Elisa Mollel na Lekule ndiyo wamepigwa bao la kisigino? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elisa Mollel na Lekule ndiyo wamepigwa bao la kisigino?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Keil, Oct 17, 2007.

 1. K

  Keil JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2007
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nimesoma kwenye magazeti ya leo hii kwamba wanaowania uongozi wa CCM mkoa wa Arusha wamechukua fomu na kuzirejesha na kwamba zitajadiliwa na mapendekezo kupelekwa kwa CC na NEC kwa ajili ya baraka za mwisho. Uchaguzi ni 1/11, na kesi ya akina Mollel itatajwa tena 30/10 na kwamba upelelezi bado unaendelea, kwa hiyo hawawezi kugombea kwa kuwa mpaka tarehe ya uchaguzi kesi itakuwa bado haijatolewa hukumu na hivyo tuhuma zinazowahusu zitakuwa bado ziko pale pale.

  Hiyo ni plan ya wana mtandao kuhakikisha kwamba Arusha inashikwa na wana mtandao?????? Kwanini uchaguzi usisubiri mpaka kesi iishe? Kwenye katiba ya CCM kuna fursa inayomruhusu mgombea kusimamisha uchaguzi mpaka kesi ya msingi iishe? Kwanini hao watu wamenyimwa haki yao ya msingi ya kuomba kuchaguliwa kama viongozi wa chama chao cha siasa? Mtu akisema CCM sasa hivi inaongozwa kiujanja ujanja tu na wana mtandao atakuwa amekosea au atakuwa amewasingizia akina JK na wahuni wenzake??
   
 2. B

  BigMan JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2007
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  nadhani sasa tufike wakati mtu ukituhumiwa tu achia ngazi,kwani ccm ni akina elisa na lekule peke yao ? watu kibao wanauwezo wacha waendelee na kesi wakishinda chaguzi zipo nyingi ndani ya ccm,hiyo nimeipenda sana,ndiyo tunarudi pale pale katika swali aliloulizwa EL kule mwanza na pia tunarudi kule kule tunakozungumzia kila siku ni kina kingunge tu tangu mdogo mpaka unakufa ?
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,689
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tunaomba quote ya kifungu cha hiyo katiba ya CCM tafadhali?
   
 4. K

  Keil JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2007
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hilo lilikuwa ni swali, au wewe hukuona alama ya kuuliza mwishoni mwa sentensi yangu? Naomba angalia tena sentensi hiyo ndipo uje kuniomba hicho kifungu ambacho hata mimi sijui kama kipo au hakipo na ndiyo maana niliuza, sisi wengine hatujui hata katiba za vyama vya siasa zinasemaje.
   
 5. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2007
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kwa faida ya wengi; elisa na mwenzie mollel wameadabishwa na mh PM baada ya wao kuwa vinara wa kumpinga kwa maelezo kuwa mh PM ni MMERU na si chaguo la wanajamii wa kimasai!!!!!!! chaguo la wana-monduli ni yule mtoto wa shujaa wa miaka ile hayati moringe sokoine ambaye nae ameshapata kashkash za mh Rich-monduli!!!! Huyu bw mkubwa alisha mwachisha kazi rafiki yake ktk moja ya NGO zinazo-operate hapa ars kisa huyo jamaa alimwazima gari lake jamaa aliyekuwa anagombea na mh PM kule monduli!!
  Habari za uhakika ni kuwa hawa jamaa wa PCCB walipewa order ya kwenda kuwa kamata na kuwaumbua hawa wabunge kutoka kwa mh PM mwenyewe! mh kwa kulipiza kisasi ni moto wa kuotea mbali...
  PM NI MBABE,JEURI NA ZAIDI YA YOTE NI LIJI-FISADI AMBALO BABA WA TAIFA ALIMKATAA KWA NGUVU ZOTE!!!! JK HUONI???
   
 6. K

  Keil JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2007
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  nakubaliana na wewe ... tatizo langu liko kwenye double standard. ni kwa nini uongozi wa CCM ni mali sana kuliko uongozi wa serikalini? mbona kuna watu serikalini wametuhumiwa ufisadi na wala hatuoni effort yeyote ya kuchunguza huo ufisadi zaidi ya Rais wao kutamka kwamba wapinzani wana uchu wa madaraka na wanataka kutumia damu ya watanzania ili kupata uongozi!

  mawaziri na viongozi wa kuchaguliwa walio serikalini wanawatumikia wananchi na siyo wana CCM tu. nina ushahidi mkubwa sana 80% ya waliompigia kura ya ndiyo JK siyo wana CCM, bali ni wananchi ambao ni wapiga kura. namna pekee ya kuwatendea haki ni kuhakikisha hayo yanayowakera kwenye chama chao (CCM) wayafuatilie na kwa watendaji walio serikalini badala ya kujifanya wao ni wakali kwenye chama tu na ikifika kwenye maswala ya utendaji wa serikalini wanafumba macho na kujifanya hawaoni na hivyo kuendelea kulindana.
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2007
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  JK ataonaje wakati na yeye yuko kwenye kilele cha ufisadi?
   
 8. B

  BigMan JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2007
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Kutokana na mjadala huu unavyoendelea nilijaribu kwenda kwenye katiba ya CCM toleo la Mei 2005,sikuona kipengere chochote lakini nikaenda mwishoni mwa katiba hiyo nikakuta sehemu imeandikwa nyongeza "B" ikieleza kanuni na taratibu za utekelezaji zilizotungwa kuongoza shughuli mbalimbali za CCM ni hizi zifuatazo na chini kuna kanuni kumi na mbili zimeorodheshwa lakini mimi nilikwenda katika ya pili inayosema kanuni za uchaguzi wa CCM,ya nane kanuni za uongozi na maadili.Hivyo ni vijitabu vya kanuni na nilifanikiwa kukipata kinachoelezea kanuni za Uongozi na maadili toleo la 2002

  Hapo ndipo nikabaini kwamba kwa upande wa CCM hao jamaa shughuli yao ilishakwisha labda wanachoshindwa kuongea ni kuogopa kuingilia ama kui-fluence kesi inayoendelea kwani katika kijitabu hicho kifungu 6.2.5 kinaeleza "mwanachama anayewania nafasi ya uongozi katika chama au jumuiya hataruhusiwa yeye mwenyewe au wakala wake,nje ya utaratibu uliowekwa,kutembelea tawi,kata,wilaya,mkoa au nchi nzima,kulingana na eneo analowania uongozi akiwashawishi wanachama wenzake kwa ahadi,misaada, michango,tafrija n.k,ili wampigie kura wakati utakapofika."

  Sasa hapo mazingira waliyokutwa ni katika baa moja nje ya mji eneo la Usa river jamaa wakiwa na wajumbe na pia nilifanikiwa kupata nakala ya barua za uteuzi wa wagombea wote nchi nzima na katika kipengele cha mwisho inaagiza "hairuhusiwi wagombea au wapambe wao kuwaandikia watendaji wa chama(makati) kwa madhumuni ya kuitiwa wapiga kura kwani kampeni ya namna hiyo inaashiria rushwa na inawanyima wagombea wengi haki."

  katika mkusanyiko ule ndani yao kulikuwa na makatibu wa kata na matawi ambao shahidi wa mazingira unaonyesha ndiyo waliowaleta wajumbe pale na pia inasemekana hata ushahidi wa simu za wahusika zilizochukuliwa na takukuru zinaonyesha kuwepo na mawasiliano.

  pia katika kipengele kingine 6.6.1 "mwanachama yeyote anayegombea nafasi ya uongozi ndani ya chama hataruhusiwa kutoa takrima(kuwasafirisha,kuwapa malazi,chakula,vinywaji)Wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wa ngazi hiyo kinyume cha utaratibu uliowekwa na kamati ya ngazi hiyo.

  Kwa kipengele hicho wanabanwa zaidi kwa kukutana na wajumbe wa mkutano ambao ulikuwa uwapigie kura.

  Ingawa ni wengi wanafanya lakini,sababu ya wengi kufanya siyo utetezi wa kosa mbona kuna watu wengi tu majambazi lakini ni wachache wanaokamatwa na polisi na kufungwa ?
   
Loading...