Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,272
Sisi tuliosoma enzi za awamu ya kwanza, enzi za Chama kushika hatamu, tunakumbuka elimu ya sanaa na ufundi. Hili lilikua somo kamili, kulikua na walimu waliohitimu mafunzo hayo.
Shule zilikua na karakana, wavulana walifundishwa useremala (labda nimekosea) na uwashi. Hata ujenzi wa madarasa na majengo ya shule baadhi ya kazi zilifanywa na wanafunzi wa kiume kuanzia darasa la tano, sita mpaka la saba.
Wasichana tulifundishwa kushona, mara nyingi mwalimu alikua ni wa kike. Pamoja na kuwa cherehani ilikua moja au mbili lakini kila mtu alipata nafasi ya kujifunza basic knowledge ya kushona.
Nimekutana na raia wengi kutoka nchi zilizokua za Soviet Union. Wanaume wote wa nchi hizi ni wajenzi wazuri. Waliniambia kuwa hii ni sehemu ya elimu nchini kwao. Hata asiyeenda chuoni anakua na ujuzi wa kuanzia maisha.
Hii dhana Mwalimu Nyerere alituanzishia. Ikiwapendeza mnaweza kuirudisha mashuleni.