Emirates yanunua ndege 40

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,497

Boeng imeanzisha maonyesho yake ya ndege huko Dubai kwa kutangaa mauzo makubwa mapya katika maonyesho hayo ya siku tano.

Ilitangaza kuwa Shirika la ndege la UAE la Emirates limeagiza ndege 40 za Boeng 787 Dreamliners, katika mkataba wa thamani ya dola bilioni 15.

Emirates kupunguza safari za Marekani

Mwenyeki wa shirika hilo Sheikh Ahmed bin Saeed al-Maktoum, amesema kuwa Boeng imechaguliwa badala ya Airbus A350.

Alikuwa ametarajiwa kutoa tangazo kubwa la kuagiza ndege za Airbus A380 superjumbo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari.

Airbus inahitajia ndege zake za A380 kuagizwa zaidii zikiwa ndizo ndege kubwa zinazotumika kwa sasa.

Emirates ndilo shirika la ndege kubwa zaidi mashariki ya kati likiwa mnunuzi mkubwa zaid ya Boeng 777 na lina ndege 165 zinazohudumu likiwa tena limeagiza ndege 164.


Muungwana
 
mbona tunaweza isipokua hatujaamua tu cc ni "donor county" kwa tariifa yako
Hahahaha hizo zilikuwa initial stories now tunaomba na kukopa kuliko wakati wowote wa awamu yoyote.
Kila anayetutembelea lazima apigwe rungu siku hizi hatuwafuati tunawasubiri hapa hapa
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hahahaha hizo zilikuwa initial stories now tunaomba na kukopa kuliko wakati wowote wa awamu yoyote.
Kila anayetutembelea lazima apigwe rungu siku hizi hatuwafuati tunawasubiri hapa hapa
Hahahaha tuna hazina ya rasirimari za kutosha tunapita nchi ya ureno hisipania uguriki. sasa tumeanza na SGR na flyover tatizo lilikua wapiga dili..tumesha wakomesha Sasa nimaendeleo kwenda mbele
 
Inamaana biashara ya ndege inalipa sana endapo ukipata managment inayo eleweka... ATCL awekwe hapo juu mwarabu wa Dubai aendeshe hili shirika

kipindi cha nyuma Iran waliweka order ya ndege 100 za Boing sijui ilikuja kuishia wapi.... hii dunia kuna nchi zenye hela....

Yote hii ni kiburi ya Mafuta, sijui yetu yatachimbwa lini
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hahahaha tuna hazina ya rasirimari za kutosha tunapita nchi ya ureno hisipania uguriki. sasa tumeanza na SGR na flyover tatizo lilikua wapiga dili..tumesha wakomesha Sasa nimaendeleo kwenda mbele
Umesikia lakini mkata wa mkopo wa SGR kuwa jk aliacha ameandaa mkopo wakulipwa kwa miaka 20 kwa interest ya 1%.
Wakati huyu kachukua wakulipa ndani ya miaka 5 kwa 7% na kila material inatoka nje hata kokoto wata deal nazo wao.
That is according to zitto.
Any way
 
Ila kiukweli binafsi nazipenda zaidi airbus kuliko boeing. They are less noisy and more comfortable. Hata takeoff na landing za airbus zimetulia mno; so smooth badala ya kugonga tairi chini had unahisi inavunjika. Hata kwenye tufani kali airbus are so smooth. Nazungumzia economy huko business hope ni pepo.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Umesikia lakini mkata wa mkopo wa SGR kuwa jk aliacha ameandaa mkopo wakulipwa kwa miaka 20 kwa interest ya 1%.
Wakati huyu kachukua wakulipa ndani ya miaka 5 kwa 7% na kila material inatoka nje hata kokoto wata deal nazo wao.
That is according to zitto.
Any way
Duh!!!!! Ilatutamshauri anapokeaga ushauri wa watu nakuufanyia kazi haraka huo mkataba tutaubadirisha kama alivo fanya na Acasia ya dhahabu tunapata 50/ 50 kwasasa
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Duh!!!!! Ilatutamshauri anapokeaga ushauri wa watu nakuufanyia kazi haraka huo mkataba tutaubadirisha kama alivo fanya na Acasia ya dhahabu tunapata 50/ 50 kwasasa
Yote kheri maendeleo yako na familia yako utayaleta mwenyewe siyo wao
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Usafiri wa anga ndio usafiri unaopendwa na kuaminiwa sana duniani na itachukua miaka mingi sana kutokea usafiri ambao unaweza kupindua fikra za watu juu ya usafiri wa anga rabda miaka 150 ijayo ndio kuna uwezekano wa kuwepo usafiri utakao tishia ushafiri wa anga na usafiri huo ni Hyperloop ambao utakuwa na speed sana zaidi ya ndege lakini itachukua miaka mingi sana mpaka kuconnect dunia kama ilivyo kwa ndege. Kuna mashirika zaidi ya 2000 duniani yanayo operate zaidi ya ndege 23,000 kwenye viwanja vya ndege zaidi ya 3,700 Duniani mpaka kufikia mwaka 2006 kulikuwa na zaidi ya safari milion 72 zilizobeba zaidi ya abiria bilion 2.3 kwa mujibu wa International Air Transport Association (IATA)

Ukuaji wa biashara hii imekuwa ikikua kwa kiwango cha 5% kila mwaka kwa kipindi cha miaka 30 mfululizo na inasadikika pato la safari za anga linaweza kukua mpaka mara mbili kwa kipindi cha mika 10-15 ijayo kwa Marekani pekee mashirika 100 ya ndege yanafanya zaidi ya safari milion 11 kwa mwaka na kubeba zaidi ya abiria 745 milion na zaidi ya watu 545,000 wamepata ajira kwenye ndege 8000 zinazofanya safari 31,000 kwa siku , kumbuka Marekani ndio nchi inayoongoza kwa raia wake kutumia sana usafiri wa ndege ikifatiwa na China na UK pato la Biashara hii ya anga kwa mwaka ni zaidi ya$ 1.2 Tillion

United Arab Emirates na Qatar nchi ambazo kwa pamoja zina eneo la ukubwa wa square kilometres 78,926 ndani ya nchi hizo kuna mashirika makubwa matatu ya ndege Qatar Airways,Emirates Airlines na Etihad Airways mashirika haya ukiangalia yameanza miaka ya 1985,1993 na 2003 lakini yamekuwa ni tishio kwa mashirika ya ndege Duniani na wao kutawala Anga la Dunia ktk Usafiri wa Anga


Mashirika haya unaweza sema hayajiendeshi kibiashara kwani kila mwaka serikali inapump mabilion ya dola kwenye mashirika haya kununua ndege za kisasa zaidi ya dola billion 50 zimetumika na mashirika haya kujijenga kutoka serikali zao si kwa mtaji wa mshirika au faida wa kampuni kitendo ambacho kinaondoa ushindani ktk usafiri wa anga kwa mashirika mengine yanayojiendesha yenyewe kwa pato la shirika pia mashirika haya pamoja na kuwa na madege ya kisasa bado yanauza ticket kwa bei ndogo si ya kisoko kitendo ambacho hakuna shirika lolote Duniani litakaloweza kupambana na mshirika hayo na mwisho wa siku Anga la Dunia katika usafiri wa anga litakuwa chini yao kama walivyoteka Anga la Europe,Asia,Africa na wanakwenda kuteka na US muda c mrefu kwani mpaka sasa order za ndege mpya kwa makampuni haya matatu yani order za kutengenezewa ndege mpya kutoka Boeing na Airbus ni 539 yani Emirates 222, Qatar 169 na Etihad ni 148 huku order za ndege mpya za makampuni yote ya US ni 159 na order zote za ndege mpya za makampuni ya China ni 76 so unaweza kuona soon waarabu wanatawala anga la Dunia
 
Back
Top Bottom