Elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum

SENGANITU

Member
Sep 19, 2012
50
15
Tanzania kwa sasa tumepiga hatua kidogo kwa kuongeza vyuo vikuu nchini. Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa hivi vyuo asilimia 99 vimeandaliwa mahsusi kwa kundi la wanafunzi wasio na ulemavu wa aina mbalimbali, na hiyo asilimia 1 (sebastian kolowa memorial university) bado si rafiki kwa wanafunzi wasioona, wasiosikia na walemavu wa viungo kwa miundo mbinu iliyojengwa, udom nayo ni maigizo tupu kwa kozi za special education. Shaka yangu ni pale watanzania tunapobaguana katika elimu ya vyuo vikuu. Elimu ni haki ya kila mtanzania na kwamba viongozi wa serikali, taasisi binafsi na watanzania kwa ujumla tunatakiwa tusaidiane kwa pamoja ili kuleta usawa katika elimu. Watanzania tufunguke na kutafakari kwa kina masuala ya elimu kama kigezo cha maendeleo. "disability is not inability, and everyone is a prime suspect for having disability".hoja yangu: Kila chuo kiwe na "resourse rooms" mahsusi kwa wanachuo wenye mahitaji maalum.
 
nina uemavu wa miguu, naappy UDOM sijui ntaenda kuishi maisha ya aina gani, yaani hadi kichwa kinaniuma hapa
 
Back
Top Bottom