Eminem ndiye rapper bora kuwahi kutokea, kikwazo ni rangi

Hakuna kigezo kimoja kumfanya mtu kuwa Goat ila unaweza angalia wiki ya Hip hop hapa kuna rank ya site mbalimbali na vigezo mbalimbali

Then kwenye reference Kuna links husika walipotoa.
Mkuu sijaona vigezo humo....
Nimeona namba tu, na nihisia za waandishi tu kama hawatoi vigezo...
Nadhani tupeane vigezo hapa wote tuthibitishe.
 
Siwezi kuongea kwa niaba ya watu wenye asili ya africa wote wanaopenda hip hop, wawe wabongo, wamarekani weusi, waingereza , n.k, lakini wacha nitoe maoni yangu, Eminem is the goat (great of all time), hata uweke big na 2pac bado sana.

Kwangu mimi hali ni tofauti, huwa sijali rangi, nachojali ni lyrics, delivery, word play, nk, na hapa ndipo napojua hakuna msanii wa kumfikia eminem kukitendea miujiza kipaza sauti na kutumia kalamu vizuri kuandaa mlyrics amazing.

Sote tunajua hip hop ilitengenezwa na kuchochewa na watu weusi, na hapa ndipo kuna baadhi ya watu wenye hii asili wanakuwa wagumu mno kukubali uhalisia kwamba Eminem ni mzungu na anafanya poa zaidi ya rappers weusi, hisia zinatumika kupinga badala ya kutumia akili kukubali ukweli.

Laiti Eminem angekuwa ni mweusi, basi ni wazi kabisa eminem angechukua ni Michael Jackson wa Hip hop

Ukija huku kwenye mitindo huru frreestyles na cyphers, ni mnyama .

Waliowahi kuingia 18 zake wengi walipotezwa, pengine cheo sahihi cha kumpa Eminem ni "Un-beefwithable"
Sema kwa maoni yako
 
Mkuu unajua Auto tune? Eminem ametoka kizazi feki na ile sio sauti yake ukimuweka live hawezi kurap vile anatumia sauti fake (Auto tune, distortion, overlap etc) ndio maana hawi regarded kama mwana Hiphop bora.

Kina rakim, 2pac, Nas, B.i.g Jay Z etc wanakuwa regarded kama bora zaidi.
Muelimishe mjinga huyo
 
Mimi nimezaliwa kizazi cha Em lakini kumlinganisha na PAC ni kukosa adabu

Jela ikuhusu tena uchapwe mboko 6 wakati wa kuingia na 6 wakati wa kutoka
 
Mkuu sijaona vigezo humo....
Nimeona namba tu, na nihisia za waandishi tu kama hawatoi vigezo...
Nadhani tupeane vigezo hapa wote tuthibitishe.
Hata vigezo vitakuja on personal opinion vilevile.

Mfano nikitaka kum favor Eminem naweza Weka vigezo kama beats (zimekuwa improved Na technology), mafanikio na vigezo vyengine vitokanavyo na recency bias.

Wewe unaona vigezo gani vinafaa?
 
Beats......technology inamfavor? Si kweli.....
Uzuri ameimba katika era ya low tech pia.
Vipo vingi sana, naomba tuanze na freestyle....
Vingine vitafuatia.
 
Beats......technology inamfavor? Si kweli.....
Uzuri ameimba katika era ya low tech pia.
Vipo vingi sana, naomba tuanze na freestyle....
Vingine vitafuatia.
Umeona? Na mimi naweza sema Tuanze na Lyric, Eminem amachojua kuimba ni introspective tu, anachofeel yeye, kujisifia etc nyimbo zake maarufu zina fall kwenye category Hio ya personal level.

Malegend wengine kama Nas unakuta wanacover kila kitu Siasa, Gangster life, maisha ya kisela, na maisha mengine ya kihalifu ambayo huzunguka jamii zao.
 
Ata ukitaka lyric sawa tu....yupo vizuri.
Ko tumekubaliana hakuna anayemzidi freestyle...?
 
Ata ukitaka lyric sawa tu....yupo vizuri.
Ko tumekubaliana hakuna anayemzidi freestyle...?
Hizi.....ni kwenye album ya Revival tu....
Part alizojikita kwenye siasa ( kwa mujibu wa billboard)
 
Hizi.....ni kwenye album ya Revival tu....
Part alizojikita kwenye siasa ( kwa mujibu wa billboard)
Nimesoma hizo verse mkuu, zinarudi pale pale kussuport point yangu, si nyimbo za siasa bali ni vionjo tu, mfano Fid Q leo aimbe akiwaponda watu wa CCM na Chadema kwenye verse mistari kadhaa ni kawaida tu, huwezi sema ni nyimbo ya kimapinduzi kama Hih hop zenyewe za asili ila Akitoa nyimbo akazungumzia Issue kabisa kwenye jamii direct kama anavyofanya Roma basi hapo kunakuwa na mahusiano direct ya kisiasa. Ama hapo Eminem akim diss trump hio ni dis kama dis nyengine.

Mifano ya Hip hop za kisiasa ni kama Police state, untitled, changes etc.

Hebu sikiliza changes ya 2pac, the way inavyogusa jamii.

Then taja nyimbo kali za Eminem then angalia theme ya nyimbo utaona theme zake zote zinavyofanana.
 
Ukiangalia Technicality(rhyme schemes, wordplay, cadence) Eminem Ni goat lakini hiphop is more than just words twisted in a cool way to make rhymes.

Kuna mambo mengi kama impact,significance and relevance
Hapo ndo wenzake kina big PAC jayZ Kendrick hata jcole wanamzidi .

And btw Eminem anapewa shavu Sana hata Na black Americans Na nahisi akitoka drake hamna rapper anayemfikia Eminem Kwa numbers
 
Kwangu Mimi best emcee to ever touch the mic Ni kendrick Lamar huyu jamaa ana Kila kitu technicality+ impact.
Eminem Hana Ngoma inayoifikia the blacker the berry
Hana story inayoifikia sing about me,how much a dollar cost,Duckworth etc.
Eminem Hana album inayoifikia GKMC,TPAB
 
Nimesoma hizo verse mkuu, zinarudi pale pale kussuport point yangu, si nyimbo za siasa bali ni vionjo tu, mfano Fid Q leo aimbe akiwaponda watu wa CCM na Chadema kwenye verse mistari kadhaa ni kawaida tu, huwezi sema ni nyimbo ya kimapinduzi kama Hih hop zenyewe za asili ila Akitoa nyimbo akazungumzia Issue kabisa kwenye jamii direct kama anavyofanya Roma basi hapo kunakuwa na mahusiano direct ya kisiasa. Ama hapo Eminem akim diss trump hio ni dis kama dis nyengine.

Mifano ya Hip hop za kisiasa ni kama Police state, untitled, changes etc.

Hebu sikiliza changes ya 2pac, the way inavyogusa jamii.

Then taja nyimbo kali za Eminem then angalia theme ya nyimbo utaona theme zake zote zinavyofanana.
Kumbuka hiyo ni Album ya revival tu ambayo ni ya karibuni......
Na nimeweka hivyo kuonesha, anacover siasa pia.....
Na huku ndiko kumempa huu ukubwa, anacover kila kitu.
Na si kweli kwamba part yake kubwa ni majigambo ( kujizungumzia yeye zaidi).
 
Pia kuna freestyle alifanya ya Donald Trump kulingana na point of view yake

View attachment 1972806
Mimi nimeleta mifano ya Nyimbo na ni katoa kabisa mfano wa nyimbo nailink hapa

Nimejaribu kugoogle top hip hop song za siasa even top 50 sijaona hata moja ya Em, zaidi ya moja alioshirikishwa, na free style especially kwenye bandwagon ya kumcritisize trump doesn't count, Hapo nchi Nzima tayari ipo Brainwashed kumchukia Trump, vyombo vya habari na social network hadi wamemfungia, hakuhitaji Guts zozote Kum critisize.
 
Amecover siasa lakini......
Na kucover siasa hakukufanyi kuwa msanii bora.
Msingi wa hii hoja ilikuwa ni kuondoa dhana kuwa hajacover hiyo part.
Motivational....
Family....
Comedy.....
Mapenzi.....
Club bangers...
Na namna zote za mziki, huwezi ukampata msanii mwingine anayecover part zote hizo kwa ubora kama wa EM.
Na kinachombeba zaidi ni msamiati, nakuhakikishia hata wewe ukiskiliza nyimbo zake saiv.....
Kila nyimbo lazima uibuke na misamiati walau mitatu .....

Na si kweli, kuwa alijipatia kibonde Trump....
Maana kuna nyimbo za nyuma kamdiss bush, kuhusu vita za mafuta mashariki ya kati.
 
Si siasa tu Nimekupa category nyingi zinashabihiana na Hip hop, mafioso, hio politicos, Gangster life etc.

Na mkuu hebu list nyimbo zako kali 10 za Em.
 
Si siasa tu Nimekupa category nyingi zinashabihiana na Hip hop, mafioso, hio politicos, Gangster life etc.

Na mkuu hebu list nyimbo zako kali 10 za Em.
Mockingbird....
Beautiful....
Loose yourself....
When am gone....
You're never over.....
Till i collapse...
Crack A bottle....
Toy soldiers...
Same song and Dance...
Legacy....
 
Mockingbird....
Beautiful....
Loose yourself....
When am gone....
You're never over.....
Till i collapse...
Crack A bottle....
Toy soldiers...
Same song and Dance...
Legacy....
So umeona mkuu? Vyovyote utakavyochagua unarudi pale pale introspective, what Eminem think na sio dunia ipoje.

Sio kwamba hao greats wengine hawana introspective songs, ila pia walikuwa na variety nyingi.

Nimeangalia lyrics kama Nyimbo tano za mwanzo zote ni introspective,
-beautifull jinsi Eminem alivyobattle drugs
-Mockingbird maisha yake na watoto wake
-loose yourself ni maisha ya B rabbit
-when am gone, kama Mockingbird kuhusu mtoto wa Eminem
-you are never over, rafiki yake eminem aliyekufa.

Kidogo hio loose yourself haimhusu yeye lakini ni expected sababu ni movie song.

Hivyo mkuu Eminem ametembea career yake kama Introspective na ndio sehemu ambayo anaijua vizuri na iliomtoa,
 
Back
Top Bottom