ElimuTiba: Jinsi ya kujieleza kwa Daktari

Hata uko kwenye hospitali binafsi zinazo jiendesha kibiashara kunatatizo.dr akishaona msururu wa foleni kubwa ya wagonja anaanza kuharakisha ili ale vichwa zaidi bila kufanya diagnosis ya kina na umakini kwa mgonjwa.ndio maana hat huku kwa nchi zilizoendelea baadhi ya tiba zinafanyika kwa appointment na umakini; dr anaweza piia kushitakiwa ikigundulika kama kuna uzenmbe wake binafsi.
 
kuna shida moja kwa wagonjwa wanaoenda private hospitals,mara nyingi hujidai ni wajuaji mno!
 
kiukweli umenisaidia sana!! cjui kwanini siwezagi kujielezea kwa dr..
 
ndio lakn shda inakuja pale ambapo wagonjwa ni wengi na mda wa kumsikilza kila mmoja kwa namna hiyo hakuna
 
Nashukuru kwa somo lako zuri, ila kwa hiyo sentenc inayotaja TBC, NA MADEREVA WA MAGARI YA MIZIGO, Ungesema walio bize sana , au ambao nature ya kazi zao hawapati muda wa kukutana na wenza wao mara kwa mara kama inavyotakiwa, ina maana wafanyakazi wa TBC Watoto wao wote wana utapiamlo? au madereva wote ndo wenye maambukizi ya vvu? nawasilisha
 
ni mifano tu!no offence!
 
Moja ya tofauti baina ya Medical Dr na traditional practitioner ni kwamba ufanisi wa Medical Dr unategemea sana jinsi mgonjwa anavyojieleza, wakati traditional practitioner anaagua yaani anadai ana uwezo wa kujua ugonjwa wa mtu bila huyo kujielleza!!
 
Ni ukweli usiopingika kuwa wengi wetu hatujui ni jinsi gani tujieleze kwa daktari ili tuweze kupata tiba sahii na kwa wakati. Pia, kuna wakati tunashangazwa na baadhi ya maswali tunayoulizwa na daktari ambayo kuna muda yanaonekana kuwa hayana uhusiano na tatizo linalotusumbua.

Nimeona ni vyema nikaelezea ni taarifa zipi muhimu za kumuelezea daktari ili aweze kufikia hitimisho la kubashiri tatizo lako.
1: Tatizo Kuu (Main complaint)
Hapa unatakiwa kumueleza daktari ni kipi kinakusumbua mpaka ukaamua kumuona. Ni muhimu sana kueleza tatizo hili limechukua muda gani. Mfano miaka kadhaa, miezi kadhaa, wiki kadhaa au siku kadhaa au limekuwa likijirudia mara kwa mara kwa muda flani.

Kwa mfano: Kukohoa kwa zaidi ya wiki mbili kunaweza kusababishwa na Kifua Kikuu, Kansa au ugonjwa wa Moyo; Kukohoa kwa wiki moja yaweza kuashiria ni homa ya mapafu; Kukohoa kwa masaa kadhaa yaweza kuwa umepaliwa na chakula; Kukohoa mara kwa mara yaweza kuwa ni pumu n.k
2: Historia ya tatizo
Hapa unatakiwa kueleza tatizo lako limeanza vipi, linatokea wakati gani (usiku, mchana au muda wote) linahusiana na nini mfano kukohoa na kutapika au tumbo kuuma na kuharisha. Pia, eleza kama tatizo lako linaongezeka au kupunguzwa na kitu flani mfano unakohoa sana unapolala chali au moyo unakwenda mbio unaposimama lakini unapata afadhali unapochuchumaa au kiungulia kinapungua unapomeza vidonge vya magnesium n.k

Kwa lugha fupi ya kitabibu, maelezo ya ugonjwa wako yatafuata acronym ya DOPARA (Duration, Onset, Periodicity, Associating factors, Relieving or Aggreviating factors).
3: Historia ya afya yako kwa ujumla
Hapa unatakiwa kujieleza kwa ujumla kuhusu afya yako toka uzaliwe. Je, umewahi kutibiwa kwa tatizo hilo hilo? Umewahi kulazwa hospitali kwa tatizo lolote? Umewahi kufanyiwa upasuaji? Usiogope kutaja hata kama ulitibiwa kwa dawa za kienyeji!

Pia, ni muhimu kueleza dawa au tiba zozote ulizowahi kupata miaka kadhaa nyuma au siku chache kabla ya kufika kwa daktari anayekuona muda huo. Mfano, tatizo lako kwa sasa ni mimba kutoka na hapo hapo ukawa na historia ya kutoa mimba kadhaa hapo ulipokuwa kigoli yaweza kuelezea kuwa shingo ya uzazi imelegea n.k!
Aidha, ni muhimu kumueleza daktari kuwa kuna baadhi ya dawa zinakuletea mzio (allergy).
4: Historia ya kifamilia
Kuna baadhi ya magonjwa yanasababishwa na mifumo ya maisha (lifestyle) yetu na pia kuna baadhi ya magonjwa ni ya kurithi hivyo ni muhimu kueleza masuala ya kifamilia kwa ujumla.

Mfano babu, baba, mama au bibi walikuwa na tatizo flani kuna uwezekano na wewe ukawa nalo.

Mtoto anaweza kuwa na tatizo la utapiamlo kisa mama ni mfanyakazi wa TBC na hivyo hapati muda wa kumnyonyesha au mume ni dereva wa magari ya mizigo ya kwenda Zambia na hivyo kamuambukiza mke wake magonjwa ya gono n.k
Haya ni baadhi ya maelezo muhimu yanayotakiwa kutolewa kwa daktari ili kufanikisha ugunduzi wa ugonjwa wa mteja aliyefika kupata huduma. Yanaweza kubadilika kidogo kulingana na mazingira ya mgonjwa au tatizo lakini huu ndio msingi wa kujieleza kwa daktari.
Baada ya kutoa maelezo haya, daktari anatakiwa kukufanyia uchunguzi wa mwili (physical examination) ili aweze kulinganisha na maelezo yako na baada ya hapo atakuandikia vipimo (investigations) ili kupata ugonjwa halisi unaokusumbua.

SOURCE: ElimuTiba: Jinsi ya kujieleza kwa Daktari | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

Elimu hii ni nzuri sana. Asante sana mtoa mada.

Bila kuongeza au kupunguza ladha na maana ya mada husika ningependa tu kusistiza kwamba patient's clerking (history taking) is a sort of detective's job. Often time unaweza kuulizwa a number of issues about you at any angle of your life. Lengo likiwa kupata taarifa muhimu ili kufikia kufahamu tatizo lako kwa ufasaha.
 
Somo zuri sana, ila tatizo la madaktari wetu ni kua unapoanza tu kujielezea hata hujamalizia kumwelezea jinsi unavyojisikia, kashajaza kikaratasi chake, kanyanyuka anakuambia nenda maabara, yaani mgonjwa anabakia kujiuliza sasa mbona hata sijamaaliza kumwelezea tatizo na yeye kashaandika maelezo yamejaa karatasi? Kwa ufupi madaktari wengine wanakua wanaharaka sana huku wakichungulia nje mara kwa mara kuangalia foleni ya watu wanaomsubiria.
 
Ili suala la kujielezea ndio maana watu hawaponi magonjwa yao coz wengi wetu hatujui kujielezea kwa daktari utajuta ukikutana na daktari mwenyewe anatakiwa kusikiliza wagonjwa 5 kwa siku ila kwenye foleni wapo 50 wanamsubiri ndio kabisaaa balaa juu ya balaaa. Asante sana ngoja nitafute notebook yangu lol
 
Lakini ikumbukwe pia kuwa madaktari wengi hupenda kumwuliza mgonjwa husika persuasive questions zaidi kuliko kumwacha mgonjwa akajieleza saaana kama yuko mahakamani.itabidi mgonjwa umsome daktari wako kwa haraka mpaka umjue anapendelea staili ipi. Madaktari wengine ukiwaambia jambo moja tu anakuwa ameshakuelewa na kukuprescibe dawa!
 
ndio lakn shda inakuja pale ambapo wagonjwa ni wengi na mda wa kumsikilza kila mmoja kwa namna hiyo hakuna

hiki kisingizio cha wagonjwa kuwa wengi kinatumiwa sana na watumishi wa afya!ingawa ukimuuliza ameona wagonjwa wangapi kwa siku na avarage time ya kumuona mgonjwa mmoja utakuta hakina ukweli ndani yake.
Kwangu mimi ni heri ukatumia muda mwingi kumuona mgonjwa mmoja vizuri na akapona kuliko kulipua na baadae mgonjwa huyo akakurudia akiwa na complications.
Naamini madaktari waliozoea kutumia utaratibu huu mara kwa mara wanapata uzoefu ambao unawafanya kuhudumia wagonjwa kwa haraka na usahihi.pia kwa uzoefu wangu mgonjwa hujenga imani kubwa ya matibabu iwapo atahojiwa kwa jinsi hii kuliko kuulizwa swali moja na kuambiwa akapime.
 
ok mkuu
 
Tunashukuru kwa elimu hii maridhawa tunaomba elimu ya uzazi kuanzia ukiwa mjamzito mpaka malezi ya mtoto mchanga maaana hospitali na clinik za siku hizi hasa za private hawatoi elimu hiyo inabidi uipate mtaani kwa mazoea ya watu kama ni mzao wako wa kwanza. Jamani hii ni kweli unamuona Dr hakuna mafunzo kwa mamawajawazito ukiuliza wanasema nafasi na ukifika kwenye clinic ya watotot ni hivyo hivyo tukikutana na wakina mama wa hospital za serikali tunashangaa wamefundishwa mpaka namna ya kushika ziwa.
Mzizimkavu tafadhali saidia huku
 
Back
Top Bottom