EMAC Imevunjwa kweli au Ilikuwa ni Boya la Kujinasua na Mbatia ili Bajeti ya Elimu Ipite?

Tumake

Member
Mar 27, 2013
56
10
Wakuu heshina yenu. Kwa wale ambao mmekuwa mkifuatilia kwa karibu yanayoendelea mjengoni mtakumbuka kuwa Mh Eng James Mbatia amekuwa mwiba mchungu kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi tangu mwezi Januari alipowasilisha hoja Binafsi kuhusu udhaifu uliokidhiri katika sekta ya elimu nchini. Hoja yake ilisheheni mambo mengi ikiwa ni pamoja na suala la Mitaala na kuwepokwa vitabu visivyokidhi vigezo vinavyopewa kibali cha kutumika shuleni na EMAC baada ya wahusika kukatiwa mshiko na wenye vitabu vyenye makosa.

Aliendelea kulivalia njuga jambo hilo kabla Kawambwa hajasoma bajeti yake alikuwa na maswali ya kawaida akaendelea kumalia vitabuvyenye makosa vya South Caroline kwamba vinaeneza sumu katika elmu. Kawambwa akagangamala kuwa hakuna sumu yoyote kuwa huo ni usushi, Mbatia alionekana kufura sana na badala ya kumpa nafasi Mbatia atoe yaliyokuwa yanamvimbisha kutokana na majibu ya Kawambwa,Spika alitumia Busara na kumwambia Mbatia aandike hicho anachokiita sumu na kukipeleka kwa waziri akifanyie kazi na wabunge wapewe taarifa.

Ilipofika kwenye vifungu Mbatia akaibuka tena na EMACna vitabu walivyoidhinisha vitakavyonunuliwa kwa chenji ya rada ambavyo navyo alidai vina makosa akatoa mfano wa hesabu kuwa 7x2=15.

Katika majumuisho wizara ikatamka kuwa EMAC imevunjwa. Swali langu kwa kuzingatia mazingira ya Mbatia kuwashambulia na tamko kutolewa, je ni kweli EMAC imevunjwa au ilikuwa ni funika kombe mwanaharamu apite?na naam mwanaharamu alipita tena kwa pongezi kutoka kwa Mbatia kwa kuvunjwa kwa EMAC. Hata hivyo, wachambuzi wa mambo wanadai kuwa EMAC bado haijavunjwa, naomba kujua kama kweli EMAC imevunjwa kama ilivyotangazwa Bungeni tarehe 05/06/2013
 
Kawambwa hana ubavu wa kufanya maamuzi magumu. Usishangae kesho ukasoma kwenye vyombo vya habari taarifa ya Wizara kukanusha kufutwa kwa EMAC. Unacheza na siasa wewe?
 
Back
Top Bottom