eMALALAMIKO: Mfumo huu wa kuwasilisha malalamiko serikalini utatekeleza majukumu kusudiwa?

Katung'a

Member
Jul 2, 2015
38
19
Serikali kupitia wizara ya utumishi wa umma imezindua mfumo wa kuwasilisha malalamiko, pongezi na ushauri kwa njia ya kieletroniki.

Wadau najiuliza mfumo utasaidia kupunguza gharama za kufika maofisini kwa waliombali na makao makuu ya nchi?

Kweli wamezindua mfumo je watakua active kupokea na kufanyia kazi malalamiko ya watumishi na wananchi na kutoa mrejesho au ndo tunaendelea kuanzisha mambo tusio na uwezo nayo?

Karibu tujadili

Screenshot_20210701-154110_Chrome.jpg
 
Ukituma kitu genuine watasema wewe umetumwa na mabeberu au wewe ni Upinzani
Iko sehemu ambayo inakuruhusu kutuma bila kutambulika wewe ni nani, so unatupa bomu lako then unasepa unawaacha wanahangaika lkn upande wako umewapa ukweli
 
Serikali kupitia wizara ya utumishi wa umma imezindua mfumo wa kuwasilisha malalamiko, pongezi na ushauri kwa njia ya kieletroniki. Wadau najiuliza mfumo utasaidia kupunguza gharama za kufika maofisini kwa waliombali na makao makuu ya nchi? Kweli wamezindua mfumo je watakua active kupokea na kufanyia kazi malalamiko ya watumishi na wananchi na kutoa mrejesho au ndo tunaendelea kuanzisha mambo tusio na uwezo nayo?
Karibu tujadili

View attachment 1837756
Watawezana? Wataalam wa IT wanaowakutosha kuhandle mfumo?
 
K

kwamba maafisa utumishi mishahara yao ni midogo kuliko watumishi wengine? Ufafanuzi tafadhali
Sasa roho mbaya ni ya nini ikiwa na wenyewe wanalipwa mishahara stahiki....yaani mtu anambania mtumishi kupanda daraja bila sababu yoyote ya msingi.
 
Niamini mimi, hapo hakutokuwa na positive feedback yoyote, halafu mbona kwenye tovuti yao hakuna hicho kipengele.? Naipataje.?
 
Sasa roho mbaya ni ya nini ikiwa na wenyewe wanalipwa mishahara stahiki....yaani mtu anambania mtumishi kupanda daraja bila sababu yoyote ya msingi.
Juzi katika nilikuwa naongea na Mkurugenzi wa halmashauri fulani akanambia maafisa utumishi wana roho mbaya sana hawapendi kuona watumishi mambo yao yanaenda poa
 
Back
Top Bottom