Enaboishu Secondary School mpo? Tujadiliane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enaboishu Secondary School mpo? Tujadiliane

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Sipo, Jul 11, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tukumbushane ya muhimu
   
  Last edited: Sep 30, 2009
 2. s

  scorpiomama New Member

  #2
  Jul 12, 2009
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tupo! 1987 - 1989 bwenini tukiwa matron bibi, mzee mashauri! mwal ndossi mchungaji sasa natumai, mwal Letara,
   
 3. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nawakumbuka mademu wazuri wa Enaboishu, wakati tunatoroka Ilboru kwenda kutuliza kiu kidogo baada ya kupiga book kali kwa mzee Kitemango.
   
 4. n

  naamnani New Member

  #4
  Jul 13, 2009
  Joined: Oct 27, 2007
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  class of '80-'83. mmmh! hebu nikumbuke jinsi lile zogo la foleni za kande (lunch) pale jikoni na mzee 'kijicho' na fimbo kuhakikisha hakuna anaerudia au kula 'anti-log' kupata kande.... ooops nimesahau na ile kazi ya kubeba mawe toka mtoni hadi mabweni (ya wasichana) wakati huo ndio yalikuwa yanajengwa.
   
 5. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ina maana humu ndani jamvini products za Enaboishu ni chache sana au?
   
 6. n

  naamnani New Member

  #6
  Sep 22, 2009
  Joined: Oct 27, 2007
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sipo (au Upo...)

  acha utani.. hivi unafikiria zile div isiokuwa namba ya kuhesabia (sifuri) zilivyokuwa nyingi unafikiria mwisho wake ni nini...

  mie mwaka wangu '83. div 1 = 2, div 2 < 10 (i blv 7), div 3 < 22 (nafikiri ni namba sahihi), div 4 sikumbuki (plenty) na div 0 > 40 kati ya (mkondo a-d) wanafunzi 152 tuliofanya mtihani wa baraza.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ehhh, hii shule naikumbuka wakati nipo TCA na kina marehemu Method Mogella. Tulikuwa hata kwenye michezo hatukutani kwani mlikuwa watoto wadogo saana kimichezo. Hivi ilikuwa mitaa gani pale Arusha? Nilikuwa naisikia tu. Ilboru wakajinyua wakaja pale chuoni tukawachapa goli hadi wakaona aibu.

  Hata hivyo nawasifu kwa ujasiri wa kuja kucheza na sisi.
   
 8. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Iko maeneo ya Sanawari karibia na mahakama ya Mwanzo Enaboishu kando kando ya mto Themi.
  Ni kweli pamoja na kuwa timu yetu ya football haikuwa imara sana lakini bado tuliweza kuwatoa jasho timu pinzani, nadhani hata nyie pia tuliwahi kuwafunga game moja.
  Ilboru wanafahamika kwa utemi wao kwenye kuongea na sio kwenye vitendo hata sisi tuliwahi kuwafunga wakanywea kama fisi maji.
  By the way umenikumbusha mchezji niliyempenda sana marehemu Method Mogella. Tunakukumbuka daima
   
 9. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ulichosema kina usahihi husiopingika ila kwa sasa shule imebadilika nafikiri baada ya Advanced Level kuanzishwa walioko Ordinary Level wamekuwa wanapata changamoto kubwa kusoma na kuondoa ile aibu ya kupata division four zisizohesabika. Pia kitendo cha kufanya mchujo wakati wa kuingia kidato cha tatu na nne umesaidia wanafunzi kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
  Ila nilitegemea kuwa wanafunzi wengi wa Enaboishu wangejitokeza kuchangia mada hii lakini naona wamejitokeza wachache sana na wengine ni kutoka shule na vyuo vingine.
   
 10. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mhe kweli wewe wa long time pale kama kipindi hicho ndio yalikuwa yanajengwa mabweni ya wasichana. Unastahili shikamoo kutoka kwangu "SHIKAMOO"
   
 11. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Waauh!! Nice eperience from ScorpioMama, hawa wote sijawakuta pale kipindi nilichosoma ila nimependa kujua haya yote please tuendelee kukumbushana mengi kuhusu shule yetu hii yaliyopita ni dhahabu jama
   
 12. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Eti Mganga wa Jadi, how do you feel now? Unaweza kumshauri mwanao au mdogo wako aende kutuliza kiu kwa style ambayo ulikuwa unatumia wewe? Do you think its conducive? Nahitaji majibu yako pindi ukipita hapa ili tuache kuwapotosha wadogo na watoto wetu
   
 13. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Mkuu Sipo

  wanafunzi wa Enaboishu tuko wengi sana hapa jamvini sema wengi hawataki kujitokeza kwasababu wanazozijua wenyewe.

  Juzi nilikutana na Mwl Letara siku hizi ni mchungaji wa KKKT anatesa na L/Cruiser Hard top ya kanisa.Mwl Mbaga ni Financial manager Leopard Tours,Mwl Losaro ni Mwl mkuu wa Kimandolu secondary na Mwl Okonkwo (mwl wa Kiingereza)sikumbuki jina lake halisi ni marehemu.

  Wanafunzi wengi wa Enaboishu wa miaka yetu wameshatangulia mbele ya haki hasa wale waliokimbilia Mbuguni mara baada ya kumaliza shule na wengi hawakungoja hata kumaliza shule.
   
 14. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu nashukuru kama nawe ni mmoja wapo, wangejitokeza wengi ingekuwa safi sana.
  Nashukuru kwa kunifahamisha kuhusu Mchungaji Letara anaishi maeneo ya karibu na Ngulelo nilikuwa sijui kama alishawahi kuwa mwalimu wa Enaboishu.
  Mwalimu Losaru sasa ni mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Ekenywa, nasikia ameibadilisha sana ile shule tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
  Thanks alot Sir
   
 15. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MWENYENZI MUNGU azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amen
   
 16. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hili la wanafunzi wengi wa shule mkoani Arusha kukimbilia migodini hasa uko Mbughuni (Mererani) ndio tatizo kubwa sana na linapelekea wengi kutokumaliza elimu zao kwenye ngazi tofauti. Ila nafikiri sasa hali itakuwa imebadilika ingawa nina muda sijafuatilia kuhusu suala hili
   
 17. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Mkuu Sipo

  Siku hizi shule imebadilika sana ukilinganisha na wakati wetu.
  Kuanzishwa A level kumesaidia sana wanafunzi wa O Level kufanya vizuri.Wakati wetu wanafunzi wa kike wengi walikuwa wanatoka DSM na mikoa ya mbali siku hizi wanatoka hapa hapa mkoani Arusha na Kilimamnjaro.

  Hali ya migodi Mererani si nzuri kwa sasa madini yanapatikana kwa shida sana.Makampuni ya wazungu ndiyo yameweza kubakia katika biashara.Wamasaai nao wameshakiambia Mererani wamejaa tele maeneo ya Arusha by night (St Thomas) .Wazawa siku hizi hawachimbi mawe wamebaki madalali.Biashara ya udalali imetawaliwa na wamasai na wajaluo siku hizi.
   
 18. K

  Kudi Shauri Senior Member

  #18
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 1, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi hii shule bado ipo? Nakumbuka 1971 nilifundisha hapa temporarily. Waalimu ninao wakumbuka ni headmaster Mr. Nkini; Mwalimu wa Hesabu Mr. Tilya; School Clerk Mr. Mngure. Baadhi ya wanafunzi ninao wakumbuka ni Eric Mziray - last time I met him he was a Night Club Manager in Arusha; Mwanaidi Saidi and several of the Mfinanga sisters; and two brothers who I forget their names but I believe they joined the army in 1973. Enaboishu was ceratainly one of the pioneering private secondary schools of the 1970s.
   
 19. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mhe. hii shule bado ipo na kama umesoma hapo juu imeshakuwa na Advanced Level toka mwaka 1999. Pia imetanuka kwa kuwa na mabweni ya wavulana kwani hapo mwanzo ilikuwa na ya wasichana pekee.
   
 20. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu wachimbaji wa kigeni kwa kiasi fulani wamewafukuza wachimbaji wa asili kwenye machimbo ya Mererani maarufu kama Mbughuni kwa mkoani Arusha. Lakini ukienda Arusha na kuwauliza vijana wengi kuhusiana na Mererani watawalalamikia sana AFGEM kuwa wamewaharibia maisha yao kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwabana na hata kuwasababishia ulemavu wa kudumu pale wanapohisiwa au kugundulika kuwa wametoka na madini kwenye migodi. Lakini cha ajabu huwa wanawashangaa hata polisi wetu ambao wamekuwa hawachukui action yoyote kutokana na either kuhongwa au masuala mengine ya influence kutoka kwa viongzi wa juu wenye mahusiano na viongozi wa AFGEM. Kipindi cha nyuma vijana wa Arusha walikuwa na maisha mazuri sana kabla ya hili wimbi la uwekezaji na wawekezaji.
   
Loading...