Elimu ya Sasa ni siasa au inaendana na wakati wetu wa sasa?

mwanzo wetu

JF-Expert Member
May 4, 2014
1,581
461
Wananchi Wilayani Kasulu mkoani Kigoma wanaendelea kuchangishwa Madawati mashuleni, baadhi ya wananchi wenye wanafunzi katika shule ya Msingi kidyakidyama wilayani Kasulu wamesema nini maana ya Elimu bure huku wengine wakidai ni wajibu wao.

Mimi nashauri pengine neno Elimu bure libadilishwe litafutwe neno lingine ili kuondoa mkanganyiko kwa wazazi wa watoto au wananchi.
 
Elimu bure ina maana gani

1. Elimu bila Ada !?

2. Elimu bila michango na Ada
 
Sasa apa lipi neno serikali pengine litumike ili kuondokana na mkanganyiko huu pengine.
 
Elimu bure maana yake ni elimu isiotija hiyo ndio maana halisi kwa muktadha wa siasa za Magufuli kwa sababu kama michango tunatoa kama kawaida mara hela ya ujenzi wa shule mara sijui chakula shuleni sasa ni elimu bure gani hii? Hii ni bure bure kichwani yaani hamna tija.
 
Elimu bure maana yake ni elimu isiotija hiyo ndio maana halisi kwa muktadha wa siasa za magufuli kwa sababu kama michango tunatoa kama kawaida mara hela ya ujenzi wa shule mara sijui chakula shuleni sasa ni elimu bure gani hii? hii ni bure bure kichwani yaani hamna tija
Lakini imesaidia kwa kiasi kikubwa ila shida ni baadhi ya wazazi kulalamikia hili la Michango midogo midogo.
 
Lakini imesaidia kwa kiasi kikubwa ila shida ni baadhi ya wazazi kulalamikia hili la Michango midogo midogo
Imesaidia nini mkuu? na wakati gani? Imesaidia kuongeza idadi ya graduates kitaani ambao hawana ajira na hawajawezeshwa kimfjmo ili wajikwamue?

Mimi ningemuunga mkono angefanya reformation ya mitaala, hatuwezi kuendelea kutumia mitaala ambayo ni completely unuseful. Tunawajaza wanafunzi content ambazo ni useless. Tubadili mitaala ndipo hata tukikazia hoja ya elimu bure itakuwa na tija.
 
Imesaidia nini mkuu? na wakati gani? Imesaidia kuongeza idadi ya graduates kitaani ambao hawana ajira na hawajawezeshwa kimfjmo ili wajikwamue?? mimi nkngemuunga mkono angefanya reformation ya mitaala, hatuwezi kuendelea kutumia mitaala ambayo ni completely unuseful. Tunawajaza wanafunzi content ambazo ni useless. Tubadili mitaala ndipo hata tukikazia hoja ya elimu bure itakuwa na tija.
Kubadili mitaala ni jmbo gumu saana kama unakumbuka kulikuwa na mchakato wa watoto kuishia darasa la sita pekee ila now mambo yapo kwapani.
 
Kubadili mitaala ni jmbo gumu saana Kama unakumbuka kulikuwa na mchakato wa watoto kuishia darasa la sita pekee ila now mambo yapo kwapani
Ila tukutaka kuboresha elimu tubadilishe mitaala ni heri elimu iwe ya kulipia pesa ila iwe productive sio kama hivi sasa mtu anamaliza digrii akirudi mtaani anakuwa mpya.
 
Wananchi Wilayani Kasulu mkoani Kigoma wanaendelea kuchangishwa Madawati mashuleni, baadhi ya wananchi wenye wanafunzi katika shule ya Msingi kidyakidyama wilayani Kasulu wamesema nini maana ya Elimu bure huku wengine wakidai ni wajibu wao.

Mimi nashauri pengine neno Elimu bure libadilishwe litafutwe neno lingine ili kuondoa mkanganyiko kwa wazazi wa watoto au wananchi.
Wabongo mnapenda vitu vya bure! Sasa hata dawati tu la kukalia mtoto wako, unalalamika.

Mbaya zaidi Jumla ya hiyo michango yote unaweza kukuta hata laki haifiki!! Toeni mchango wa madawati bhana ili watoto wenu wasikae chini.

Kwa hali hii mkitaka mfanyiwe kila kitu, mnategemea yule Rais wenu wa wanyonge atamaliza kweli ile miradi yake yote kwa wakati?
 
Elimu Bure imesaidia sana, ila naomba suala la watoto wa sekondari kutoka shuleni saa 11 jioni , afu waanze kugombania dala2 na wafanyakazi wafike nyumbani saa 1; 40 jioni, afu hiyo ni kwa ku chukulia kwamba mtoto amechangia chakula, wazazi walioshindwa kuchangia chakula, watoto wao wanashinda na njaa kama wafungwa na ni wengi, ( kama hamuamini - fuatilieni shule zilizo nje ya manispaa ) kwa nini watoto wasitoke shuleni saa 8 mchana , mtoto apumzike afu afanyie mazoezi yale aliyosoma ? mbona sisi wengine tuliweza na hatuoni shida ya hili suala ?
 
Back
Top Bottom