'Empowerment of Women' kama 'Matusi' kwa Wanawake.

hovyohovyo

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
547
157
Naomba maoni yenu wanajamii.

Kuna jambo limekuwa likinikera na kunifikirisha sana. Jambo lenyewe ni hii dhana ya kuwawezesha wanawake, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kunakuwepo na uwiano unaoridhisha ktk nafasi za kiuongozi nk. Wakati nakubaliana na dhana nzima, sikubaliani na namna mafanikio yake yanavyoelezwa na zaidi namna inavyotafsiriwa na wakuu hasa viongozi wenye mamlaka ya uteuzi. Ninaposema mamlaka za uteuzi, nakusudia mamlaka zote, hata iwe mwalimu mkuu anapotakiwa kuteua mwalimu ktk nafasi fulani, mpaka ngazi za juu kabisa za nchi. Kuna makundi mawili yanajitokeza: Kuna wanawake wanateuliwa kwa misingi ya umahiri wao na si kwa sababu ya kusawazisha pengo. Hawa wamekuwa mfano mzuri wa empowerment. Kundi la pili ni wale ambao wanapata hizo nafasi kutokana na sababu zingine zikiwemo na za kingono. Baaadhi yao wanajitutumua kiasi, baadhi wanachemsha kabisa.
Hao wote wamekuwa wakihesabiwa kama sehemu ya empowerment. Swali: Je hatuoni kwamba hawa wanaharibu dhana nzima ya empowerment? Je, serikali inapotumia takwimu zinazowajumulisha hao ktk kujitangazia mafanikio, hatuoni kwamba ni matusi kwa wanawake? Nini mchango wa makundi mengine ya wanawake ktk kuliongelea hili jambo?-badala ya kufurahia takwimu tu?

Wasalaam
 
Back
Top Bottom