Elon Musk anaongoza kwa utajiri duniani. Utajiri wake ni wa kutisha

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
13,666
28,962
Mzuka wanajamvi!

Elon Musk ni tajiri namba moja sasa hivi duniani baada ya kumpita Jeff Beezos wa Amazon na utajiri wake ni wa kutisha ambao ni zaidi ya utajiri wa Bill Gates (4) na Warren Buffet (9) ukiunganishwa pamoja. Bill Gates ni number 4 na Buffet ni number 9 kwa utajiri duniani.

Elon Musk ambae ni muanzilishi wa Tesla na SpaceX amejikuta anakuwa na utajiri wa kutisha baada za hisa za makampuni yake kupaa kwa 33% na kuuza kwa dollars za Marekani Billion 100.

Screenshot_20211017_234831.jpg


Cha kushangaza mwaka jana kama sasa hivi Elon Musk hakuwepo top ten ya billionaire na wakati huo Jeff Beezos aliongoza sana akiwa na 113 billion dollars.

Magari ya Tesla sasa hivi yanauzika kama Njugu hadi Uingereza, China na Ujerumani Tesla imeongoza kwa mauzo miezi mitatu mfululizo toka mwezi wa saba.

Soma zaidi kwa Kiingereza kwa kubofya hapo chini.

 
Mkuu hivi inawezekana je technolojia izidi hela mafuta. Bado hii kitu inanishangaza kwasababu mafuta siyo mchezo.
Mkuu Dunia ina shift kutoka kwenye raw materiao na kwenda kwenye Informations zaidi, Kipindi cha nyuma miaka kama 10 na nyuma, makamouni ya nishati kama Bp, wakina Total, wakina Exon Mobile, and alike ndo walikuwa wana tisha Dunia kwa ukwasi, leo hii hata top 20 hawapo tena.

Sisi bado mfano tunaendelea kuamishwa tuna Mali asili nyingi, mambo ya Mali asili yanaanza kupitwa na wakati sana kwa sababu ndo mali za kwanza kabisa wakati Dunia Inaimbwa.

Leo hii mfano kuna Almasi inazalishwa Maabara iko sawa kwa asilimia 100 na ile inayo chimbwa, so miaka michache tu kuanzia sasa migodo ya almasi haitakuw na kazi tena.

Tulichelewa sana kuvuna Mali asili zetu na kuzitumia vilivyo kwa sasa anaelekea kuwa too late
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom