Elimu ya Ufundi ni muhimu lakini inategemea sana mambo yafuatayo ili ilete tija na matokeo katika kupambana na Tatizo la ajira

Ushauri wako utakua umekosa mana endapo hujazungumzia 'Uboreshaji wa sekta ya AFYA'...AFYA nimuhimu sana kuliko yote hayo...ongeza kitu hiyo
asante mkuu..ndio maana pale chini nimeandika haya ni maoni yangu ninayoyapendekeza pamoja na yale yatakayopendekezwa na wachangiaji wengine (ukiwemo wewe)...Asante mkuu.
 
Kwamba aliyepata division four au zero ndo anafaa kuwa mcheza mpira,mwimbaji n.k....mnachanganya akili na kipaji.
 
Nakumbuka hata dada yangu kipindi anasoma secondary miaka ya 2003 alikuwa anasoma na somo la agriculture....sijui imeishia wapi hii...asante kwa mchango wako.
Kulikuwa na shule za kilimo, hilo somo ilikuwa lazima ulisome kwenye hiyo shule ya kilimo, kama zilivyo shule za ufundi ambapo lazima usome masomo ya ufundi.

Shule niliyosoma somo la kilimo lilikuwepo lakini ilikuwa option kulisoma, masomo mengine ya option yalikuwa Kifaransa na Addition Mathematics.

Nilipofika kidato cha tatu, nilichagua kusoma Addition Maths kwenye masomo ya option, wengine walichagua French na Agriculture.
 
Soil science zina walimu wa kutosha.
Kwa taarifa yako kila mwalimu wa chemistry Tanzania ni mwalimu wa soil science.
Tulikuwa na shule za ufundi kama ifunda, moshi tech, Arusha tech, mbeya tech hizi tuliziua na nyingine ziligeuzwa vyuo lakini wanafunzi walitoka wakiwa na ujuzi kamili.
Binafsi nimesoma shule ya kilimo o level tulifundishwa vitu vingi kuanzia soil science, livestock keeping, agro mechanics, rural economy, bee keeping, fishing ni knowledge ambazo zinamsaidia mwanafunzi akimaliza shule changamoto kuna baadhi ya topic kama soil science hazina walimu wa kutosha
 
Back
Top Bottom