Elimu ya Tanzania haimkomboi kijana zaidi ya kuendeleza ujinga

Josh J

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
1,320
2,000
HIZI NDIZO SABABU KUU MBILI ZINAZO SABABISHA UMASIKINI TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA

1: UDHAIFU WA ELIMU YETU
Elimu yetu haijitosherezi wala haiendani na dunia tuliyo nayo leo tofauti na mataifa mengine kama Uingereza, Marekani, Canada n.k

Mfano mwanafunzi Alie Soma kombi ya HGK/HGL/HKL kwa level ya kidato cha sita unaweza kunambia ni kitu gani ambacho mwanafunzi huyu anakua ametoka nacho shuleni ambacho kinaweza msaidia kuja kutatua changamoto za mtaani?

Just imagine mwanafunzi alie Soma history anatoka shuleni akiwa anafahamu mambo yaliyo tokea nyuma miaka 70 iliyo pita; mfano vita vya Kwanza ya dunia, anguko la uchumi wa dunia.

Sasa ashumu mtoto anatoka shuleni amekalili mambo ya miaka 70 nyuma, mtoto anatoka shuleni anajua mambo ya kuandika insha, kujitambulisha, kutafasiri maneno na namna ya kuwasiliana (IELTS) kwenye language.

Ukija kwenye geography mtoto anakuja kasoma mambo ya ma barafu kama topic, ukiangalia barafu tunazo zisoma zinapafikana nchi za wenzetu canada, USA n.k Sasa hapa unategemea lini Africa tutajikomboa kwenye dhahama ya umasikini?

Just imagine msomi mwenye level ya form 6 anakuja nyumban kichwani akiwa amebeba 85% ya mambo ambayo hayana impact kwenye suala la kujikwamua kiuchumi. Shame.

Viongozi tunao waona leo ni zao la elimu yetu kwa aslimia kubwa, labda ukitoa elimu za juu walizo kwenda kupata huko ughaibuni.

Ushauri wangu kwenye suala la elimu, Tanzania tunahaja ya kuireform elimu yetu tusiendelee na elimu ya kukalili kujibu mitihani, Tunahitaji elimu ya kuweza kutatua changamoto tulizo nazo.

Wanafunzi wasome kama ni mambo ya kilimo, ufugaji uvumbuzi ingali wakiwa vidudu, wasome namna ya kutumia vyanzo vyetu vya maji katika kukuza secta ya kilimo kuanzia vidudu mpaka vyuoni,

Wasome namna ya kutumia kilimo chetu kulingana na mazingira ya kila kanda, huwezi amini wavyetinam walikuja Tanzania kujifunza kilimo Cha alizeti, lakin leo sisi ndio tunaagiza mafuta ya kula kwa wanafunzi wetu na alizeti yetu haina ubora tena. Inaumiza Sana.

Kama ni ufungaji wajifunze ufugaji unao patikana kwenye taifa letu na namna ya kutumia,

Tuache kukalili ufugaji ambao unapatikana ulaya na Marekani afu mwanafunzi anaenda kujibia mtihani huu ni ujinga kwa Africa nzima.

Inasemekana kwasasa kuna hatari ya kupoteza kuku asilia kutokana nakukosa ubora yaan wanakua wadogo na si wazito hivyo hukosa sifa katika soko la biashara, lakin kumbe kuku wa kitanzania akifungwa vizuri anauwezo wa kufikisha mpaka kilo 4) ila mtoto anamaliza form 6 hajui hata namna ya kufunga kuku afu Wana siasa wanao kula mshahara wa zaid ya 11ml anakuja anakwambia watoto wajiajiri, hawa ni wajinga walio zalishwa na elimu yetu.

2: SIASA NA WANASIASA (mfumo wa utawala na viongozi)
Tukatae tukubali kalibu 98% za hatima ya maisha yetu hasa ki uchumi huamuliwa na wanasiasa kwakua wao ndo hutunga sera zote za maendeleo ya taifa.

Kama nilivyo sema kwenye hoja ya elimu viongozi tulio nao Leo ni zao la elimu yetu hii tuliyo achiwa na mkoloni ambayo ni duni na haitoi hatima ya kujikomboa kama taifa.

Imekua kawaida Sana kuwa na wanasiasa ambao hawana vision kwa taifa lao wala mikakati maarumu ya kiukombozi kwa taifa letu.

Viongozi walio bahatika kupata elimu za juu, huja na maneno ya ki ulaghai, na kuwaaminisha watu kua uzalendo ni kuhakikisha unapambania chama kubaki madalakan, na kwa bahati mbaya wamefanikiwa pakubwa kutuaminisha hivyo kwa maslahi yao wenyewe.

Sisi kama taifa tunaongozwa na maono ya mtu mmoja, katiba yetu ya Tanzania imempa mamlaka makubwa Sana kiongozi wetu mkuu wa nchi yeye ndo muamzi wa kila kitu, mfumo wetu wa utawala na uongozi ni mmbovu kuanzia ngazi ya chama mpaka serikali, katika chama silaumu Sana maana mfumo unaminufaisha chama na wala sio taifa.

Yaan kwamba rais anakua mwenyekiti wa chama na Bado ni kiongozi wa taifa na ni amiri jeshi mkuu.

Katiba yetu inampa kiongozi wa nchi mamlaka makubwa na kuwekewa kinga, huu ni udhaifu kama taifa. Kwakua muwekezaji anauwezo wa musoma katiba yetu leo na sheria zetu za nchi akagundua udhaifu wetu kama nchi upo wapi na ni sehem gani pa kupitia.

Mfano mwekezaji akipitia katiba sheria zetu akagundua udhaifu wetu sisi ni kutoa mamlaka yote kwa rais na kumpa kinga, yeye atawaza namna ya ku deal na rais akimuweza rais ujue ameweza taifa.

Yatatokea yale ya kiongozi mmoja aliye kuja na sera za ubinafshaji, kwenye mgodi wa geita Tanzania ikawa inachukua 3%, kampuni GGM 70% zileeeee 27 utajua mwenyewe aliye kua anazichukua.

Just imagine yaan taifa linapata 3% kweli? Shame

Hapa kama taifa ndipo kuna udhaifu.

Ushauri wangu kwenye inshu ya siasa

Sisi kama watanzania wenye uchungu na nchi yetu maamuzi yetu ni hatima ya taifa letu, tunawajibu wa kuyatafakari maisha yetu na haya ya wana siasa, tuna wajibu wa kutuliza akili na kukuunga mkono kila mwenye hoja ambayo unaona utalikomboa taifa, tukubari tuwe na katiba mpya
 

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
10,891
2,000
Hata level ya chuo kikuu nako tatizo imagine kozi kama "Industrial Psychology" duuh kazi kweli kweli!!
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,787
2,000
Elimu yako wewe mwenyewe kwanza!??? Pls tuanzie hapo, sawa!??? Kwa vile unashindwa hata kutofautisha ^ARA^ na ^ELO,^ basi kweli elimu nzuri ya Tanzania haijakusaidia.

Nyie ndio sampuli ya watu mlikuwa mnawatukania walimu home kwa wazazi wenu mkitoka shule. Umeona sasa!? Sasa umekua, umepanua wigo wa matusi, unatukana taifa zima na elimu husika.

Ukifikisha miaka 25 au 30 utakuwa unatukana dunia nzima, siyo siri. Au nasema uongo ndugu zangu!???
 

Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
9,101
2,000
Elimu yako wewe mwenyewe kwanza? Pls tuanzie hapo, sawa? Kwa vile unashindwa hata kutofautisha ^ARA^ na ^ELO,^ basi kweli elimu nzuri ya Tanzania haijakusaidia...
Tatizo tulilonalo ni wanafunzi wa vyuo kufikiri wote baada ya kuhitimu wanaweza kuajiriwa na serikali. Hakuna nchi duniani iliyoweza kufanya hilo.

Nawafahamu vijana wengi wa kichaga mtaani wenye elimu nzuri na wamejiajiri na kuajiri wengine. Hii ndiyo kind of mentality we need as a nation. Kama wachaga wanaweza, hawa wapumbavu wengine wanaolilia kuajiriwa kila siku wanashindwa wapi?
 

Josh J

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
1,320
2,000
Elimu yako wewe mwenyewe kwanza? Pls tuanzie hapo, sawa? Kwa vile unashindwa hata kutofautisha ^ARA^ na ^ELO,^ basi kweli elimu nzuri ya Tanzania haijakusaidia. Nyie ndio sampuli ya watu mlikuwa mnawatukania walimu home kwa wazazi wenu mkitoka shule. Umeona sasa!??? Sasa umekua, umepanua wigo wa matusi, unatukana taifa zima na elimu husika. Ukifikisha miaka 25 au 30 utakuwa unatukana dunia nzima, siyo siri. Au nasema uongo ndugu zangu!?
Mkuu Kuna Mahali Nimetukana?
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,787
2,000
Tatizo tulilonalo ni wanafunzi wa vyuo kufikiri wote baada ya kuhitimu wanaweza kuajiriwa na serikali. Hakuna nchi duniani iliyoweza kufanya hilo.

Nawafahamu vijana wengi wa kichaga mtaani wenye elimu nzuri na wamejiajiri na kuajiri wengine. Hii ndiyo kind of mentality we need as a nation. Kama wachaga wanaweza, hawa wapumbavu wengine wanaolilia kuajiriwa kila siku wanashindwa wapi?

Suala la msingi hapa siyo kuajiriwa au kujiajiri. Hoja kubwa ni iwapo elimu inakidhi mahitaji -- is it competitive enough!??? Kwa sababu, kama Tanzania ajira ni kiduchu, mwenye elimu competitive anaweza hata kuajiriwa kwenye Sayari ya Mars. Unaelewa sasa!??
 

Nibiru

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
241
500
Mkuu kitu chochote ambacho ni mainstream ni kwa ajili ya kukutawala na kukunyonya, formal educations zote zimetengenezwa ili uwaze ajira na kuwachumia wenzako.

Ukitaka kupata madini ya ukweli kuhusu Life, secrets na propaganda za hii dunia zama deep/dark web.
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,240
2,000
Mtoa hoja hii u got my vote, umeelezea tatizo na umekuja na mawazo mbadala, kudos kwako mkuu, tuliobahatika kusoma kipindi nchi ina heshima na adabu, kuliundwa tume ya J.

Makwetta(rip)ilitembea nchi nzima kupata maoni kuhusu mfumo wetu wa kielimu na baada ya politics kubadilika ile ripoti inaoza pale wizarani na haya ndio matokeo yake.

Moja ya mapendekezo ilikuwa tuimarishe elimu ya ufundi, tuondokane na hii level ya form 5na form 6, tutumie mfumo wa grades yaani once on matric unaweza kwenda varsity straight na wengi waingie kwenye technical institutions.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
23,382
2,000
Elimu yetu inachezewa na kushikwa shikwa na kila anayejisikia kwa miaka zaidi ya 50. Mitaala haina consistency na haiendani na mahitaji ya jamii ya Tanzania maajabu yake haiendani na soko la dunia pia.

Leo hii kijana akitaka kuomba scholarship anakuta automated interface yenye vyuo vyote duniani, tafuta chuo chako, utafurahi. Unaweza ukaikuta UDSm tu vingine hakuna na UDSm ipo kwakua once ilikua na wataalamu waliotoa machapisho na walifanya utafiti wa kusaidia Tz na dunia.

Siku hizi hakuna hao watu siyo huko UDSM wala Amazon college wamechagua kua madokta na maprofesa ili wakapige kwenye siasa.
 

ndenjii handsome

JF-Expert Member
Apr 27, 2021
288
500
Elimu yako wewe mwenyewe kwanza? Pls tuanzie hapo, sawa? Kwa vile unashindwa hata kutofautisha ^ARA^ na ^ELO,^ basi kweli elimu nzuri ya Tanzania haijakusaidia. Nyie ndio sampuli ya watu mlikuwa mnawatukania walimu home kwa wazazi wenu mkitoka shule. Umeona sasa? Sasa umekua, umepanua wigo wa matusi, unatukana taifa zima na elimu husika. Ukifikisha miaka 25 au 30 utakuwa unatukana dunia nzima, siyo siri. Au nasema uongo ndugu zangu!???
Wee jomba jinga hivi haya unayo hoji yana impact gani ? Umeacha mambo muhimu aliyo andika unakuja kosoa jambo dogo saana asee
Broo nakuhukumu hapahp ww ni

Sent from my VFD 200 using JamiiForums mobile app
 

Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
9,101
2,000
Suala la msingi hapa siyo kuajiriwa au kujiajiri. Hoja kubwa ni iwapo elimu inakidhi mahitaji -- is it competitive enough!??? Kwa sababu, kama Tanzania ajira ni kiduchu, mwenye elimu competitive anaweza hata kuajiriwa kwenye Sayari ya Mars. Unaelewa sasa!???
Stupid thinking. Hao wachaga wanaofungua biashara kila kona mtaani kwako wana elimu gani special? Think outside the box. Kama mmeamua ku-embrace capitalism, take it whole. No execuses. Marekani wana-outsource from allover the earth, if you think you,re qualified enough, why not go compete with them! Kama kina Mataragio waliweza, unakwama wapi wewe?

Unajua namba ya wataalamu wanaofanya kazi nje ya nchi graduates wa UDSM?! I am not talking about these so called vyuo vya kata. Talk about UDSM.
 

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
1,948
2,000
Ndugu kutofautisha R na L sio tatizo la Elimu ni tatizo la kikabila.


Nije kwenye Mada:

Mkuu kubadilisha hilo Ombwe itatuchukua miaka mingi sana ijayo hasa kwa hawa vijana tulionao kwa sasa hivi. ( Vijana wanapewa nafasi ya kuongea na Rais wanaishia kusema yaleyale ya kusifu na kuabudu )

Tanzania kama Taifa tuliamua kuwekeza kwenye propaganda na matumbo ya watu.

Mf: kuna Nchi ilikuja Tanzania kuchukua mbegu za mafuta ya kupikia na leo ndio nchi inaongoza kwa kuuza hayo mafuta Duniani sisi tuliotoa mbegu bado tuna uhaba wa mafuta tena wa kutisha.

PENDEKEZO
Tanzania iache haraka sana kuwekeza kwenye Siasa na propaganda za kisiasa ambazo hazitoisaidia Nchi badala yake iwekeze kwenye ujuzi na usawa wa kimaslahi.
 

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
1,948
2,000
Mkuu kitu chochote ambacho ni mainstream ni kwa ajili ya kukutawala na kukunyonya, formal educations zote zimetengenezwa ili uwaze ajira na kuwachumia wenzako.

Ukitaka kupata madini ya ukweli kuhusu Life, secrets na propaganda za hii dunia zama deep/dark web.
Can you please elaborate?
 

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
1,948
2,000
Mtoa hoja hii u got my vote, umeelezea tatizo na umekuja na mawazo mbadala, kudos kwako mkuu, tuliobahatika kusoma kipindi nchi ina heshima na adabu, kuliundwa tume ya J. Makwetta(rip)ilitembea nchi nzima kupata maoni kuhusu mfumo wetu wa kielimu na baada ya politics kubadilika ile ripoti inaoza pale wizarani na haya ndio matokeo yake, moja ya mapendekezo ilikuwa tuimarishe elimu ya ufundi, tuondokane na hii level ya form 5na form 6, tutumie mfumo wa grades yaani once on matric unaweza kwenda varsity straight na wengi waingie kwenye technical institutions.
Tatizo Wanasiasa kitu chochote ambacho kinafungua milango kwao ni tatizo kubwa sana hawajali kesho ya Taifa wanaangalia leo na jinsi gani wataendelea kula posho.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,787
2,000
Sina hakika kama nyie watu mnajua hata kusoma na kuandika!??? I cannot afford to waste my precious time on you, guys!??? You're a provocative headache. I guess Asprin itawafaa sana.


Wee jomba jinga hivi haya unayo hoji yana impact gani ? Umeacha mambo muhimu aliyo andika unakuja kosoa jambo dogo saana asee
Broo nakuhukumu hapahp ww ni

Sent from my VFD 200 using JamiiForums mobile app


Stupid thinking. Hao wachaga wanaofungua biashara kila kona mtaani kwako wana elimu gani special? Think outside the box. Kama mmeamua ku-embrace capitalism, take it whole. No execuses. Marekani wana-outsource from allover the earth, if you think you,re qualified enough, why not go compete with them! Kama kina Mataragio waliweza, unakwama wapi wewe?

Unajua namba ya wataalamu wanaofanya kazi nje ya nchi graduates wa UDSM?! I am not talking about these so called vyuo vya kata. Talk about UDSM.


Ndugu kutofautisha R na L sio tatizo la Elimu ni tatizo la kikabila.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,244
2,000
Ndugu kutofautisha R na L sio tatizo la Elimu ni tatizo la kikabila.


Nije kwenye Mada:

Mkuu kubadilisha hilo Ombwe itatuchukua miaka mingi sana ijayo hasa kwa hawa vijana tulionao kwa sasa hivi. ( Vijana wanapewa nafasi ya kuongea na Rais wanaishia kusema yaleyale ya kusifu na kuabudu )

Tanzania kama Taifa tuliamua kuwekeza kwenye propaganda na matumbo ya watu.

Mf: kuna Nchi ilikuja Tanzania kuchukua mbegu za mafuta ya kupikia na leo ndio nchi inaongoza kwa kuuza hayo mafuta Duniani sisi tuliotoa mbegu bado tuna uhaba wa mafuta tena wa kutisha.

PENDEKEZO
Tanzania iache haraka sana kuwekeza kwenye Siasa na propaganda za kisiasa ambazo hazitoisaidia Nchi badala yake iwekeze kwenye ujuzi na usawa wa kimaslahi.
Tatizo ni CCM mkuu hakuna kingine
 

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
5,516
2,000
Hizo kombi ulizotaja si kwamba hazifai. Ndani yake tunapata watafsiri lugha, wanasiasa, wanahabari, wanamazingira, wanasheria nk.
Tatatizo la elimu tz halitokani na kombi bali falsafa yake mfano elimu ya kujitegemea.
Ni vpi elimu inamtayarisha mtoto kuyakabili mazingira yake. Hatakama ni pcb, pcm nk. Wazo kuu si ajira bali kutatua matatizo katika jamii na mazngira.
Kwa hivi, elimi bora ni ile inayomfungamanisha mlengwa na mazingira yake ili aweze kuendelea. Haijaalishi ni somo gani bali mantiki gani.
Mfano tunajifunza mapinduzi ya viwanda England je tunachokipata kinasaidia nini, labda kuna vitu tutafanya kupitia haya, mfano ujenzi wa miundo mbinu kama kichocheo cha ukuaji wa viwanda.
So, hakuna kombi mbaya bali kusudio ni nini. Outcome ni nini. Main philosophy!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom