ili kujua nini kinaendelea ndani ya nchi yao? Tunajua ahadi ambazo Kikwete aliahidi wakati wa kampeni zake ambazo ndizo zilizomfanya achaguliwe kwa 'ushindi wa Tsunami' Je, ni kipi alichokifanya hadi hii leo kutimiza ahadi hizo!!!? Jibu ni hakuna chochote alichokifanya. ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya, maisha bora kwa kila mtanzania, nitaipitia upya mikataba ya dhahabu ili kuhakikisha Tanzania inanufaika na rasilimali zake yote yalikuwa ni maneno hewa tu. Sasa mtu kama huyu anastahili kweli kurudishwa madarakani kwa kipindi kingine cha miaka mitano!!?
   
 11. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kikwete kukoseshwa nafasi ya kuwania urais mwaka 2010 ni vibaya kama vile ilivyo vibaya mtu yeyote, akiwamo Shibuda, kunyimwa nafasi ya kuwania urais.

  Kwa "kukoseshwa nafasi ya kuwania urais" namaanisha kukoseshwa nafasi hiyo ndani ya CCM.Ushindi wa kweli dhidi ya Kikwete ni pale atakapopewa nafasi ndani ya CCM na kushindwa kupata wajumbe wa kutosha, au kupata wajumbe wa kutosha na kuiwakilisha CCM lakini kushindwa kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu.Ushindi mwingine wowote utakaohusisha kumkatalia kabisa Kikwete kushiriki katika mchakato huu utampa nafasi Kikwete kuweza kusema kuwa hakushindwa kihalali.

  Swala kubwa ni kwamba, je, tumedhamiria kusimamia demokrasia kwa kiasi gani? Tukianza kuyumbishwa na hizi habari za "mgawanyiko" ndipo tunapoanza kufikiria kwamba "Watuhumiwa wa EPA hawashitakiki kwa maana wakishtakiwa nchi haitatawalika".

  Utawala wa sheria, demokrasia na misingi ya utaifa visimame juu kuzidi kitu chochote, ukiwamo uoga wa kupandikizwa na wachache.

  Waacheni CCM waamue kidemokrasia bila mizengwe, kama wanamtaka Kikwete sawa, kama wanamtaka Shibuda sawa, kama wanamtaka Lowassa sawa.Halafu wawaachie Watanzania wafanye uchaguzi, liwalo na liwe al muradi limekuwa kidemokrasia ya kweli.

  Tusije kuwa kama Wamarekani ambao waliingia mashariki ya kati kwa mbiu ya kutaka kuleta demokrasia, sasa wanaona demokrasia kwa waarabu inaweza kumaanisha wananchi kuwachagua vyama vyenye mlengo wa kigaidi, wanaweza vizingiti katika demokrasia hiyo.

  Bila kumuwekea njama Kikwete, tutake demokrasia ishinde.Kama kuna haja ya kuwaelimisha wananchi kuhusu uozo wa Kikwete na CCM na ufanyike kidemokrasia, kama kuna sababu ya kutotaka Kikwete asiwekewe njama za kumzuia kuwania urais, iwe ni kutokana na kusimamia demokrasia na haki ya Kikwete kuwania urais, siyo kwa sababu ya mbegu za uoga zinazopandikizwa na wasioweza kukubali ukweli na gharama ya kweli ya demokrasia, endapo tuna harara ya kumuonea imani Kikwete, basi imani hii itokane na sababu za msingi.
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Nov 18, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii 'yes we can" najua una beef nayo kibinafsi twende kwenye hoja maana tukianzisha mjadala wa ni namna gani slogans zimeweza kuleta changes duniani, uuhshhhhhhhhh! sorry najua neno "change" pia hulipendi well the list is long.

  Enway turudi kwenye hoja..........
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Nov 18, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Tusiende mbali...tuanze na ari mpya, nguvu mpya, na kasi mpya na maisha bora kwa kila Mtanzania.....hizi kauli mbiu zimeleta mabadiliko gani Tanzania..?
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Well this is if any of us believed it, kiukweli hii ilikuwa ni vague statement na watanzania hata hatukuwahi kuuliza how and when. Na ndio maana hazisikiki tena na mayb we wil neva hear 'em again!!!!!!!!!!!!!
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Nov 18, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Okay, tuje Marekani sasa na hii ya change change change.....zaidi ya kumchagua raisi chotara, ni change gani watu wanayotegemea? Kwamba serikali itaanza kulipia car note na mortgage note zao kila mwezi na kuwawezesha watu kubakiza hela nyingi za matumizi hence kuboresha maisha zao au?

  Au ndio yale yale ya kuibuka na "vague statement" na kuchota akili za watu ili wakupigie kura uwe raisi? Ni change gani unapoajiri karibu robo tatu nzima ya timu yako kutoka katika utawala wa raisi mstaafu? Is that change we can believe in?
   
 16. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #16
  Nov 18, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Swali lako limekaa too simplistic  lakini kwa sababu swali lako lenyewe limekaa kiform two, two nadhani walengwa wako ambao inaeleka walilijibu hilo swali ha history la FORM 2 watakujibu unavyotaka
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Nov 18, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Weka la kwako la levo ya mastaz basi.....
   
 18. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #18
  Nov 18, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  ahhh unajua JF kwa sasa should be different from other forums bwana weee


  swali kama hilo ukiliona kwenye forums za IPPMEDIA au kule TANZANIA DAIMA au kule kwingine sawa


  sasa hebu niambie wachambuzi kama akina ES na wengineo watajibu hilo swali la FORM 2?
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Nov 18, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Sasa wewe unatafuta ugomvi.....mie simo na mchanga wa pwani huo.....Lol
   
 20. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #20
  Nov 18, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Chmooooooowa!
   
Loading...