Elimu yetu na nini kifanyike

jeff mahugi

Member
Jul 15, 2021
7
16
ELIMU KUCHUKIWA
Habari wanajamvi natumai hamjambo napenda kuanza kama ifuatavyo wahitimu wengi hivi karibuni wamekua hawafurahishwi na usomi wao pamoja muda mwingi na nguvu nyingi walizo tumia katika kukamilisha masomo hayo ambayo walidhani ndio ufunguo wa maisha yao. hali ambayo imekua ni kinyume na matarajio yao ule ufunguo wa maisha umekua ufunguo wa kufunga ndoto za walio wengi. huku wakizomewa na wale walio wapita kimasaomo kwa kua wale ambao si wasomi waliowengi wamepiga hatua kubwa mtaani. wasomi wanaporudi mtaani na kukuta wenzao wamefanya mabadiliko makubwa huanza kulaani usoomi wao ilihali hawana matarajio ya kuajiliwa na serikali kama walivyo ahidiwa na kulazimika kuanza maisha upya hapo ndipo wanaona wamepoteza muda ambayo ni rasilimali muhimu sana.

MFUMO WETU WA ELIMU, kama tujuavyo mfumo wetu wa elimu ambao ni 2+7+4+2+3... ni mfumo ambao unachukua muda mwingi wa msomi na ambao ndani yake kuna mambo yanajirudia. mfumo huu unakumbwa na changamoto kama uhaba wa watendaji pamoja na uhaba wa vifaa vyakutosha vya kusomea na kujifunzia. kukosekana kwa kujifunza kwa vitendo. mapenwkezo ya wazazi walio wengi wamekua mstari wa mbele kuwashajiisha watoto wao kufuata barabara mfumo huu na wanaona wale ambao hawaufuati mfumo huu ni watu walio potea. sera nazo zimekua zikibadilika badilika katika kuwaajir wahitimu waliopitia mfumo huu mabadiliko haya hutokea tu Rais anapobadilishwa hali inayo pelekea kuyumbisha wale ambao wapo chini.

NINI KIFANYIKE, kwa wazazi au jamii kwa ujumla ni vyema wakaeleweshwa vizuri juu ya mfumo wa kielimu ili wao wafanye maamuzi kulingana na wanavyo muona mtoto wao. mfumo wa elimu uwe huru kumruhusu mwanafunzi kujifunza kitu anachoweza na anachokipenda. muda wa mafunzo upunguzwe kutoka 2+7+4+2+3 mpaka kufikia 2+5+3... katika mfumo huu pendekezwa unapaswa uwe wavitendo zaidi kuliko nadharia.

Faida zake kutakua na muda mchache wa kukaa shule na muda mwingi wa kutumika katika fani, ubunifu utaongezeka kwa kua wanafunzi watajifunza kwa vitendo na wataingia kazini wakiwa umri mdogo hivyo watatumika kwa muda mrefu zaidi . serikali itaokoa gharama zake katika kuwasomesha wanafunzi wake ukilinganisha na sasa amabapo inasomesha kwa muda mrefu ikiwa rejesho la pesa yake inakua kidogo. naomba kuwasilisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom