Emmanuel Buhohela: Hatuna taarifa rasmi kuwa Uingereza ilipiga marufuku wasafiri kutoka nchini Tanzania kuingia nchini humo

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,493
2,000
Mkurugenzi wa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje, Emmanuel Buhohela, amesema wao hawana taarifa rasmi kwamba Uingereza imepiga marufuku wasafiri kutoka nchini Tanzania kuingia nchini humo na kueleza kuwa hayo ni mambo ya mitandaoni na wao hawayafuatilii.

Chanzo cha Taarifa: EastAfricaTV

==========

Mkurugenzi wa Habari Wizara ya Mambo ya Nje, Emmanuel Buhohela, amesema kuwa wao hawana taarifa rasmi kwamba Uingereza imepiga marufuku wasafiri kutoka nchini Tanzania kuingia nchini humo na kueleza kuwa hayo ni mambo ya mitandaoni na wao hawayafuatilii.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 23, 2021, wakati akizungumza na EATV&East Africa Radio, na kuongeza kuwa serikali inao utaratibu maalum wa kupokea taarifa hizo za namna hiyo na kwamba ingekuwa vyema zaidi kama Ubalozi wa Uingereza ungeulizwa kama hiyo kauli ni ya kwao.

"Utaratibu wa serikali ni kwamba kuna utaratibu wa kuwasiliana, kwahiyo hayo mambo ya kwenye mitandao hatuwezi kuyazungumzia, mimi binafsi nimeiona kama wewe ulivyoiona, serikali haiwasiliani kwenye mitandao bali ina utaratibu wake", amesema Buhohela

Aidha Buhohela ameongeza kuwa, "Kwenye mitandao mambo mangapi ya uongo yanayoandikwa, kama tukipata maandishi au document kutoka Uingereza tutalizungumzia, au mngewapigia Ubalozi wa Uingereza kuwauliza kama hiyo kauli ni ya kwao"

Katibu Mkuu wa Uchukuzi wa Uingereza Grant Shapps, kupitia ukurasa wake wa Twitter, aliandika kwamba zuio la wasafiri kutoka Tanzania na DR Congo, limeanza jana Ijumaa Januari 22, 2021, ikiwa ni hatua za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19, kufuatia kuibuka kwa kirusi kipya cha ugonjwa huo nchini Afrika Kusini
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,377
2,000
Kwa Cheo / Wadhifa wake hapaswi kusema kwamba hatujapata taarifa rasmi, anapaswa kusema kweli / si kweli au kwanini hizi habari zimetokea au zimetokea wapi na kwanini...

Majibu rahisi kwa maswali magumu hayatakiwi hususan kwa mtu mwenye majukumu kama yake
 

Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
1,835
2,000
Tena wafikirie, mbona Afrika Kusini yenywe chanzo cha hiyo aina mpya ya covid hawakuipiga marufuku?
Kwa wenye maono, tatizo linakwenda ndani sana.
Lakini watakwambia: hatuna haja ya kwenda Uingereza!
Wamepigwa marufuku na nchi zote za SADC. Fuatilia vizuri . Au kuna mpya zingine ?.
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,063
2,000
Wamepigwa marufuku na nchi zote za SADC. Fuatilia vizuri . Au kuna mpya zingine ?.
Safi sana umemjibu vema kabisa south Africa ilikuwa nchi ya kwanza raia wake kuzuiliwa kuingia UK,tatizo kubwa hawa middle class wetu ni manyumbu mno na mpaka wanakera.
 

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
296
500
Ni kweli kwamba serikali haifanyii kazi taarifa za kidiplomasia kupitia mitandaoni.

Serikali inayo ofisi katika wizara ya mambo ya nje ambayo inahusika na masuala kama haya yanayohusu mahusiano ya kidiplomasia.

Pia tunaye mwakilishi wetu katika ubalozi wa nchi yetu huko uingereza.

Pia tunaye balozi wa uingereza hapa nchini ambaye ana iwakilisha nchi hiyo hapa kwetu.
Hivyo vyote ni vitengo mahususi katika upeanaji taarifa nyeti kama hizo kiserikali.

Mitandaoni sio mahali pake.
Jiulize swali dogo....je serkali yetu nayo ikijibu kupitia MITANADAONI.
Ina maana tuanzishe mipasho kwenye mitandao?
Je nini itakuwa umuhimi wa ubalozi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom