The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,452
- 17,156
Jana nilikuwa naongea na bwana mdogo anafanya mitihani ya wahasibu ya CPA mbayo inaanza jumanne. Bwana mdogo amefanya hii mitihani muda mrefu sasa jana namuuliza unamaliza lini mbona kila mara unarudia rudia, dogo akajitetea kwamba kutokana na shughuli zake huwa anakosa muda wa maandalizi vizuri ya mitihani lakini akaniambia kitu kilichonishangaza.
Dogo akasema alipofaulu mtihani wa term hii basi mwakani mwezi wa 2 atanunua mitihani. Nikamuuliza kununua kiaje, akasema bodi ya uhasibu, NBAA imeanzisha utaratibu wa mitihani ya katikati ambayo gharama yake ni kubwa ila hakuna kushindwa/fail. Kwamba atajitoa mhanga alipie mitihani 2 milioni 1.1 ili afaulu kwani mitihani hiyo ya Mid sessions ni kama vile NBAA huwa wanawauzia kwa bei kubwa.
Akaniambia kwa sasa ni wewe kuchagua, ufanye mitihani ya kawaida ya ratiba za board kwa mwezi 5 na 11 kwa bei ndogo ya laki moja na nusu kwa mtihani ama ununue mtihani kwa mid sessions kwa mtihani mmoja kwa laki 5 na elfu hamsini ufaulu.
Dogo anasema hii ya katikati hata hihitaji kuwa maandalizi mazuri ili ufaulu, unafaulu tu kwani ni rahisi sana ndio maana wanasema huwa ni kama inauzwa ila hii ya ratiba za kawaida kama huna maandalizi ya kutosha hutoboi, mitihani migumu sana.
Dogo anasema matajiri wengi ana watoto wa matajiri ama mwenye uwezo sasa hawafanyi ya kawaida, wanafanya mid sessions ambako money talks, unalipa hela nyingi unakuwa na uhakika wa kufaulu, hii ya ratiba za kawaida ndio wanafanya choka mbaya wengi kwani bei yake ni rahisi ila inahitaji msuli mkubwa.
Kwamba kaa sasa ni wewe kuchagua utumie Pesa yako uwe na uhakika wa kufaulu ama utumie muda wako kujisomea na kulipa kidogo ila hakuna uhakika wa kufaulu mitihani.
Siku Hizi taaluma Tanzania zimekuwa ni hovyo hovyo tu, juzi mtihani wa madaktari umevuja wazi kabisa wamama walikuwa wanafungia vitumbua kabla hata mtihani haujaanza.
Kwa hiyo leo hii ukisikia mtu ana CPA wala usishtuke, siku hizi zinauzwa na kununuliwa kisheria kabisa.
Elimu ya Tanzania haitaisha vituko.