Elimu ya Tanzania chini ya Serikali ya CCM na dhana ya kujiajiri, vinakwepana. Kuna dosari sehemu

Lugumya

Senior Member
Apr 26, 2021
183
1,093
Nianze kwa nukuhu ya Bwn.Lewis Carroll, ambaye alipata kunena kwamba “If you don't know where you are going, any road will get you there”. Kwa maana kwamba kama hujui unakoenda, njia yoyote itakufikisha!

Nimeamua kutumia kunuhu hiyo kuiangazia elimu inayotolewa nchini Tanzania kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vikuu, na kujiuliza hivi ni kweli tunajua tunakotaka kwenda kama Taifa? Akili inaniambia bado hutujui tunaenda wapi?

Elimu yetu haiakisi uhalisia wa mahitaji ya soko la sasa, wala haituwezeshi kupambana na mazingira yetu. Ipo ipo tu, ni kichaka cha kupotezea muda na kujipa nafasi ya kutoka umri wa miaka saba hadi 22.

Ukichunguza vizuri utagundua kuwa elimu ya Tanzania bado imejikita katika kujua kuhesabu, kusoma na kuandika (Maintaining the 3Rs). It is more of storytelling and never for liberation or self-employment. Unaanza madarasa ya awali ukijikita katika katika kujua kusoma. Ukishajua kusoma utarundikiwa hadithi za Pazi na Jogoo,Mfalme ana mMasikio mMarefu Kama ya Punda, Kibanga Ampiga Mkoloni, Ndoto za Kimweri na Mua Uliozamisha Meli.

Ukimaliza hapo utapata A zako kadhaa, na kwenda Sekondari, ambapo utapambana na Watoto wa Mama Ntilie, Unanswered Cries, Mine Boy, The Great Ponds, the River Between, Chimurenga War, Samouri Toure Resistance, Mabara the Farmer na Hawa the Bus Driver!

Inafika sehemu mwalimu anakuchorea ramani ya Mandika Empire, na kukuonesha mji wa Bisandugu na namna jeshi la Samouri Toure lilivyokuwa imara kupambana na Wafaransa. Hapo nimeruka habari za Mwenemtapa empire, Tunkamanini, Sundaiata Keita na Mansa Kankani Musa.

Mwalimu ataingia darasani amechomekea balaa, na wanchoma kumoyo bila daftari au kitabu, atatiririka wee,na mwisho wa siku ataoekana kipanga na mwenye maarifa ya kutosha katika eneo lake la utendaji. Lakini mwisho wa siku story zake hizo hazitkokuwa na msaada wowote katika maisha yako. Hazikupi nafasi za kujiajiri au kupambana na mazingira yako. Story hizo hazikupi nafasi ya kujua kuwa mazao yako yakidumaa shambani ufanyeje maana sayansi Kilimo ilishaonekana haifai mbele ya Manenge na Mandawa.

Kupitia hizo stori stori, utapimwa na mtihani wa mwisho na baada ya hapo utalazimika kwenda kidato cha tano, ambapo kama ni mwanasayansi utafundishwa histori ya kemia, histori ya fikizia,na histori ya Biolojia.

Wengine watapigwa Betrayal in the City, I will Marry When I want au Pesa zako zinanuka, au Vuta ni Kuvute na kukutabasamisha namna akina Maua walivyotoa uroda. Kicheko kitatamalaki darasani na kukuacha kapa au solemba.

Kule wanasayansi wataambiwa watafute specimen, na wanapigwa alternative to practical. We uliona wapi practical ikawa na mbadala unaoitwa alternative to practical? Uliona wapi?

Basi bana, utaendelea chuo kikuu na kupata kachumba kako pale mabibo hostel. Utakaa kisomi pale mdigrii tree na kulumbana kwa hoja na kusubiri mhadhara wa profesa au Daktari. Akifika ataanza, na course outline, na mwisho wa siku atakwambia lengo la programu hii ni kukufanya uwe mtengeneza ajira na si msaka ajira.

Moyo unaanza kufarijika na kujua hapa sasa, naenda kufundishwa namna ya kutengeneza batiki, namna ya kutengeneza viberiti, namna ya kufufua viwanda amabavyo vilihabriwa na serikali ya Chama cha Mapinduzi. Lakini mambo yakianza sasa, unakutana na Kinjekitile Ngware mkazi wa Ngalambe, unakutana na decolonization process, unakutana na nadharia mbalimbali za kukusaidia kupigia story vijiweni na kujipambanua kuwa umeenda kidato, na mwisho wa siku hapa napo unatoka kapa!

Wale walioenda ngazi za kati watakutana na CBET(Competence Based Education and Training) ya NACTE, hapa utaambiwa lengo ni kujenga umahiri kwa kuleta mazingira ya kazi katika eneo kufundishia na kujifunzia. Wapi wewe? CCM bana.

Utayasubiri hayo mazingira yaje, lakini utaishia kusikia unachukua Related Task (hizi ndo competence), unatreat SELO (Sub-enabling Learning Outcomes) baada ya hapo kichwani utajaziwa minadharia tu lakini hizo competence hutoziona, na wala mazingira ya kazi utayaona katika eneo la ujifunzaji.

Masomo yenyewe hayawi linked na uhalisia kwa sababu wanaofundisha tu hawajawahi kuwa katika maeneo ya utendaji. Ni wageni wa kazi,hizo, watazifundishaje? Uongo mtupu!

Mambo mengi tunayosoma ni mambo ya ziada ambayo mtu anaweza kusoma kama leisure. Mistory nayo ni kumfundisha mtu na kumpima weledi wake? Kweli ? inasaidia nini sasa? Yaani Things Fall Apart, au The Lion and the Jewel, inisadie nini katika maisha jamani. Si kupotezeana muda kweli?

Nafikri tatizo ni Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Hili ndiyo jipu kubwa, ambalo inabidi litumbuliwe ili kipatikane chama au mgombea binafsi atayeweza kuja na mtazamo mpya wa utekelezaji wa dhana ya kujiajiri. Akisimama Job, utasikia ajira hakuna, jiajirini, lakini hapo hapo anajua kuwa wakati mwingine kunahitajika mtaji.

Na fedha ambazo zingeelekezwa kwenye mitaji kwa vijana, ndo wanajilipa matibabu huko India, ndo wanawalipa Uviko-19 kule bungeni, ndo wanajilipa mafuta, posho za vikao, mishahara mikubwa na posho za kujikimu. Wanaishi dunia ya peke yao hawa miamba ya CCM.

Lakini si mtaji tu bali fikra zitengenezwe kutoka shule za awali. Serikali ya chama imeng’angana na Siku ya Gulio Katerero, Shona-Ndebere resistance na Alternative to practical ambavyo havina uhsusiano na ubunifu ama maarifa ya kusaidia kujiajiri.

Chama hiki kinastahili kuwajibishwa, ili tuweze kupiga hatua, au kinatakiwa kifanye mapinduzi makubwa katika elimu yetu kwa kuja na elimu za ujasiriamali kuanzia shule za msingi, ikiwemo upatikanaji wa vitendea kazi vya kuigizia.

Ukisoma Ilani, ina matamko ya kisiasa kama vilivyo vitabu vya Kiu ya Haki, au Three Suitors: One Husband, au A man of the People. Full chief Nanga, full Mangungo wa Msovero. Wamejigeuza kuwa wakoloni weusi, dhidi ya ndugu zao wenye rangi kama yao. Hiki ndo chanzo cha matatizo yote ya ajira hapa nchini. tTujitathimini dhidi ya chama hiki. Maana mzizi wa tatizo unaanzia hapa.

Pili, Mitaala inayotumika kufundishia imepitwa na wakati. Bado ni ya Kikoloni na haiakisi mahitaji ya soko la sasa. Kimsingi haina majawabu ya kuondoa umasikini kupitia kujiajiri au kuajiriwa.

Mfano, rafiki mmoja alienda China, alivorudi alinionesha kifaa kimoja fulani hivi, ambacho alisema kimetengenezwa na mwanafunzi wa darasa la pili China, wakati kifaa hicho hicho professor wa physics aliyesoma Tanzania hadi mwisho hawezi kukitengeneza (Sijadharau maprofesa wetu, nina shida na mitaala inayowandaa).

Mitaala hii inatoa maarifa tu, lakini haitoi umahairi kwa wahitimu kutenda. Imejaa vitu visivyo vya msingi, katika utatuzi wa changamoto tulizo nazo kama Taifa, bali ina mambo mepesi mepesi ambayo kimsingi hayana msaada kwa wahaitimu.

Ndo maana utakuta kibanda cha betting kimejaa vijana wengi kwa kuwa hawana maarifa na umahairi wa kutosha japo wana, Astashahada, Stashahada, shahada ya Kwanza au shahada ya Umahiri. Walichofundishwa huko ni vichekesho.

Wizara ya elimu tafadhalini sana, na timizeni wajibu wenu. Sasa hivi tuko katika uchumi wa kati wa viwanda, lakini mitaala haijajielekeza kuwaandaa vijana kupata ujuzi utakaowasaidia kushiriki katika uchumi huo. Viwanda vyenyewe kikwazo namba 1 hapo juu (Serikali ya chama cha Mapinduzi) imeshaua karibia vyote. Na watakwambia huku wamekodoa macho kuwa vyerehani vitatu ni kiwanda. Wasomi wetu tafadhali, shaurini, tuweze kupiga hatua. Vingenevyo tutawalaumu vijana bure wakati tatizo si wao.

Tujue basi tunataka kwenda wapi, ili tuikane njia tuliopita na kujisahahisha.
Nimetania, kwa kimasihara!!!
 
Nataamani wangepitia hapa ili wajifunze kitu! Ulicho andika ni ukweli mtupu! Yaani tangu enzi na enzi, mitaala yetu iko vile vile!

Ni kukaririshana tu vitu vya kijinga na visivyo na msaada wowote ule katika maisha halisi ya mtaani.
 
Kwahiyo unataka elimu ya chama gani? Kile ambacho mwenyekiti wake kaishia la nne?... au kile cha profesa mapumba?
 
Ni mshikaki wenye mfupa! I love this japo nimelewa lakini nimeelewa
 
Yatatokea wapi mabadiliko kama wanaoongoza wizara ya elimu nao wamelelewa na kukuzwa na mfumo huo? Kuna mbunge gani aliyewasilisha hoja bungeni kutaka mabadiliko ya elimu? Huu mfumo umeharibu future za wahitimu wengi wamejikuta wanafanya shughuli zisizo rasmi na kuishia kupambana na migambo ya miji. Ni mfumo mkongwe uliopitwa na wakati. Sasa hivi ni aibu kujinasibu umehitimu chuo huku huna ajira uliyoisomea, inabidi useme una elimu ya msingi ili jamii isikushangae kwa kukosa ajira huku una elimu ya juu.
 
Hivi serikali huwa inajiuliza maswali wanafunzi wanaoishia darasa la saba na kidato cha nne wanaenda wapi? Maana hawa kwa mfumo wa elimu huu mkongwe hawachaguliwi kuendelea na elimu ya juu hata kama wanaitaka na wana uwezo wa kupokea maarifa mapya, maana ni wengi.

Au ndio hao wanaoelekezwa waende VETA? Kwani wanafunzi wa shule za misingi hawawezi kujifunza ufundi tangu wakiwa msingi na wakapata stadi za kujiajiri mapema kuliko kwenda kupoteza muda kwenye masomo hata ukihitimu utakuwa bado huna sifa ya kuajiriwa au kujiajiri. Mfano mwanafunzi anafundishwa physics, chemistry na biology kwa miaka minne au sita anafanya mtihani wa mwisho anapata alama ambazo si za kuchaguliwa kuendelea kupata maarifa zaidi anatangaziwa amefeli.

Sasa hayo maarifa aliyojifunza miaka yote hiyo atayapeleka wapi? Maana hana sifa ya kuajiriwa wala kujiajiri, atakua daktari? Famasia? Maabara? Kwa sifa ipi? Maana anaonekana ana elimu hiyo nusu na haruhusiwi kuendelea ahitimishe. Basi inabidi uachane na maarifa ya pcb uwe machinga
 
Cha msingi tafuta pesa..viongozi wenyewe wanaojiita wazalendo..huwezi kuta anamsomesha mtoto wake shule za serikali..wanajua elimu hii ni ya kutengeneza mazuzu na wapiga kura.

#MaendeleoHayanaChama
 
Yatatokea wapi mabadiliko kama wanaoongoza wizara ya elimu nao wamelelewa na kukuzwa na mfumo huo? Kuna mbunge gani aliyewasilisha hoja bungeni kutaka mabadiliko ya elimu? Huu mfumo umeharibu future za wahitimu wengi wamejikuta wanafanya shughuli zisizo rasmi na kuishia kupambana na migambo ya miji. Ni mfumo mkongwe uliopitwa na wakati. Sasa hivi ni aibu kujinasibu umehitimu chuo huku huna ajira uliyoisomea, inabidi useme una elimu ya msingi ili jamii isikushangae kwa kukosa ajira huku una elimu ya juu.
Kweli mkuu mimi nimemaliza elimu ya chuo ngazi ya shahada.. ¡ Lakini eneo nalofanyia kazi nimejitambulisha kamu aliefeli kidato cha nne.. Ili nipate amani na kukwepa vidole
 
Elimu yetu ni changamoto kwa kweli, yaani haina ladha kabisa huku mtaani hususani ukizingatia mabadiliko haya ya sayansi na teknolojia yanayoenda kwa kasi sana.

Lakini pia, sisi vijana kweli tupo serious kutaka kujifunza na kuujua vizuri ulimwengu na kutatua changamoto zilizopo? kwasababu siku hizi mtu anaweza endelea kujifunza online mf. YouTube videos, Google nk, je wangapi wanafanya hivyo?

Asilimia kubwa wapo kufuatilia udaku wa Diamond na kina Messi na Ronaldo huko, sasa kwa hivyo kweli tutafika?

Haya watu wanasomea vitabu? Hapa nazungumzia vitabu vyenye dira nzuri Kama vya 'Think and grow rich' , 'Rich Dad, poor Dad' nk, ama tupo busy kuangalia movies za watu wanapaa na kuchinjana tu!.

Ndiyo serikali inaweza kulaumiwa, Ila na sisi vijana bado hatujasimama ktk msimamo wa kwamba tupo tayari kupambana na huu ulimwengu wa karne ya 21.
 
Cha msingi tafuta pesa..viongozi wenyewe wanaojiita wazalendo..huwezi kuta anamsomesha mtoto wake shule za serikali..wanajua elimu hii ni ya kutengeneza mazuzu na wapiga kura.

#MaendeleoHayanaChama
Umenena vyema Kiongozi! Kula likes 10
 
Badala ya kusoma mavitabu kama Things fall apart na Three Suitors kwenye kiingereza. Tuweke vitabu vya kumfunza mtu kitu fulani na kiingereza kwa wakati mmoja. Kitabu kama The Richest man in Babylon nk. Elimu yetu ni changa, bado ni ya mkoloni ya kutaka kutengeneza makarani na si watu wenye uelewa wa kuweza kujiajiri.

Mbaya zaidi ni kuwa zama hizi A internet zimekuja kuwaumbua wasomi wetu jinsi walivyo vilaza.
 
Badala ya kusoma mavitabu kama Things fall apart na Three Suitors kwenye kiingereza. Tuweke vitabu vya kumfunza mtu kitu fulani na kiingereza kwa wakati mmoja. Kitabu kama The Richest man in Babylon nk. Elimu yetu ni changa, bado ni ya mkoloni ya kutaka kutengeneza makarani na si watu wenye uelewa wa kuweza kujiajiri.

Mbaya zaidi ni kuwa zama hizi A internet zimekuja kuwaumbua wasomi wetu jinsi walivyo vilaza.
Hahahaha, vilaza! Vilaza!
 
Back
Top Bottom