Elizabeth Michael(Lulu) akutwa na hatia ya kuua bila kukusudia, ahukumiwa kwenda jela miaka 2

Badaaamu batamwagika

Leo ndio leo Tanzania itasimama kwa muda kufuatilia kesi ya kuua bila kukusudia ya mwigizaji Elizabeth Michaeli. Kuna watakaolia na watakaofurahi.

Lulu anatuhumiwa kumuua msanii Kanumba => Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Mahakama kuu ilimtia mtuhumiwa na kumkuta na kesi ya kujibu => Mahakama kuu imesema msanii Elizabeth Michael (Lulu) ana kesi ya kujibu

Wazee wa baraza wasema 'Lulu' ameua bila kukusudia, Jaji kutoa hukumu Novemba 13

Usikose kufuatilia thread hii kujua mbivu na mbichi

*******Updates******






Elizabeth Michaele (Lulu) ameshawasili Mahakama Kuu kusikiliza hukumu yake.

Pia mama wa msanii Marehemu Steven Kanumba naye ameshawasili katika viunga vya mahakama kuu.

Wanasubiriwa majaji waanze kusoma hukumu.

----
Jaji Rumanyika ameanza kusoma hukumu

Elizabeth Michael kwa Mara kwanza alipelekwa Mahakama ya kisutu iliyopo Dar es salaam, akishtakiwa kuua bila kukusudia tarehe 7 mwaka 2012"

"Ushahidi wa mazingira ni ushahidi ambao mstakiwa alikubali kwamba yeye ni MTU wa mwisho kuwa na marehemu ambapo mshtakiwa alikuwa na mahusiano na marehem kwa miezi 4"

Ushahidi wa mazingira unaweza kutumika kama msingi pekee wa kumtia hatiani mshtakiwa tena mshtakiwa pekee, Sasa ninapokwenda kuangalia maelezo ya mshtakiwa kama yanakidhi vigezo nilivyosema awali"

"Kwa mujibu wa mshtakiwa alisema alianza kupigwa na marehem, Mshtakiwa alisema kuwa marehemu alilewa lakini kuhusu mshtakiwa anatakiwa kutoa Maelezo yanayo jitosheleza kwa hili mshtakiwa alijikanganya"

Mshtakiwa katika maelezo yake hakueleza kuwa marehemu alianguka au laah!! wakati anamkimbiza, Maelezo ya Dkt. Josephine siyo maelezo ya cheti cha hospitali hayakuwa na hadhi ya hospitali"

"Inakinzana na hekima ya kawaida kwamba hata pale marehemu alipoendelea kumpiga na kumshambulia na akaenda kiwango cha kumtishia kumuua, mstakiwa hakuthubutu hata kumpiga..."

.ina maana alifanya kama maneno ya biblia yanavyosema mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na la kulia lakini hili mshtakiwa hakulisema."

"Hata kama marehemu angefufuka kwa miujiza Mahakama hii haitaweza kuchukua ushahidi wake.


Muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia na hukumu itatolewa baada ya mawakili wake kujitetea.


Kibatala (Utetezi):

Mshtakiwa wazazi wake hawaishi pamoja, huwa wanakutana kwenye matukio kama haya.

Mshtakiwa anategemewa na mama yake na mdogo wake.

Muigizaji wa Filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.

Wakili Peter Kibatala (Utetezi)

Tutakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wangu.

Bongo movie na sinema zetu BALOZI WENU HUYO KALA MVUA MBILI.Mjipange kuitangaza SINEMA ZETU MKIWA NA BALOZI mwingine!!!
 
Pole sanaa Elizabeth! Kweli ulikuwa mtoto...kuna mtu hakuwajibika ipasavyo kukulea hadi ukajiingiza katika mapenzi katka umri ule mdogo, Kanu nae alikosea mawili tu..kutembea na mwanafunzi wake alietakiwa kumuelekeza njia za maisha pia kujilegeza mnoo alipokuwa na hicho kitoto hadi kuanguka/ kupigwa pigo moja tu la kumtoa maisha!
 
Mzee wa varangati watanzania huwa hawapatwi na maumivu mpaka issue imguse yeye mwenyewe. Eti Kanumba kauwawa na freemason, kwanini wasimuue jana yake? kwanini wamuue mpaka lulu aingie ndani amkute mwenzie na pensi lake la draft akipata kinywaji ndiyo wamuue?

Lulu alikubali mahakamani na ndivyo ilivyokuwa ya kwamba yeye ndiye mtu wa mwisho kuonana uso kwa uso na marehemu kanumba akiwa hai, kabla ya umauti kumfika. Na eti kanumba alimpiga sana akitaka kumnyanganya simu amjue aliyekuwa akiongea naye mbele yake, mpaka akatishia kumuua na nani anauhakika lulu haja-reply kipigo? na mwanamke ambaye hana training za kupigana atapigana na nini kama siyo kutumia silaha yoyote iliyoko mbele yake ama kumsukuma adui yake bila kujali wala kujua ataangukia wapi nyuma ya kichwa chake...

Kisa walikuwa wakinyanganyiana simu Kanumba anataka kujua lulu mpenz wake alikuwa anaongea na nani, lulu alihakikisha na alikuwa tayari kufa lakini Kanumba asione wala kujua yule aliyekuwa amempigia simu na kuongea naye, alikuwa radhi kwa chochote. Hawa wanawake wengine wanadharau sana, kama alikuwa fair na hakuwa na hatia na asingetaka kusababisha haya yote kwanini asingempa simu kwa ridhaa yake mwenzie aone namba na amtambue aliyekuwa akitiririka naye mbele ya mpenz wake?

Lulu alijua alichokifanya chumbani mkwa Kanumba:
1.Kwanini lulu alivyotoka chumbani kwa kanumba alimpita mdogo wake Kanumba Seth sebuleni mbio na kukimbilia gari yake aina ya Opel iliyokuwa nje na kuichukuwa na kukimbia zake mbio?

2.Kwanini alikwenda kujificha mpaka akakamatwa na polisi?

3.Anajificha nini kama hakuwa kamaliza kazi aliyokuwa ameifuata mle chumbani?

4.Je maelekezo ya aliyekuwa anaongea naye aliyatimiza kwamba sasa tubaki mimi na wewe maliza?

5.Elizabeth Michael LULU alikiri alienda kwa Steven Kanumba mpenz wake, alimkuta hai siyo mgonjwa na alikuwa akipata kinywaji, walipokuwa chumbani wawili wote wakiwa hai walisikika wakigombana, kunyanganyiana simu ya lulu, Steven akitaka kujua lulu mpenz wake alikuwa akiongea nanani mbele yake, hatukujua ni maneno gani waliyokuwa wakijibizana Steven na Lulu, hatukujua Steven alisikia maneno gani Lulu alikuwa akiongea na huyo "third party" mpaka akangangania kumjua ni nani.. mara kukasikika kishindo kikubwa puuuuu!!!!!! baada ya dk chache lulu akatoka chumbani kwa kanumba na kuondoka kurudi kwake alipotoka.....mdogo wake Steven..Seth anaingia ndani Steven ameshakufa....daktari wa Steven anathibitisha kifo chake..kimetokana na "brain concussion" kama amepigwa na kitu kizito ama ameangukia kitu chenye ncha kali kikasababisha hiyo brain concussion, bado tunatafuta muuaji wa Steven? tunaambiwa ameuwawa na freemason labda kama huyo mdada ni freemason.

Tusikimbilie freemason huo ulikuwa ni upepo wa kupumbaza jamii freemason walipanga watoe adhabu lakini siyo kumuua na ndiyo maana hata alipokufa yule mchungaji alisema wasifanye arobaini-40 kwa sababu ile siku ya 40 ilikuwa ndiyo siku ya kumpa adhabu Steven, je pengine ni adhabu ya viboko na kumgema damu lita kadhaa?

MAMA KANUMBA HATA MUONA STEVEN KANUMBA MILELE NI SAWA NA KIFUNGO CHA MAISHA, MAMA ELIZA-LULU ATAKUWA AKIMUONA BINT YAKE HAI JELA, JAPO ATAKUWA KIZUIZINI KWA MIAKA 2 AMBAYO NI SAWA NA MWAKA MMOJA

Tuache utani kama ni mzazi wa Kanumba hii miaka miwili haitoshiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.....ilibidi lulu apate adhabu kali ambayo itakuwa ni fundisho kwa jamii na pia hiyo tabia ya kukataa kutoa simu kwa mwenzi wa pili ili kujua alikuwa anaongea na nani imekithiri sana kwa wakina mama, wanaume wapo kimya tu lakini wakipata jukwaa watasema. Kwa hukumu za namna hii...sijui.. la sivyo hawa wanawake watatuua bila ya kukusudia wengi....na kusingizia ni freemason....Bi Mtogoe...rufaa inakuhusu.......
siyo kweli kwamba miaka miwili ni sawa na mmoja jela, hukumu inahesabiwa mara tu anapohukumiwa in court anakuwa tayar ametumikia 1/3. Kwa maana hiyo yeye anakaa jela mwaka mmoja na nusu yaani miezi 18 maana robo kaitumikia kuanzia kesi ilipoanza mpaka leo hii
 
Naamini Hapa ni mahali sahihi, Ujumbe Huu ufike kwa Peter Kibatala Wakili wa Lulu.

Miaka miwili si mingi, Ila kwa Maisha ya Jela ni mingi Sana. Ila Mimi kama shabiki wa Lulu Ningependa Wasikate rufaa hata kama sheria inaruhusu, Muache Lulu Atumikie hiki kifungo. Akitoka awe huru aanze upya umri bado unaruhusu hata akitoka anauwezo wa kufanya mambo makubwa zaidi ya Sasa na Atakuwa amejifunza.


Naomba mods uzi msiuonganishe Tafadhal.
View attachment 629999
Haki imetendeka kwanza alitakiwa kuanzia kipindi kile cha kifo angekuwa mahabusu akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake.Kesi za mauaji sio mchezo mchezo! Ngoja na mijeda ikajionjee tunda la kihaya na bongo movie!
 
LULU SI MTUHUMIWA PEKEE. maoni yangu.

Wiki iliyopita, Wazee wa Baraza Mahakamani wametoa maoni yao katika kesi dhidi ya msanii Elizabeth Michael maarufu kama Lulu na kusema mtuhumiwa huyo aliua bila kukusudia. Na leo mahakama imetoa hukumu.

Ukweli ni kwamba sikufuatilia kujua nini kiliwasilishwa mahakamani lakini mimi kama mtaalamu wa mambo ya usalama wa raia, safety na watoa huduma wa kwanza (First responders) nachelea kusema Lulu kama Lulu na kwa mazingira yaliyokuwepo kwa wakati ule, sioni wapi Lulu anakuwa mtuhumiwa wa kwanza ila tu kama marehemu alikutwa na Sumu mwilini.

Tuangalie 'scenario' zifuatazo:

1. Kama ni kutokana na trauma mazingira yangeangaliwa. Umbo la Lulu na Marehemu vilikuwa tofauti sana. Ile theory ya kusukumwa kwa mazingira ya kiumbo yanamtoa Lulu.

2. Kama kilikuwa ni kipigo, bado mazingira yanamtoa Lulu kwa sababu ya tofauti ya maumbile pia.

3. Lakini kikubwa hasa hapa ni muda toka alipoanguka hadi alipofariki. Hapa ndipo ninapotaka tujadili kwa kina na wanasheria mtusaidie.

a. Je ambulance iliitwa kupitia police? Na ilichukua muda gani? Kama police waliitwa na wakaja baada ya masaa mawili hapo nani wa kulaumiwa?

b. Baada ya kubebwa majeruhi akiwa bado mzima, naambiwa walipitia polisi kuchukua PF

3. Niambie kama nia ilikuwa kuokoa maisha kwa nini wapitie police kuchukua PF3 (kwa uzembe huo Lulu bado anakuwaje mtuhumiwa?)

c. Hapo kwenye PF 3 ilichukua muda gani?

d. Madaktari wanasema (postmortem) ni nini kilimuua Marehemu? Je ilikuwa ni baada ya kuanguka or ni kwa sababu ilichukua muda mrefu kumfikisha hospitalini?

e. Kama ni kucheleweshwa kufika Hospitalini, kwa nini kesi iwaruke woooote hao na kumng’ang’ania aliyesukuma tena ka binti kadogo dhidi ya lnjembe tena bonge?

Wanasheria tusaidieni
 
  • Thanks
Reactions: ovi
Back
Top Bottom