MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,757
- 48,404
Ni ngumu kumeza hii, huyu Mkenya anataka kufanya kitu ambacho hakiingii akilini, sijui nini anawaza muda huu, neno 'badass' litapata maana na tafsiri mpya leo.
Mbio zenyewe ataanza 09:15am
Kwa watani wetu wa Kusini, ili kuwapa picha ya umbali anaokimbia chini ya masaa mawili, ni kama kutoka Dar hadi Mlandizi, kwa ndugu zangu hapa Kenya hiyo ni kama kutoka Nairobi hadi Lari.
TV nyingi duniani zitapeperusha moja kwa moja mubashara, hata zetu hapa Kenya naona zimeweka live, anajadiliwa kitaani nyumba kwa nyumba. Muhimu sana maana inawapa hamasa vijana wengi kwamba linawezekana na itawezekana.
Pia kampuni ya Youtube inapeperusha mubashara
----UPDATE----
Eliud Kipchoge ran a staggering 1:59:40, shattering the mythical sub-two marathon barrier as he completed the #INEOS Challenge in majestic fashion on the streets of Vienna
--
ELIUD KIPCHOGE: MWANARIADHA WA KWANZA KUKIMBIA KM 42 KWA CHINI YA SAA 2
Mwanariadha raia wa Kenya, Eliud Kipchoge ameweka rekodi ya kuwa Mwanariadha wa kwanza Duniani kumaliza mbio za marathon kwa muda wa chini ya saa mbili
Kipchoge mwenye miaka 34, amekimbia Kilometa 42.2 kwa kutumia muda wa saa 1, dakika 59 na sekunde 40 kwenye michuano ya Ineos 1:59 huko Vienna, Australia
Hata hivyo, rekodi hiyo haitatambuliwa kama rekodi rasmi Ulimwenguni kwasababu ameweka rekodi hiyo katika michuano isiyo ya wazi
Aidha, katika jaribio lake la mwisho kutaka kuweka rekodi hiyo mnamo mwaka 2017 alishindwa kwa sekunde 25