"Mwisho wa uchaguzi mkuu mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mkuu mwingine"
JAKAYA KIKWETE.
Je, Rais wetu 2025 awe mtu wa aina na sifa zipi? Hapa chini natoa baadhi kwa maoni yangu (nawe toa yako):
- Awe na sifa, uzoefu na uwezo wa kusimamia vyema tunu za taifa kwa manufaa ya wote. Mfano amani, haki na usawa, uhuru, umoja, utawala bora na muungano wenye tija.
- Atoke CCM ila asiwe mhafidhina wa U-CCM ule ulioathiri taifa na kutufanya kuendelea kuwa maskini miaka 59 toka tupate uhuru, kwa maoni yangu upinzani kwa mwaka 2025 hautaweza kuaminika kuchukua dola kwani mifumo ya ndani ya vyama bado ni dhaifu na pia mifumo nje ya vyama bado ni hatarishi kuweza kuvipa vyama hivyo smooth operation.
- Awe muislam na mwenye mawazo huru. Hapa sizungumzii udini, nazungumzia life principles. Kwa maoni yangu viongozi wa kiislam wanaonesha sana kusikia na kujali vilio vya watu. Tumeona kwa awamu zake nchi hii. Nina imani kwa maumivu yaliyopo sasa, kiongozi wa aina hiyo atatufaa sana.
- Awe kiongozi atakayependa serikali mseto. Uwakilishi wa vyama kadhaa ndani ya serikali na jinsia pia.
- Awe tayari kurekebisha mfumo wa utawala wa nchi kwa kuridhia upatikanaji wa katiba mpya itakayohakikisha, mihimili ya dola inakuwa huru zaidi, madaraka ya raisi yanapunguzwa zaidi, muungano unakuwa bora zaidi, wananchi wanafurahia uhuru wao na mipaka yake zaidi n.k.