Ellon Musk awa Tajiri namba moja

ismail hassan

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
685
1,611
Mwanzilishi, Mkurugenzi Mkuu, Fundi Mkuu na Mbunifu Mkuu wa kampuni ya SpaceX inayojihusisha na utengenezaji wa vyombo vya kusafiri na kufanya uchunguzi katika anga za mbali; pia mwekezaji na Mkurugenzi Mkuu na Fundi Mkuu katika kampuni ya kutengeneza magari ya umeme -Tesla; pia mwanzilishi wa kampuni ya Boring (The Boring Company) inayojihusisha na uchimbaji matanuri na mahandaki kwa ajili ya usafiri wa magari na treni; pia mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Neuralink inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kupandikiza kwenye ubongo na kuufanya ubongo uweze kuwasiliana na 'computer'; pia mwanzilishi mwenza wa kampuni (ya kujitolea) ya OpenAI inayojihusisha na tafiti za kiteknolojia - Ellon Musk ametangazwa kuwa mtu tajiri kuliko wote duniani.

Elon Musk alizaliwa jijini Pretoria nchini Afrika kusini mnamo mwaka 1971. Kwakuwa baba yake ni raia wa Afrika Kusini wakati mama yake ni raia wa Canada, Musk alipatiwa Uraia wa nchi hizo mbili; Afrika Kusini na Canada. Akiwa na miaka 17 alihamia nchini Canada na kujiunga na chuo kikuu cha Queens, lakini miaka miwili baadaye alihamia nchini Marekani na kijiunga na chuo kikuu cha Pennislvania. Hapo alifanikiwa kuvuna shahada mbili kwa pamoja; shahada ya Uchumi na shahada ya sayansi katika tawi la Fizikia.
Mwaka 1992 alipatiwa uraia wa Marekani na kuwa mtu mwenye uraia wa nchi tatu; Afrika Kusini, Canada na Marekani.

Mwaka 1995 alihamia jimboni California kwa ajili ya masomo ya shahada ya uzamivu (Ph.D.) katika masomo ya fizikia na sayansi ya nyenzo kwenye Chuo Kikuu cha Stanford, lakini baada ya siku mbili tu aliachana na masomo ya uzamivu na kuanza kujihusisha na biashara.

Akawa mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Zip2 iliyokuwa ikitengeneza programu pepe za tovutini (web softwares). Mwaka 1999 kampuni hiyo ya Zip2 ilinunuliwa na kampuni maarufu ya Compaq kwa dola za kimarekani million 307. Baadaye Musk alianzisha kampuni ya X.com ambayo ni benki ya mtandaoni (online bank). Katikati ya mwaka 2002 kampuni ya X.com iliungana na kampuni ya Confinity na kupata kampuni mpya ya PayPal, ambayo Oktoba 2002 ilinunuliwa na kampuni ya eBay kwa dola za kimarekani bilioni 1.5

Kabla ya kuuza PayPal, Musk alikwisha anzisha kampuni ya SpaceX miezi mitano nyuma; mei 2002. Mwaka 2004 Musk aliomba kujiunga na kampuni ya Tesla Motors, Inc. (sasa Tesla, Inc) ambayo ilikuwa imeanzishwa mwaka mmoja nyuma, akawa mbunifu magari katika kampuni hiyo. Mwaka 2008 akawa mkurugenzi mkuu wa Tesla, Inc.

Hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka 2020 Ellon Musk alikuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni 27, akiwa nje ya watu 50 tajiri zaidi duniani. Lakini ndani ya kipindi cha miezi 12, Musk amevuna zaidi ya dola bilioni 150, kiasi ambacho ni kikubwa kuliko utajiri wa Bill Gates aliovuna kwa maisha yake yote. Sasa Ellon Musk ana utajiri wa dola 185 za kimarekani, amempiku Jeff Bezo aliyekuwa akishikiria nafasi ya kwanza duniani kwa kuwa na dola 184.
Kupanda sana kwa thamani ya hisa za kampuni la Tesla, Inc. kunatajwa kuwa moja ya sababu za kumtajirisha kwa haraka mzaliwa huyo wa Afrika Kusini. Musk, baba wa watoto saba, anatajwa kuwa mtu anayetajirika kwa kasi zaidi katika historia ya utajiri na matajiri duniani.

Hizi mambo za hisa sasa inabidi kujifunza kwa nguvu.
#hisanahatifungani
#Wekeza.

Credit: Dr. Christopher Cyrilo.
FB_IMG_1610077330333.jpg
 
He is an inspirational figure, huwa nasema kile kilicho ndani ya mtu mara nyingi kina nguvu sana,angekomaa na hiyo PhD labda angekua engineer somewhere na asingefika hapa alipofika
 
Back
Top Bottom