Employee Share Option Plan-Mfumo wa malipo kupitia Haki za Umiliki(HISA)

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,529
Habari za wakati huu;

Katika kufanya kazi na wajasiriamli wengi huwa nakutana na wale ambao huwa wanatafuta Mbia(Partners) kwa sababu mbalimbali ikiwamo mahitaji ya mtaji,ujuzi,connnection etc.Wengi wao huwa wanjua nini wanataka na suluhu yake ni nini ili wanakuwa hawajui namna bora ya kushughulikia swala hili.

Katika biashara na ujasiriamali huwa kuna kitu kinaitwa,EMPLOYEES SHARE OPTION PLAN au kwa majina tofauti ambapo ni mfumo unampa mwajiriwa uwezo au haki ya kuwa sehemu ya umiliki wa kampuni baada ya kufanya kazi kwa kipindi fulani kulingana na mkataba an malengo ya kampuni.Mfumo huu unalenga kuhakikisha kwamba mwajiriwa anweka maslahi ya kampuni mbele..

Kwa mfano leo hii unaweza kuanzisha kampuni kwa mtaji wa milioni kumi,ila kwa malengo na mipango uantaraji kampuni iwe na thamani ya milioni 100 baada ya miaka kumi.Ili uweze kufikia malengo hayo unahitaji aina fulani ya utaalamu na fursa ambazo unaweza kupata kutoka kwa wafanyakazi wako.Katika hili unaweza kuamua kuwapa wafanyakazi wako nafasi ya kuwa sehemu ya wamiliki ka tima mfumo huu wa ESOP.

Faida za ESOP ni kwamba inawapa HAMASA wafanyakazi na kuwafanya wawe loyal.Lakini pia ni namna bora zaidi ya kuhakikisha kwamba kampuni yako inapokuwa kuwa inakuwa na Hazina ya utaalamu na ujuzi kwa kuretain timu BORA.

Swali la kujiuliza leo ni JE sheria za nchi yetu zinasemaje kuhusu ESOP?Je wamiliki wanaonaje iwapo watawapa wafanyakazi nafasi ya kununua hisa za kampuni kwa masharti nafuu?

Je njia inaweza kuwa chachu ya maendeleo na kukua kwa makampuni na biashara hapa nchini?

TUJADILI
 
Back
Top Bottom