Elimu ya tz imekufa?

Kifulambute

JF-Expert Member
May 8, 2011
2,539
755
Habari za asubuhi wana Janvi....kweli ilinisikitisha sana jana nilipokuwa napitapita mahala basi nikakuta wanafunzi wa shule moja hapa arusha ya Secondary. Nikawa napiga nao story za masomo na kuwaulizauliza maswari japo nijue kweli wanayosoma wanayaelewa ama wanakwenda shule kama ratiba ilivyopangwa tu..

Basi nikawa naongea na mwanafunzi mmoja wa form two na maswali yangu yalikuwa ni kama yafuatayo.

1. Unajua mito mikuu iliyopo tanzania?
Jibu: Mimi huwa nasikia tu ipo Songea na Mwanza ila mwalimu wetu hajatuambia iko wapi.
2: Ni nani aliyepandisha bendera ya Tanzania na kuondoa ile ya mkoloni?
Jibu: Simjui
3: Ni nchi gani Africa mashariki ilianza kupata uhuru
Jibu: Sijui

Nilipoachana nae ila nikawa na maswali mengi sana kichwani mwangu hivi siku hizi watoto hawasomi geography na history? iweje mtoto wa form two asijue haya wakati sisi tulikuwa tunajua hadi... Ni nini na ni wapi garaganze, kumbi saleh? basi nilipofika home nikawa naongea na katoto ka english medium Trust st. patric.

1.Two plus two
Jibu: Four
2. Mbili jumlisha mbili
Jibu: .......... sijui

basi kufikia hapo nikaanza kusema elimu yetu iko wapi? watoto wanaelekea wapi jamani? hebu waalimu mnisaidie
 
Mfumo wetu wa kupata wafundishaji na wale wanaoitwa wamefaulu ndo tatizo! ili usomee ualimu mpaka uwe umefeli!!!
 
Back
Top Bottom