Elimu yetu ndio tatizo

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Ukiona zaidi ya 50% ya watanzania wanashindwa kutafsiri neno siasa basi ujue elimu yetu ni kanjanja na hatujui tunacho kitaka.

Kuna watu wanasema tuache siasa tufanye kazi, wakiwa na maana ya siasa kama mbadala wa porojo au story za vijiweni wasijue kuwa siasa ndio zilizo tupa uhuru.

Kama nyerere angesema hivyo leo tungekua bado tupo watumwa , Nyerere aliacha ya ya ualimu akaingia kwenye siasa , sasa wanao sema tuache siasa tufanye kazi , mmesoma elimu gani.

Yawezekana hata mimi nipo chaka lakini tusema ukweli siasa ni nini?

Je siasa ni kudanganya wananchi?

Je nini maana ya demokrasia, jaribu hata kuzama wikipedia tuletee hapa maana ya demokrasia isiyo na neno siasa.

Je kuna maendeleo kama nchi kama hakuna siasa na demokrasia

Hapa tunazungumzia ustawi wa jamii, sizungumzii ustawi wa viongozi na utawala wa mtu mmoja.

Ndarichako rudia kitabu kile cha zamani kilicho kua kinafundisha uraia sawia.

1466838780222.jpg
 
Ni kweli tupu ,tumeanza kusikilizishwa maneno ya tuache siasa tujenge nchi ,ila kuna kosa hapo tuache siasa tuzidi kuila nchi, hawa watu wanataka kuzima moto kwa mafuta,hivi sijui wanategemea polisi,wanategemea jeshi wanategemea usalama wa taifa ,hii nchi ikichafuka basi wote hao wanaotegemewa waatakaa pembeni na si hasha na wao wakajiunga upande wa wananchi ,kusimamisha siasa ili tujenge nchi ni kutaka kuziba sauti za wananchi ,si watu wote wapo CCM,kusema kila kitu tuishitakie ccm,hilo haliwezekani .
 
Ni kweli ndugu yangu tatizo hilo neno tuache siasa tujenge nchi wanaona lina wafaa wapinzani. Kwanini ccm hawaambiwi kulikoni?

Cha ajabu kuna asilimia kubwa ya wananchi wameanza kuamini kwamba hilo.linawezekana kupata maendeleo bila siasa.

Ukitaka kumtawala mtu mnyime elimu naona madhara yake sasa.
 
Back
Top Bottom