ElimuTiba: Jinsi ya kujieleza kwa Daktari

Interview in healthy setting should always be a client centered, doctor should avoid leading the patient,what you must know as a doctor is" a healthy history flows spontaneously from the patient in disorderly manner but the task of organizing the story into a logical sequence is yours, and that is what forming a basis of the medical professional"
Am categoricaly not buying it,maybe it depends on ur profs which taught u.From my simple semiology knowledge, the dialogue dépend on the docter and patients too.Your questions are the guidline.[/QUOTE]
from Bates' guides to history taking and physical examination ,different schools mkuu wangu.
 
Am categoricaly not buying it,maybe it depends on ur profs which taught u.From my simple semiology knowledge, the dialogue dépend on the docter and patients too.Your questions are the guidline.
from Bates' guides to history taking and physical examination ,different schools mkuu wangu.[/QUOTE]
Yeah, nadhani hapo nimekuelewa mkuu.Tuchape kazi, kusaidia ndugu zetu wa kipato cha kawaida.
 
imenisaidia maana ni kweli wengi wetu tukifika tunaanza kusema magonjwa badala ya kuelezea unavyojisikia
 
JINSI YA KUJIELEZA KWA DAKTARI
WENGI WETU HATUJUI KUJIELEZA,
WENGI TUNAISHIA NAUMWA MWILI MZIMA

Ni ukweli usiopingika kuwa wengi wetu hatujui ni jinsi gani tujieleze kwa daktari ili tuweze kupata tiba sahii na kwa wakati.pia kuna wakati tunashangazwa na baadhi ya maswali tunayoulizwa na daktari ambayo kuna muda yanaonekana kuwa hayana uhusiano na tatizo linalotusumbua.
Nimeona ni vyema nikaelezea ni taarifa zipi muhimu za kumuelezea daktari ili aweze kufikia hitimisho la kubashiri tatizo lako.

1: Tatizo kuu (main complaint)
Hapa unatakiwa kumueleza daktari ni kipi kinakusumbua mpaka ukaamua kumuona.ni muhimu sana kueleza tatizo hili limechukua muda gani.mfano miaka kadhaa,miezi kadhaa,wiki kadhaa au siku kadhaa au limekuwa likijirudia mara kwa mara kwa muda fulani.kwa mfano,kukohoa kwa zaidi ya wiki mbili kunaweza kusababishwa na kifua kikuu,kansa au ugonjwa wa moyo,kukohoa kwa wiki moja yaweza kuashiria ni homa ya mapafu ,kukohoa kwa masaa kadhaa yaweza kuwa umepaliwa na chakula ,kukohoa mara kwa mara yaweza kuwa ni pumu n.k

2: Historia ya tatizo
Hapa unatakiwa kueleza tatizo lako limeanza vipi,linatokea wakati gani (usiku,mchana au muda wote),linahusia
na na nini mfano kukohoa na kutapika au tumbo kuuma na kuharisha,pia eleza kama tatizo lako linaongezeka au kupunguzwa na kitu fulani, mfano unakohoa sana unapolala chali au moyo unakwenda mbio unaposimama lakini unapata afadhali unapochuchumaa au kiungulia kinapungua unapomeza vidonge vya magnesium n.k
kwa lugha fupi ya kitabibu maelezo ya ugonjwa wako yatafuata acronym ya DOPARA(Duration,Onset,Periodic ity,Associating factors,Relieving or Aggreviating factors).

3: Historia ya afya yako kwa ujumla
hapa unatakiwa kujieleza kwa ujumla kuhusu afya yako toka uzaliwe, Je umewahi kutibiwa kwa tatizo hilo hilo? umewahi kulazwa hospitali kwa tatizo lolote, umewahi kufanyiwa upasuaji? usiogope kutaja hata kama ulitibiwa kwa dawa za kienyeji. Pia ni muhimu kueleza dawa au tiba zozote ulizowahi kupata miaka kadhaa nyuma au siku chache kabla ya kufika kwa daktari anayekuona mda huo.mfano tatizo lako kwa sasa ni mimba kutoka na hapo hapo ukawa na historia ya kutoa mimba kadhaa hapo ulipokuwa kigoli yaweza kuelezea kuwa shingo ya uzazi imelegea. n.k
Pia ni muhimu kumueleza daktari kuwa kuna baadhi ya dawa zinakuletea mzio(allergy)

4: Historia ya kifamilia
Kuna baadhi ya magonjwa yanasababishwa na lifestyle zetu na pia kuna baadhi ya magonjwa ni ya kurithi hivyo ni muhimu kueleza masuala ya kifamilia kwa ujumla.
Mfano babu,baba,mama au bibi walikuwa na tatizo fulani kuna uwezekano na wewe ukawa nalo.

Mtoto anaweza kuwa na tatizo la utapiamlo kisa mama anafanya kazi muda mrefu na hivyo hapati muda wa kumnyonyesha au mume ni dereva wa magari ya mizigo ya kwenda masafa na hivyo kamuambukiza mke wake ukimwi.n.k

Haya ni baadhi ya maelezo muhimu yanayotakiwa kutolewa kwa daktari ili kufanikisha ugunduzi wa ugonjwa wa mteja aliyefika kupata huduma.yanaweza kubadilika kidogo kulingana na mazingira ya mgonjwa au tatizo lakini huu ndio msingi wa kujieleza kwa daktari.
Baada ya kutoa maelezo haya daktari anatakiwa kukufanyia uchunguzi wa mwili (physical examination) ili aweze kylinganisha na maelezo yako na baada ya hapo atakuandikia vipimo (investigations) ili kupata ugonjwa halisi unaokusumbua.
 
sina hakika sana kama uzi kama huu ulishawahi jadiliwa humu JF, kama tayari basi uunganishwe na kama bado naomba nitumie time yangu hii niwashirikishe hili japo kwa ufupi.

kujieleza kwa daktari huchangia 80%-90% kujua ugonjwa, na 10% zilizobaki ni vipimo mbalimbali mfano vya maabala. kumbe sehemu ya kuhojiwa na dakatari ni muhimu sana kwanza kwa mgonjwa kujieleza vizuri, lakini pia kwa daktari mwenyewe kuwa na " sanaa" ya kuuliza maswali na kumsikiliza vizuri mgonjwa. na mgonjwa asishangae kuona anaulizwa maswali yaleyale na madaktari mbalimballi wajibu wake ni kujieleza.
ikumbukwe pia kuongea ukweli, madaktari wamekula kiapo kutunza siri za wagonjwa, kuna mswali yatakupasua kichwa itabid ujibu tu. mfano (kama una mchepuko, kama uliwahi toa mimba, kama uliwahi tumia dawa za kulevya, kama uliwahi shiriki mapenzi ya jinsia moja, kama uliwahi kuwa na magonjwa ya zinaa n.k) usiogope kujieleza madakari washasikia mazito mengi zaidi ya hayo.

Duniani kote mfumo wa kuhoji maswali kwa wagonjwa ni uleule, Hivyo kila swali lina maana yake. na huweza hufuata mtiririko huu.
1.utambulisho 2.matatizo ya mgonjwa 3. ufafanuzi wa tatizo moja baada ya lingine 4. hali ya sehemu za mifumo ambazo haziumwi 5. historia yako tiba tofauti na ugonjwa wa sasa 6. kwa wanawake historia ya uzazi 7. historia ya kifamilia na kijamii.
baada ya hapo unafanyiwa vipimo kwa mikono ya dakari na vifaa mbalimbali vya kawaida.

1.UTAMBULISHO/INTRODUCTION.
hapa daktari anauliza taarifa za kumtambulisha mgonjwa. majina kamili, anapoishi (hii husaidia kwa sababu kuna magonjwa yapo eneo fulani tu) dini (hii husaidia kwani baadhi ya dini hawatumii nyama ya "mdudu" hivyo ni ngumu kuwa na minyoo ile itokanayo na nyama yake), umri, na jinsi ya mgonjwa. pia maasiliano na majina ya ndugu wa karibu.

2. MATATIZO/CHIEF COMPLAINS
Hapa ni sehemu fupi ila pagumu saana kwa wagonjwa kujieleza. hapa inamaanisha utaje dalili zilizokupeleka hospitali bila kuelezea kwa undani. na katika kutaja unafuta mtiririko mzuri kuwa kipi kilianza kipi kikafuata. mfano kichwa kuuma, homa, tumbo kujaa gesi, kukohoa n.k tena unataja ulianza kuumwa lini hii ni muhimu sana kwa sababu kichwa kuumwa na homa ya siku tatu huenda daktari akaanza kujifikiria malaria, lakini ikiwa dalili hizo hizo ila ni miezi 6, haiwezekani ikawa malaria hapo. hapa utakuta mgonjwa anajieleza eti ana U.T.I sijui mara ana pressure, yule naye atasema ana tezi dume.. hapa hutakiwi kutaja ugonjwa hata kama ulishawahi pimwa.

3. UFAFANUZI WA MATATIZO (HISTORY OF ILLNESS).
Hapa ndo pa kujimwaga kuelezea shida moja baada ya nyingine. KWA KILA SHIDA utaulizwa haya yafuatayo.
-dalili hiyo ilianza lini?
-ilianzaje? ghafla au taratibu
-je tatizo linaongezeka siku kwa siku au lipo vilevile?
-je kitu gani kinaongeza dalili hizo.. mfano kulala flati, chakula, baridi nk?
-kitu gani kinapunguza tatizo hilo.
kisha daktari anamalizia maswali kwa kujiridhisha kuwa sehemu zingine za mfumo wa mwili ambapo umepata ugonjwa zipo salama. mfano kama unalalmika kuwa unatapika kwa siku 6. daktari ata uliza maswali ya mfumo wa chakula, mfano kama unaweza kumeza chakula, tumbo kuuma, kuharisha n.k
lakini pia sehemu hii unajieleza historia ya ugonjwa uliokuleta hospitali, ikiwa ni pamoja na dawa ulizotumia, na vipimo ulivyofanya.

inatosha kwa leo... ntamalizia yaliyo baki siku nyingine.
 
Thread Hii Ipo

Nakaribisha Maswali Kuhusu Tiba/Dawa

Hicho Ndicho Kichwa Cha Habari Ya Thread Ambayo Tayari Ipo Hapo Juu Kwenye Jukwaa Hili Imewekewa Sticker

Mods Waiunge Hii Kule Ili Tupate Mapya Toka Huku Na Kule Kwa Ujumla Wake!!
 
Kuna wakati mwingine maswali ya madaktari yanahudhi na kuona kama vile unadharirika. Au ukijibu anaacha kufuatilia ugonjwa anaanza kukukejeli! sijui hili unalisemaje?
 
Asante daktari.
 
Mods Naomba Thread Ya Member Mwenzetu KIWETELE Iunganishwe Hapa Maana Italeta Wigo Mpana Kujadiliwa Ama Kufutilia Michango Mbalimbali
Baadhi Hawajui Kama Thread Wanayojadili Inaendana Na Hii
 
Thread Hii Ipo

Nakaribisha Maswali Kuhusu Tiba/Dawa

Hicho Ndicho Kichwa Cha Habari Ya Thread Ambayo Tayari Ipo Hapo Juu Kwenye Jukwaa Hili Imewekewa Sticker

Mods Waiunge Hii Kule Ili Tupate Mapya Toka Huku Na Kule Kwa Ujumla Wake!!
asante kwa taarifa..
nadhan mods watafanya hivyo
 
Kuna wakati mwingine maswali ya madaktari yanahudhi na kuona kama vile unadharirika. Au ukijibu anaacha kufuatilia ugonjwa anaanza kukukejeli! sijui hili unalisemaje?
daktari pia anapaswa kukushauri juu ya ugonjwa wako. mfano ukiambiwa uache au upunguze sigara hiyo siyo kejeli ni ushauri. lakini kama nilivyo andika hapo juu daktari anapaswa kuwa na mbinu au sanaa 'art' ya kuongea na mgonjwa. ili mgonjwa awe huru kujieleza, na mwisho aridhike. labda baadhi ya madaktari na wahudumu wengine wa afya ambao pengine umeaminishwa ni madaktari hawana hizo mbinu..
 
Mmenikumbusha siku na hospital ambayo siwezi isahau, nilikwenda hospital baada ya kuumizwa mazoezini nilihisi maumivu makali ya mbavu nikajua imevunjika, nimemuelekeza dokta kilichofuata nikapimwa mkojo, damu, haja kubwa na mwisho nikaambiwa nina UTI, niliomba tu bima yangu na siku rudi mpaka leo
 
Back
Top Bottom