Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,268
Gender ni jinsia ya kike na kiume. Afrika mtoto wa kiume anapewa nafasi kubwa katika famila tangu akiwa mdogo. Mfano tu mama kunyanyaswa na mumewe kwakua hana mtoto wa kiume.
Kuna familia unakuta wamezaliwa mabinti na wavulana. Imetokea mabinti ndiyo wenye uwezo wa pesa, watasaidia uchumi wa nyumbani lakini kwenye maamuzi ya kifamilia hawashirikishwi.
Mgawanyo wa ardhi pia humpendelea mtoto wa kiume. Wanaamini mtoto wa kike ataolewa. Sasa ikitokea hukuolewa au umeolewa mume ndoa ya wake wengi na ardhi imekwenda kwa mke mkubwa
Kuna kisa nilikisoma gazetini, mama analalamika wakati wa kulima mume wake anashinda chini ya mfenesi anacheza bao na rafiki zake. Analima mpunga mwenyewe. Wakati wa mavuno mume ndiye anahesabu magunia na kutafuta soko.
Pesa yote anashika yeye. Tena si ajabu pesa ya mauzo ikawa mahari ya kuoa mke mwingine.