Elizabeth michael aka Lulu ahukumiwa jela miaka miwili


T

the banker

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Messages
451
Likes
854
Points
180
T

the banker

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2011
451 854 180
Hayo ni maamuzi ya mahakama mapema leo hii baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake marehemu steven kanumba

Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemhukumu kwenda jela miaka miwili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa anaendesha kesi hiyo, na kusema kwamba mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira, hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.

"Ushahidi wa mazingira unaweza kutumika kama msingi pekee wa kumtia hatiani mshtakiwa tena mshtakiwa pekee, sasa ninapokwenda kuangalia maelezo ya mshtakiwa kama yanakidhi vigezo nilivyosema awali, kwa mujibu wa mshtakiwa alisema alianza kupigwa na marehemu, marehemu alilewa lakini kuhusu mshtakiwa anatakiwa kutoa maelezo yanayo jitosheleza, kwa hili mshtakiwa alijikanganya" amesema Jaji Rumanyika.

Jaji Rumanyika ameendelea kwa kusema kwamba.."mshtakiwa katika maelezo yake hakueleza kuwa marehemu alianguka au laah wakati anamkimbiza, maelezo ya Dkt. Josephine siyo maelezo ya cheti cha hospitali, hayakuwa na hadhi ya hospitali".

"Inakinzana na hekima ya kawaida kwamba hata pale marehemu alipoendelea kumpiga na kumshambulia na akaenda kiwango cha kumtishia kumuua, mstakiwa hakuthubutu hata kumpiga, ina maana alifanya kama maneno ya biblia yanavyosema mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na la kulia lakini hili mshtakiwa hakulisema.", amesema Jaji Rumanyika.

"Na wakati huo mshtakiwa alikuwa na miaka 17, leo ana miaka 22, alikuwa mtoto hivyo asingetambua kuwa kinachofanyika ni kibaya au kizuri, huyu mtoto sio mshtakiwa aliyelengwa nasheria ya watoto, kama mtoto wa umri huu na anaweza kafanya ya watu wazima, mahakama hii haikubaliani bali mshtakiwa ni mkomavu, hakuna mashaka kuwa kifo cha marehemu kilitokana na ugomvi", ameendelea kusema Jaji Rumanyika mahakamani hapo.

Baada ya hapo jaji rumanyika aliwapa nafasi upande wa mshtakiwa kujitetea ambapo wakili wake Peter Kibatala alimtetea mshakiwa kwa kusema kuwa mshtakiwa anategemewa na familia yake.

Baada ya hapo Jaji Rumanyika alitoa hukumu yake na kumuamuru mshtakiwa kwenda jela kwa miaka miwili.

Elizabeth Michael (Lulu) anahukumiwa kwa kumuaa aliyekuwa mpenzi wake Steven Charles Kanumba ambaye pia ni muigizaji mwenzake, mnamo April 7, 2012. Credit mpekuzihuru.com
 
Ed n Edd nEddy

Ed n Edd nEddy

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Messages
4,792
Likes
3,387
Points
280
Ed n Edd nEddy

Ed n Edd nEddy

JF-Expert Member
Joined May 3, 2011
4,792 3,387 280
Aiseee
 
radika

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Messages
16,480
Likes
23,723
Points
280
Age
36
radika

radika

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2014
16,480 23,723 280
Aiseh but ashukuru Mungu maana nilipitia Uzi flani humu hii kesi ingeweza mbeba had miaka 10 au 15
watoa hukumu wamemuonea huruma sana kwa kumchapa hata miaka miwili ashukur mungu kesho tu anarud kesi kitu kibaya sana kila kitu kinaharibika huwez hata kupanga mipango yoyote unahesabu tarehe tu za kwenda mahakamani.
 
zeshchriss

zeshchriss

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Messages
5,979
Likes
8,124
Points
280
zeshchriss

zeshchriss

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2017
5,979 8,124 280
Pole yake kwa kweli
 
Jungle Warrior

Jungle Warrior

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Messages
2,148
Likes
2,320
Points
280
Jungle Warrior

Jungle Warrior

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2015
2,148 2,320 280
Inabidi amshukuru sana Mungu na avumilie tu mana hapo atatumikia miezi 6 jela iliyobaki itakua kifungo cha nje
 
Mchizi

Mchizi

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2009
Messages
1,157
Likes
1,803
Points
280
Mchizi

Mchizi

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2009
1,157 1,803 280
Kama ingetumika silaha ndio ungezungumzia hukuma ya miaka 10 au 15, lakini hakuna silaha iliyotumika.Na wala hakuna aliyetoa ushahidi kwamba alimuona lulu akimsukuma kanumba.Hukumu imeangalia mazingira tu ya tukio.
 
Jungle Warrior

Jungle Warrior

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Messages
2,148
Likes
2,320
Points
280
Jungle Warrior

Jungle Warrior

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2015
2,148 2,320 280
Vipi kuhusu kumiliki leseni ya gari akiwa mtoto? Au Jaji alisahau
 
A

AGOLA

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
1,302
Likes
1,706
Points
280
A

AGOLA

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
1,302 1,706 280
Pole sana Lulu haya maisha hakuna anaeyajua zaidi ya Mungu,akuwahi kujua kama kuna siku unaweza kutumikia kifungo cha Jela,anywa Jaji kakuonea huruma.
Ukimaliza kifungo chako utakuja kuungana na sisi katika kazi ya kujenga Taifa.
 
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
30,684
Likes
87,146
Points
280
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
30,684 87,146 280
Itakwisha tu na akirudi atafungua ukitaka mpya wa maisha yake.
 
Soso J

Soso J

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2011
Messages
1,995
Likes
1,014
Points
280
Soso J

Soso J

JF-Expert Member
Joined Aug 17, 2011
1,995 1,014 280
Kama nawaona watu wa parole,atakaa jela miez michache tu atatoka kwa msamaha wa Rais,na hivi ni kosa lake la kwanza!Soon tutakuona mtaani akiishi maisha yake ya kawaida
 
W

wiser1

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Messages
1,733
Likes
1,689
Points
280
W

wiser1

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2015
1,733 1,689 280
Naomba kuuliza miaka miwili maana ake wanahesabu usiku na mchana au 2019 ndo tatoka huko Maana mtu moja kaniambia atatoka mwaka kesho miezi km hiii
 

Forum statistics

Threads 1,250,179
Members 481,248
Posts 29,723,322