Elimu yetu inahitaji tiba, iko hoi katika kitanda cha mauti

Ahmet

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
1,537
3,404
Najaribu kutafakari ni vipi tunaweza kujikwamua ili tuwe na elimu bora, lakini nakosa majibu.

Huenda shida si mtaala au content ya kinachofundishwa. Inawezekana tuna mtaala mzuri lakini tumeshindwa kudhibiti ubora wa elimu katika Mambo mengine.

Kwangu shida kubwa katika mfumo wetu wa elimu ni utekelezaji wa makusudio ya elimu katika ngazi mbalimbali. Yaani Kama tutatekeleza yale yalitungwa na watunga sera na mitaala kwa asilimia kubwa basi huwenda tukawa sehemu mzuri.

Wengi wa watekelezaji wa mitaala (curriculum implementers) kwa kiwango kikubwa huwenda hawajui majukumu yao, wanayapuuza au wanajali masilahi yao pekee na kusahau lile walilotumwa na taifa ili kuikomboa jamii yetu.

Nikijaribu kutafakari matukio yanayotokea kila siku katika sekta ya elimu huwa napata mashaka.

Matukio ni mengi lakini kila siku tunashuhudia matukio ya kuvuja kwa mitihani, rushwa ya ngono hasa vyuo vikuu n.k. na wahusika ni baadhi ya watu tuliowapa dhamana katika elimu.

Hivi vitu ndio vinauwa elimu yetu, ni juzi tu tumeona habari ya mtihani wa udaktari kuvuja, just imagine sehemu nyeti Kama afya alafu mitihani inavuja!

Kuna tukio la mhadhili kuhusika na rushwa ya ngono ili awafaulishe wanafunzi. Sasa mitihani ya shule ya msingi inavuja, kidato Cha nne na sita ndio usiseme.

Ni wazi kuwa baadhi ya wasimamizi wa elimu yetu (walimu, wahadhiri na viongozi katika elimu) huenda hawajui lengo la elimu, wanapuuza malengo hayo au wanajali masilahi yao tu.

Mbaya zaidi wanafunzi wenyewe, wazazi na wasimamizi wa elimu wanaamini marks kubwa ndio mafanikio katika elimu, marks ambazo sometimes mwanafunzi amezipata kwa kutumia mtihani uliovuja, kuhonga pesa au kutoa rushwa ya ngono. Marks ambazo ni alama tu, just A, B, C, D au F katika karatasi lakini haziwezi kukupa hata maji by itself.

Mwisho wa siku tunapata madaktari, walimu na mainginia ambao hawana ujuzi wowote. Na hapo ni Kama tunajichimbia kaburi ambalo litakuja kutuzika wenyewe au tunatengeneza bomu ambalo litatulipua wote.

Kikubwa ni kubadilisha mtazamo, let's change our mindset, let's build brilliant future. Tusifikirie faida ambayo tunaipata leo bali tuifikirie na kesho pia. Hata kama ni mtoto wako usimpe mtihani uliovuja, acha apimwe uwezo wake halisi ili tuijenge jamii imara yenye maendeleo endelevu.

"The whole purpose of education is to turn mirrors into windows"
Sydney J. Harris

“Whatever the cost of our libraries, the price is cheap compared to that of an ignorant nation.”
Walter Cronkite
 
Kweli kabisa nchi yetu ina mambo mengi ya ajabu sana na kwenye elimu tunazidi kurudi nyuma ,hatua stahiki zinapaswa kuchukukiwa kuokoa taifa..
 
hivi hizi ndio division one za siku hizi? sayansi?
1635555642851.png
 
Kweli kabisa nchi yetu ina mambo mengi ya ajabu sana na kwenye elimu tunazidi kurudi nyuma ,hatua stahiki zinapaswa kuchukukiwa kuokoa taifa..
Kabisa kabisa, tunakoelekea siko
 
Back
Top Bottom