Emmanuel Mbaga wa Mbaga Real Estate Agency ANAHITAJI KUPELEKWA SHULE YA CUSTOMER CARE

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Kuna kijana mdogo anamiliki kampuni ya udalali wa nyumba na viwanja, inaitwa Mbaga Real Estate Agency. Yeye mwenyewe anaitwa Emmanuel.

Nilipewa jina lake na rafiki yangu fulani. Nikampigia na kumwambia kuna biashara ya kiwanja kinauzwa, tena mahali penyewe ni pa bei mbaya.

Tukakubaliana, kimsingi, kwamba tungekutana njiani, mahali ambapo ningemsubiri, kisha tungefuatana mpaka kwa mmiliki wa kiwanja, aliyenituma kazi hiyo.

Jamani, hii ni biashara. MIMI ndiye niliyempigia, kumpelekea biashara; kiwanja hiki, uza, upate commission yako, ukifanikiwa na mimi utanipa kitu kidogo. MIMI ndiye niliyemtafuta, kumpelekea biashara.

Wakati niko njiani kwenda kwenye sehemu ya ahadi, nikampigia tena. Nanukuu alichonijibu:

"Sikiliza bwana mdogo, sisi ni real estate agency, hatuna wakati wa kukusubiri wewe umalize shughuli zako mia moja. Ukishamaliza, tupigie, tutakuambia tuko wapi, utatufuata!"

Nikamwambia: Sawa.

Nikakata simu.

Nikaona hii imeshakuwa soo. Kwanza mimi si BWANA MDOGO. Ni mtu mzima mwenye ndevu zangu, familia na watoto. Nimetumwa nimpelekee biashara hiyo na mtu ambaye NINAMHESHIMU SANA, TENA MNO! Sio kawaida yangu kutafuta DEAL za viwanja, n.k. Nina shughuli zangu rasmi. Huyu kijana aniite mie BWANA MDOGO? EBOOOO!

Alinipigia tena baada ya nusu saa, nikamwambia BADO SIJAMALIZA! Nadhani aligundua kosa lake, inaonekana walikuwa kwenye ulabu, kwani leo ni Ijumaa, na vijana HUANZA MAPEMA masuala ya ulabu siku za wikiendi.

Ndio tatizo la vijana. Wakipata vijisenti, wanachofikiria ni pombe na starehe (soma NGONO). Hakuna kupanga mambo ya maana!

Nimemtafuta mtu mwingine, mtu mzima, anayefanya kazi hiyo kama PROFESSION, sio HOBBY! Nitakamilisha biashara.

Emmanuel, YOU NEED TO GO TO CUSTOMER SERVICE SCHOOL! YOU REALLY SUCK!
 
Hovyooooooooooo!!
 
Lakini mkuu kwani kumuanzishia thread humu ndiyo itamfundisha nini? Au you are hoping mtu anayemfahamu ataisoma na kwenda kumtaarifu? Nadhani uli takiwa kumpa ukweli pale pale kwenye simu kwa sababu ulisha amua kuhamishia biashara yako pengine. But nakubaliana na wewe. Mtu aki pata pesa kidogo tu huchanganyikiwa. "Masikini akipata.....
 
Nakusaidia kumalizia "..............hulia mbwata" Vijana wakipata vijisenti akili kuwaruka hata kabla ya kuanza kunyoa!!
 
Watu mnagombana uswazi kwene mishemishe zenu mnakuja kufungua thread JF...naona hii ni spirit mpya ya JF.
 
Pole sana this is bongofalav generation so be careful........bahati yako hujaingizwa mjini
 
Watu mnagombana uswazi kwene mishemishe zenu mnakuja kufungua thread JF...naona hii ni spirit mpya ya JF.
lakini kafanya vema kuileta hapa hiyo thread,kwasababu amewatahadharisha pia wengine wanaoweza kumtafuta huyu mtu kwa masuala kama hayo.
 
Kwani Mbaga kafanyaje? Kaiba? mtu kama unashindana naye kwene practices na discipline za biashara si unaachana naye tu? Uswahili at best huu.
 
Tunamdiskasi mtu hapa. hatudiskasi tabia i presume.
Mwanahaki if I may ask. Is that a message you intend to place it here? Maana mtu mwenyewe sidhani kama ana muda wa kuja hapa na kuwa shocked kwa umaarufu wa ghafla alioupata hapa.

Cha msingi piga chini au vumilia umalizane naye kisha ignore him big time.

Conclusion yako imekaa kimpasho zaidi ya kujadili au kupiga vita tabia.
 
Watu mnagombana uswazi kwene mishemishe zenu mnakuja kufungua thread JF...naona hii ni spirit mpya ya JF.

Thread ilikuwa nzuri kama ingetolewa kama fundisho kwa wafanya biashara vijana wote. Nadhani kosa lililotokea hapa ni kuwa amei-personalize sana kuwa ni kati yake na Mbaga tu, ambavyo alitakiwa atumie hiyo experience yake na Mbaga kama mfano tu.

Nimeshaona vijana wadogo wakishapata misheni ya pesa basi wanakuwa na kiburi hata na kwa wateja wao wanaoingizia pesa. Nadhani kosa kubwa ni lugha ya kistaarabu ndiyo watanzania wengi tunakosa. Juzi nilisoma barua iliyotumwa kwa Bashe kumwomba asaidie CCM kwenye kampeini za ubunge nzega, lakini mwandishi wa barua ile aliandika kama vile anamwamrisha Bashe badala ya kumwomba.
 
Nafkiri aliyeleta hii thread hana makosa yoyote!... ameiweka ili wadau wamjue huyu bwana MBAGA NI MTU WA AINA GANI!?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom