Elimu ya umiliki wa Kampuni na Hisa

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,576
18,894
Kwenye hoja yoyote Kuna aina tatu ya audience Kuna prisoners, graduate na holdermaker. Graduate ni aina ya watu ambao wanajifanya wanajua kila kitu wakati vingine hawajui ukimpempeleka kwenye soka yeye anakuwa kocha ingawa taaluma ya ukocha hana, ukija kwenye siasa anajifanya anaijua siasa kuliko watu ambao wapo kwenye siasa.

Tukija kwenye Hili suala la umiliki wa hisa nimeona wengi ni weupe na hawataki kukubali wao ni weupe.Bahati nzuri nasomea course ya business administration na haya mambo nayajua lakini pia baba yangu ni mmiliki wa company na huyo ndie amenifanya nisomee biashara

FORMS OF BUSINESS
Kuna aina tatu ya mfumo wa biashara me nitajita mbili ambazo ni very common in Tz ambazo ni sole proprietorship na Partnership.Sole proprietorship ni mfumo wa biashara ambao mmiliki wa company anakuwa mmoja wakati partnership mmliki anakuwa more than one person.

PARTNERSHIP
Kwenye Huu mfumo Mara nyingi Kuna kuwa na founder au mwazilishaji wa company na mwalizishaji anaweza kuwa mmoja au zaidi Kama ni mmoja huwa anatafuta watu wengine ambao wataingia ubia kwenye biashara yake Kama watakuwa wanafurahishwa nayo.Hao watu wataingia wakiwa na capital zao kwajina lingine wanaitwa angels au shareholders na wanakuwa ni sehemu ya umiliki.

Hisa zitatofautiana kutokana na capital zilizowekezwa miongoni mwenu baada ya kuingia ubia kwenye company na mapato yakipatikana yatagawiwa kutokana na asilimia za hisa mlizo nazo kwenye company.

Tukija kwenye WASAFI MEDIA mwanzilishi au founder wake ni DIAMOND PLATNUMZ na yeye pia ndio CEO ambaye ameingia ubia na mrs kusaga na jamaa mmoja.Founder Mara nyingi anakuwa CEO ni Kama unavyoona Facebook founder wake ni Mark Zuckerberg na pia yeye ni CEO pia Microsoft founder wake ni billgates pia ni CEO

DECISION MAKE
Mwanzilishi wa company au founder ndio mwenye maamuzi na mamlaka makubwa katika kufanya decision na si major shareholder Ila Kuna conditon inaweza major shareholder akawa na maamuzi makubwa ya kufanya decision mfano ikiwa ukiachana

Yeye kuwa na share kubwa pia kuwa founder wa company.Baadhi ya watu wanaamini eti ukiwa na share kubwa wewe ndo una maamuzi hiyo shule mmesomea wapi? Tofauti ya mzungu na mbongo ni moja especially pale ambapo hawajui mambo mzungu atadadisi either kwa kuuliza au kwa kufanya utafiti mbongo yeye anameza kitu Kama kilivyo.

Mark Zuckerberg ana hisa 28.1% za Facebook ambazo ni ndogo lakini yeye ndio mwenye nguvu ya kufanya decision because he is founder wa Facebook mfano mwingine ni Billgate huyu ni second largest of shareholder of Microsoft but ndio mwenye nguvu ya kufanya decision kwa sababu zipi yeye ni founder na CEO.

Tukija kwenye WASAFI MEDIA mwenye nguvu ya kufanya decision ni Diamond ya kuajiri wakina Jonijoo, Maulidi Kitenge n.k wote wale wamesajiliwa na Diamond na wanalipwa mishahara na Diamond ndio maana wanamuita boss pale Wasafi Media lakini pia kamweka ndugu yake Romy Jones kama vice president pale Wasafi Media pamoja na marafiki zake ambao alihustle nae Kama Ricardo Momo, Makame, James Mwampamba, Madebe ambaye pia producer wa kipindi Cha block89 ambaye huyu wakati Diamond anatafuta wadau wa kumwezesha kipindi hiko hajatoka alikaa kwa huyu pale Kariakoo.

Diamond ana uwezo wakusema fulani wimbo wake usipigwe na haupigwi ila yeye akaja na slogan hii ni yetu sote so wanapiga nyimbo za wasanii wote hata waliogombana na wanagombana na familia ya Kusaga,Ruge mfano Jide, Dudu Baya, Niki Mbishii n.k Clouds ngoma zao hazipigwi ila wasafi wanapiga ngoma zao maana ya Mondi so hiyo nguvu ya Kusaga ipo clouds sio WASAFI.

MTINDO WA HISA
Hisa za share holders wa kampuni husika zinaweza kupanda au kushuka kutokana na distribution ya mtu kwenye company.Ukitokea kuna mtafaruko kwenye company mtu anayebaki ni founder wa company tukizungumza kwa WASAFI MEDIA anayebaki ni Diamond ambaye ni founder na CEO wa WASAFI MEDIA wengine wanauza hisa zao either kwa Diamond yeye mwenyewe au kwa watu wengine.
 
Heading uliyoandika na maelezo haviendani, it seems lengo lako ilikua kutoa uchambuzi kunusu wasafi media company ila si kutoa elimu kuhusu company business.

Kwa kukusahihisha tu huwezi kuita umiliki wa company ni sole proprietorship kama ulivyosema hapo, sole proprietorship ni single ownership of the business, na company haina single ownership, umiliki wa company huanzia watu wawili kwa private company na saba kwa public company.

Pia ni makosa kuiita company ni partnership kwa kigezo eti ina wamiliki zaidi ya mmoja. Partnership ni aina nyingine kabisa ya biashara tofauti na company, kinachoifananisha company na partnership ni uwepo wa wamiliki zaidi ya mmoja na kinachotofautisha ni ile limited liability pamoja na legal personality of the entity ambapo partnership ni unlimited na company ni limited.

I think unatikiwa usome zaidi forms of business ownership pamoja na sheria zake, maana umesema bado upo chuo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom