Embe: Tunda linalopunguza kiwango cha asidi mwilini

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,497
EMBE+PICHA.jpg


Matunda ni moja ya vitu muhimu kwa ujenzi wa mwili wa binadamu, kwa sababu yanavirutubisho vingi vinavyosaidia mwili kuwa na afya bora na miongoni mwa matunda hayo ni embe.

Tunda hili lina ladha nzuri na ni tamu. Hiyo ni sababu kubwa ya watu kupenda kulitumia katika milo yao licha ya kuwa ni tunda la msimu.

Ulaji wa mara kwa mara wa tunda hilo husaidia kupunguza kiwango cha asidi mwilini, kuboresha mmeng’enyo wa chakula, kurekebisha kiwango cha insulin, kusafisha damu, kuboresha ngozi, kuzuia Saratani, kuimarisha kinga ya mwilini, kutibu joto la Kiharusi (Heat Stroke), hupunguza kiwango cha Kolestero na husaidia kupunguza mawe kwenye figo.

Faida nyingine ni kwamba, tunda hilo huongeza madini ya chuma kwa wajawazito, husaidia pia kupunguza uzito na hulinda macho dhidi ya maradhi kwa kuyaboresha na kuwa na uono mzuri.

Unywaji wa juisi ya embe kila siku husaidia kuleta uoni mzuri kwa sababu ina vitamin A inayoimaeisha afya ya macho na kuwasaidia wale wenye macho makavu na wenye uoni hafifu wakati wa usiku ‘blindness’.

Hata hivyo, juisi ya embe inapotumika bila kuwekwa sukari huwa ni nzuri sana kwa watu wenye tatizo la kisukari kwa sababu kusaidia kurekebisha sukari ya mwili kuwa nzuri na kurekebisha mapigo ya moyo kuwa sawa pamoja na kuondoa sumu mwilini.

Vile vile juisi hii inasifika kwa kuimarisha mfumo wa umeng’enyaji wa chakula mwilini, pamoja na kusaidia kuondoa shida ya ukosefu wa choo kwa kuchanganya na mchanganyiko wa nanasi huwa nzuri na hutibu tatizo hilo.

Ndani ya juisi ya embe huwa kuna vitamin C na vitamin A pamoja na ‘carotenoids’ ambazo zote husaidia kuimarisha kinga za mwili.

Kuhusu kuboresha ngozi

Embe linafaida kubwa katika afya ya ngozi. Kwani unaweza kupaka makapi yake usoni na kukaa nayo kwa muda usiopungua dakika 10 na baada ya hapo osha uso wako kwa maji yanayotiririka au yale yanayotoka bombani. Kwa kufanya hivyo kutakusaidia kuonekana na ngozi mbaya pamoja na kutibu tatizo la chunusi kama unalo pia.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom