Elimu yetu: Hivi wabunge na Serikali wana lengo thabiti la kuwasaidia wananchi?!

Vyura99tu

Member
Jan 14, 2017
46
125
Leo hii nimekuwa nasikiliza taarifa ya habari na kusikia eti shule moja huko Ruvuma wanafunzi hawana bwalo la kula chakula! Kweli au mautani?!?!

Nilishangaa kuona picha hiyo.

Hivi kweli posho ya wabunge kwa siku moja tuu achilia wiki moja wangelikuwa na uchungu wa wanakotoka wakishirikiana na serikali kwa maana ya kodi za Halmashauri tungelikuwa na matatizo haya madogo kiasi hiki!!

Tunaelewa kabisa taifa liendelee Elimu muhimu sana sasa kwa niki tunaacha wanafunzi kupata a shida za namna hii! Bado tunasema twatoa elimu bure hivi darasa moja linatakiwa kuwa na wanafunzi wangapi? Nadhani idadi imezidi.

Wazo: Malipo wabunge wanayopata walau asilimia 5 tu wanaweza kuleta mabadiliko makubwa kila Mkoa au Wilaya.

Tuache siasa na tuwasaidie wananchi .
Aibu kwa Taifa.

WaBunge/Mawaziri wetu acheni kjnena uongo huko Bungeni. Tunashuhudia yanayoendelea.
Hatutajikwamua katu kwa mtindo huu

Nimemsikia mheshimiwa Waziri wa mambo ya ndani kauli tata mbele ya kadamnasi kweli?!?!?

Hatari kubwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom