Elirehema Kaaya na Wiliam Sarakikya kuhamia CHADEMA

Sina hakika kama kuna uchaguzi wowote unaofanyika kwa wanaCCM bila mambo ya rushwa. Hata kama mtu anagombea peke yake lazima atatoa rushwa tu!!!!!
 
Huu ni uwongo mtakatifu!.
Comon sense logic haikubali dhana ya hawa vijana kukutana na Lema Impala mahali ambapo ni open na wakapose kupigwa picha!.


CCM bado haijafanya uteuzi rasmi hivyo madogo hao hawawezi kutishia nyau!. Wana CCM wote wanajua rushwa is the order of the day katika kutafuta uongozi wowote top to buttom, sasa hiyo tisha toto wanataka wamtishe nani?!.

Picha ni picha tuu, haiwezekani ikawa walipiga zamani ila wewe ndio umeitia picha maneno ambayo sio?!.
Ukiwa muongo una dhani wote tu waongo kama wewe, aliekwambia waliweka pozi wapigwe picha nani? nilitumia utundu kuweza kupata picha hii ndyo maana hata haionekani vizuri na kama una bisha waulize kama hawa kukutana na Lema usiku wa kuamkia jana pale Impla au uliza mtu alioko pale Impala kama hawa kuwepo pale...mimi naamini wewe kama pasco una mtandao una weza kuzipata habri hizi ukitaka.....hivyo fanya uchunguzi badala ya kukimbilia kusema uongo......au picha ya ukweli ni ya kushika mikono JK na Dr Slaa....
 
Cdm sio kapu la magamba gamba shibuda anatosha waende tlp kwa babu yao msee mrema lyatonga anahitaji kampani jamanii!
 
Hawa vijana wenu machachari kabisa mnawaita makapi?

Kweli hamna maana nyie watu!
Watu wamepata kura 200+ unawaita makapi?

hata aliyekutuma hapa akiona hii lazima atakuita kukukemea.
this is just a story. Hamna popote wamedeclare kuwa wanaihama CCM. Wakifikia stage ya kukimbia CCM regardless wamepata kura ngapi, tutawagroup kwenye kundi la walafi wa madaraka na makapi. Kwenye demokrasia ya kweli lazima ukubali kushinda na kushindwa.
 
Katika watu ambao huwa hawaaminiki humu JF hata kwa kuliko punje ya mchanga ww uwa humo, kwa mashaka na picha yako lazima yawepo makubwa sana tu
Niwekee bandiko moja tu ambalo niliweka na mwisho wa siku ikaonekana ni uongo na kama ukikosa utakuwa umezihilisha kuwa wewe ni ma.akobrain....
 
this is just a story. Hamna popote wamedeclare kuwa wanaihama CCM. Wakifikia stage ya kukimbia CCM regardless wamepata kura ngapi, tutawagroup kwenye kundi la walafi wa madaraka na makapi. Kwenye demokrasia ya kweli lazima ukubali kushinda na kushindwa.
Kushindwa kupo hata sisi chadema tuna chaguzi zetu tatizo lenu MAGAMBA/MAFISADI/WAUWAJI mnatumia rushwa na namoja ya sifa ya mgombea wa CCM ni uwe fisadi unae jua kutoa rushwa kwa kwa kiwango cha juu hili nawaombeeni mliweke kwenye katiba yenu..huwezetu tu kusema na hamia chama furani wakikukataa lazima uombe na ndicho wanacho kifanya.....
 
Busara ya kawaida tu walipaswa kutumia. Nyumbani kwao Lowasa halafu wamshinde mkwewe!? Kaaya na Sarakikya hawawezi kuhama CCM physically labda mentally tu. Wana ajira nzuri tu ndani ya serikali ya CCM. Baba ya mgombea wa sasa alishinda Ubunge akiwa kitandani, Sioi atashindwaje?
 
Ni vizuri wakihama ndani ya CCM hawa watakuwa ni viongozi maslahi waende huko kwenye chama cha viongozi maslahi huku CCM kuna demokrasia ya uchaguzi yule anayechaguliwa na wanachama kwa kura nyingi ndiye anakuwa mgombea wetu sasa kama wao wamepata kura chache ndiyo wanalalamika kwa nini hawakusema tokea mwanzoni wahame tu CCM haitaki viongozi ving'ang'anizi wa madaraka.

Wahame waende huko kwenye vyama ambavyo havina demokrasia ya uchaguzi yani wagombea wake majina yao yanatoka makao makuu wala si wanachama wanaopiga kura kumchagua ambaye wanapenda agombee kupitia chama chao.

CCM itashinda kwa kishindo Arumeru kwa kuwa Sioi Sumari ni chaguo la wengi na anao uwezo mzuri wa kuwatumikia wanaarumeru kama kiongozi na wananchi wa Arumeru wanajua hilo, wapinzani wasubiri kile kilichowakuta Uzini ndicho kitakachowakuta huku Arumeru,Kidumu Chama Cha Mapinduzi CCM!
 
hadi waliposhindwa uchaguzi ndipo wanajua kuwa CCM mbaya!!! Chadema wanatakiwa kuwa makini sana kupokea wanasiasa wa aina hii.

Hawa ndio wale wa sizitaki mbivu hizi baada ya kushindwa ndo wanasema watahama kwa sababu ni chama cha kifisadi au uchaguzi urudiwe kwa hiyo ukirudiwa na wakashinda watafuta ufisadi ndani ya ccm? unafiki mbaya sana huu.
 
taarifa iunganishwe na ile tulokuwa tunaijadili hapa jana,hii wala si mpya tushaiona.
 
lema mwenyewe hatakiwi kukanyaga arumeru sasa wao wanaenda kufanya mazungumzo na mtu aliepigwa wanted,ajabu kweli.
 
Wanambeep Lowassa....................Kama hawakuwa chaguo la Lowassa walijisumbua kuingia kwenye kinyang'anyilo hicho.
 
this is just a story. Hamna popote wamedeclare kuwa wanaihama CCM. Wakifikia stage ya kukimbia CCM regardless wamepata kura ngapi, tutawagroup kwenye kundi la walafi wa madaraka na makapi. Kwenye demokrasia ya kweli lazima ukubali kushinda na kushindwa.
Lakini sababu waliyoitaja sio kushindwa ila matumizi ya rushwa,jambo ambalo kwa CCM ni dhahiri. Na mtu kama hukubaliani na matumizi ya rushwa una haki ya kujitoa.
 
Back
Top Bottom