Elirehema Kaaya na Wiliam Sarakikya kuhamia CHADEMA

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Siku chache baada ya kuchakachuliwa hatimae vijana wawili Elirehema Kaaya na Wiliamu Sarakikya watangaza nia ya kuhamia Chadema kama uchaguzi hautafanyika upya.

Walisema uchaguzi uliofanyika rushwa ilitumiaka kwa kiwango cha juu sana, hivyo hawako tayari kuendelea kukaa kwenye chama cha mafisadi wanaotumia kodi ya wananchi kujinufaisha kwa faida ya familia moja wameahidi kama uchaguzi usipo rudiwa basi wana hamia chadema kwenye chama makini na kuwahakikishia jimbo hilo linaenda chadema, haya yalijitokeza usiku wa kuamukia jana baada ya kuamua kukutana na kamanda Godbless Lema kwenye hotel ya Impala ilikuangalia uwezekanao wa kuhamia Chadema.

Nilifanikiwa kujipenyeza na kuchukua picha ingawa haionekani vema.

attachment.php


Wa kwanza kulia ni Elirehema Kaaya katikati ni Kamanda Godbless Lema na kushoto ni Wiliam Sarakikya.
wakiwa kwenye kikao cha siri hoteli ya Impala Hotel.


=========================
Upadate
Baada ya kubaini mpasuko uliko ndani ya kambi Mbili za Membe na Lowasa. Ripoti ya Mwigulu imependekeza kukata majina ya Kwanza hadi namba 4, kama njia ya kupunguza uhasama ndani ya chama hivyo itafanya kambi ya Lowasa na Membe zote kukosa kama hili litafanyika litakuwa pigo kubwa kwa Sioi alietumia kiasi cha 100mil kuhonga wajumbe hiyo Huku chama kikitumia kiasi cha mil 68 kama posho kwa wajumbe waliokuwa wakipewa kuanzia 50,000.

=============
UPDATE
Siku chache baada ya Wiliam Sarakikya kutaka kuhamia Chadema huku aliekuwa mshindi wa tano (Msani) akihamia chadema chama cha Mapinduzi wamekubaliana na matakwa ya Wiliam Sarakikya kuwa uchauguzi huo urudiwe, kamati kuu ya ccm (CC) kupitia msemaji wake Nape Nauye amesema uchaguzi huo utarudiwa tarehe 1-3-2012, huku akiwataja watakao chuana kuwa ni Wiliam Sarakikya na Sioi Sumari alie tumia zaidi ya mil 100 kwenye uchaguzi uliopita.
 
Waje ila wasiwe gambamaslahi,wakija wasitegemee vyeo coz Sisi tunamjua nassary kule meru
 
photoshop.....picha ya kuunga kwa kompyuta angalia kwa makini kwa wataalamu wa picha za photoshop.
 
Mbwee CDM musiruhusu vimeo sasa hivi wambieni watulie kwanza ,mpaka uchanguzi umalizike,kwasababu nimesikia CCM ,wanatafuta kupunguza kura ,simeona TLP na SAU kama kawaida sina uhakika na CUF kwasababu wao ni kwinsineea,kinachoonekana sasahivi ni kutaka kuingiza mamuluki ili iwe huyu mtoto waweze kupeta kirahisi.

Ni kukomaa nao tu hakuna lolote hapo.Tendwa mwambie aache mambo yake ya kusubiri uchanguzi ndo anaelezea kanuni za gharam aza uchanguzi ,huyu mzee mie simpendi kama nini ,sijuwi watoto wake wanamchukuliaje..na mambo ya kizamani sana huyu.
 
Kama walijua c.c.m ni chama cha kifisadi kwa nini wasingetoka huko mapema mpaka wamekosa fursa za kugombea ubunge ndio wanataka kujitoa?mbaya zaidi eti watajitoa iwapo uchaguzi hautarudiwa,ila ukirudiwa watabaki c.c.m,kwa hyo uchaguzi ukirudiwa uchafu wa c.c.m ndio utakua umekwisha?cdm kuweni makini msije mkaongeza kina shibuda wengne!
 
hadi waliposhindwa uchaguzi ndipo wanajua kuwa CCM mbaya!!! Chadema wanatakiwa kuwa makini sana kupokea wanasiasa wa aina hii.
 
Makapi yote ndani ya CCM aka losers yanakimbilia CDM.
CCM inabaki na wale wote walio bora!
 
Siasa za siku hizi ni za ajabu sana kuhama chama mpaka usubiri siku ya kushindwa kwenye uchaguzi? zamani wanasiasa walikuwa wanalinganisha sera za vyama. Ubora wa vyama siku hizi ni madaraka, wakikunyima au ukishindwa unahama. mmmmh
 
Back
Top Bottom