Endapo CHADEMA itawazuia Wabunge wa Viti Maalumu kwenda Bungeni hautakuwa ni unyanyasaji wa kijinsia?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,852
141,787
Nauliza tu kwa wale wabobezi wa masuala ya Haki za Binadamu kama itakuwa ni halali kwa viongozi wa CHADEMA kuwazuia Wabunge wake wa Viti Maalumu ( Wanawake) kwenda kuapishwa na kushiriki vikao vya Bunge.

Iwapo CHADEMA itakuwa imepata 5% ya kura za jumla walizopigiwa wabunge wote basi wata-qualify kupata uwakilishi wa Viti Maalumu Bungeni na kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi Mwenyekiti wa Bawacha Halima Mdee atakuwa miongoni mwa wabunge hao.

Maendeleo hayana vyama!
 
Maamuzi yamefanywa bila kuwashirikisha wanawake. Ni unyanyasaji wa kijinsia wa hali ya juu.

Viti maalum inastahili wanawake wachaguane wenyewe kwa vigezo walivyowekeana wenyewe bila kuingiliwa.

Uamuzi wa kushiriki Bunge unatakiwa ufanywe na wanawake wenyewe.
 
Nimekuelewa mkuu!
 
CDM itakuwa haijatenda haki pia watakuwa wamevunja Sheria za viti maalumu. Pia wanaume waache ubinafsi wakishinda wao ni sawa ikifika wanawake tu hawataki, so naona hapo Kuna gender discrimination flani
 
Back
Top Bottom