Elimu ya tanzania kushuka nani anachangia zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu ya tanzania kushuka nani anachangia zaidi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Monyiaichi, Sep 28, 2012.

 1. Monyiaichi

  Monyiaichi JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 1,825
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Nimeguswa kuanzisha hii mada kwa sababu mbalimbali nilizoziona na kuzipima katika swala zima la kushuka kwa kiwango cha elimu katika nchi yetu ya Tanzania. Elimu kushuka inachangiwa na mambo kadhaa kama yafuatayo;
  • Serikali haijatilia mkazo kuinua kiwango/viwango vya elimu katika level mbali mbali tukianzia upatikanaji wa waalimu wanaokidhi katika kufundisha. ukiangalia factors kama elimu yao, malipo yao nk, vitendea kazi kuanzia majengo, vitabu, labs nk na uwiano wa haya yote katika nchi nzima ukoje? mikoa mingine ni worse na michache ina nafuu.
  • wizi wa mitihani katika level zote, kwa nini unatokea-wasabishaji ni wanafunzi? waalimu? wazazi? na kila mmoja anachangiaje katika hili?
  • waalimu wako fair kwa wanafunzi, tukianzia vyuoni-hakuna wanafunzi wenye uwezo wanaofelishwa kwa sababu aidha za chuki au interest za waalimu? hakuna wanafunzi wanaofaulishwa bila kuwa na uwezo wa hivyo na waalimu kwa hizo hizo interest binafsi (rushwa ya fedha, ngono, undugu, urafiki n.k). kama secondary o-level au A- level exams zote ziko fair katika masahihisho? hakuna wanaodhulumiwa na wanaojikuta wamependelewa na hawakustahili alama walizozipata? na kama hivyo vitu vipo tunazalisha taifa la vipi? kama wanaodhulumiwa hawana uwezo wa kifedha na nafasi wanaishia wapi na ndoto zao?

  kwa hayo machache niseme kama hizo zipo si tunahitajika kubadili mwelekeo na mwenendo ili walao elimu iboreshwe na tupate wataalam stahili?

  naachia michango ya wengine, na hayo ni mawazo yangu tu kama observation ya muda niliyofanya.
   
 2. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wote mnachangia kwa vile hampendi kusoma wala kusota bali kuukata hata kama ni kwa kujiibia. Isitoshe wengi wanajifanya wajuzi wakati ni vihiyo. Watu wanaghushi shahada au kutumia za kupewa bado mnawavumilia. Hapo mwenye kustahiki lawama zaidi ya wabongo wenyewe nani?
   
Loading...