Elimu Ya Ngono Kwa Watoto. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu Ya Ngono Kwa Watoto.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Feb 20, 2009.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Feb 20, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  SEMINA YA ELIMU YA NGONO KWA WATOTO KUANZIA MIAKA MITANO MASULENI (UK)​

  Shule za msingi hapa zimo mbioni katika kuanza kusomesha somo hili la ubaradhuli kuanzia watoto wa umri wa miaka mine hadi kumi na moja.

  Tayari shule 14 zimo katika majaribio kuwasomesha watoto kwa kutumia vitabu vya hadithi za kitoto kama “King and King” kinachozungumzia mtoto wa mfalme aliyekataa kuoa watoto wa kifalme watatu na hatimaye kupendana na mtoto wa kiume mwenzake. “And Tango Makes three” ikiwa ni kisa cha penguin wa kiume wawili waliopendana katika hifadhi moja ya wanyama New York Marekani. “Spacegirl Puke” ni kitabu kinachozungumzia mtoto kidogo wa kike akiwa na “mama” wawili.

  Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, mradi huu utasaidia kuweza kupata njia nzuri za kuweza kulisomesha somo hili mashuleni. Lengo la mradi huu, kwa mujibu wa kauli ya Dk Elizabeth Atkinson, ambae ni mwalimu wa soshiolojia na utafiti wa kielimu katika University ya Sunderland, ni kuzisaidia shule kuweza kufikia viwango vilivyowekwa na muswada wa sheria ya Equality Act ambayo inazitaka taasisi zote zinazotoa huduma kwa jamii kuhakikisha matakwa na mahitaji ya wasagaji na mabaradhuli(lesbians and gays) yanatimizwa.

  Sheria hii inaweza kuzibana shule zitakazoshindwa kutimiza masharti kushitakiwa kwa kukiuka maagizo ya muswada huu.Muswada tayari umeshapitishwa na Bunge na utaanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 30 Aprili 2007.

  Karibuni tume ya pamoja ya haki za binadamu inayojumuisha wabunge ilitoa mapendekezo kwamba shule zote za kidini nchini kulazimishwa kubadilisha mitaala(curriculum) ili iendane na mipango hii ya serikali. Hata hivyo ripoti hii imedai kwamba taratibu hizi hazitozuia wanafunzi kusomeshwa kwamba kuna baadhi ya dini zinasema kwamba tabia hii ni haramu na dhambi lakini shule zisiruhusiwe kusomesha itikadi za dini fulani tu kama ndio za kweli.

  “Tahir Alam ambae ni Kamishna msaidizi wa kamati ya elimu ya Muslim Council of Britain ameeleza kusikitishwa kwake kwa kusema; “ Mpango huu ni kinyume kabisa na mafundisho ya dini yetu ya kiislamu hivyo kila mzazi muislamu atasikitishwa na mpango huu”

  Na Dr Majid Katme, msemaji wa Islamic Media Council UK anasema;” Wazazi na viongozi wa dini zote wamestushwa na kuingizwa vitabu hivi katika mitaala ambavyo vitafundisha na kuutangaza ubaradhuli kwa watoto wadogo ambao hawana hatia yoyote.”
  “Sote tunajua watoto huzaliwa na wazazi wa jinsia mbili ya kike na kiume sasa kuwafundisha watoto kinyume na hivyo ni kuwachanganya na si kuwasaidia. Watoto wadogo kama hawa kusomeshwa kuufahamu na kuukubali ubaradhuli kama ni sehemu ya maisha ni kukaribisha hali isiyo kawaida kitabia na kimaadili”

  Sijui wazazi wa jamii yetu ya Kiswahili tumejiandaa vipi na kuikabili hali hii ambayo tayari kuingizwa katika masomo na hivyo kupewa kazi ya ziada wazazi kuanza kuwaelimisha watoto wetu kwamba tabia hii si miongoni mwa tabia za kiislamu.

  Sijui tutakuwa na uwezo wa kuweza kukabili mtihani huu mzito kwani mbinu za kiusomeshaji huwa za kitaalamu sana mashuleni na mbinu za kuikabili hali hii itabidi ziende sambamba na mbinu zinazotumika kuufikisha ujumbe huu kwa jamii yetu. Vyenginevyo tayari tutakuwa tumeonesha dalili na alama za kushindwa na watoto wetu kukosa dira na mwelekeo sahihi. Haitotosha tu kumwambia mtoto kwamba ubaradhuli ni haramu au dhambi wakati shule anapikwa na kupewa sababu na hoja za kuhalalisha jambo hili.

  Tukumbuke mashuleni, mitaani na kwenye TV(ambapo muda mwingi wa watoto wetu hutumika), ubaradhuli na usagaji unazungumzwa bayana na kwa wengi unakubalika na hivyo watoto wetu kuathirika na kuwa na masuala mengi ya kujiuliza kuliko majibu. Majibu haya yanatarajiwa kutoka kwa wazazi kuweza kuwafahamisha kwa njia na mbinu nzuri ya kuweza kufahamu vyema kwa nini uislamu umeharamisha hali hizi ambazo ni kunyume na maumbile. Majibu haya yanatarajiwa kutoka kwa jamii na viongozi kuwaelimisha wazazi kwa kadri ya uwezo wao kukabiliana na mbinu hizi ambazo kila kukicha zinayafanya maisha yetu katika nchi hizi kuzidi kuwa magumu.

  Ikiwa hatutokuwa tayari kwanza kuunganisha nguvu na kufuatilia kwa karibu wanayosomeshwa watoto wetu na kuweza kukabiliana nayo kwa kila mbinu kama kuwasilisha wasiwasi na duku duku letu kote kunakohusika basi tujiandae kuilea jamii itakayojaa mabaradhuli na wasagaji miongoni mwa watoto wetu ambao ni wepesi mno kuiga mambo huku wakiendelea kuathirika na kusomeshwa kwamba hali hii ni sehemu tu ya maumbile ya binadamu.
  Waislamu na wazazi tupooo!
  Wabillahi Tawfiyq
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  wizi mtupu....! haya wanaokumbatia u-magharibi na uarabu wafunzeni wana wenu wawe na wapenzi wa jinsia zao......!
   
 3. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sasa X-Paster tuko pamoja!Ni kweli kabisa kwamba somo hili ni la kibaradhuli,na mimi naongeza linatekelezwa by orders from the devil himself.Oh!Mungu aiepushe mbali Tanzania na ushenzi huu.

   
 4. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haitanishangaza kuona hapa TANZANIA viongozi wetu wakachukuwa hatuwa kama hiyo na kama ni kweli huko UK wanafanya hivyo basi hiyo itakuwa ndio sababu kwa viongozi wetu kuleta hali hiyo hapa bila kuzingatia kuwa sisi ni wafrika mila na tamaduni zetu hazikubaliani na hao wazungu kwa hali yoyote ile na ndioleo tunaona madhara katika jamii na koo zetu hatujuwi wapi tunakwenda
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Feb 22, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hata mimi nakubaliana nanyi, ila tufahamu kuwa viongozi wetu kwa kupenda sana kwao kuomba omba misaada ya kiuchumi toka nchi za ulaya na marekani... itafikia kipindi watalazimika kufuata hiyo hiitwayo demokrasia kwa kutakiwa kuwakubali hawa mabaradhuri na hata huko mashuleni vijana wetu watalazimishwa kufundishwa kuwakubali na kuwaona kuwa ni sawa tu kwa mtu kuwa baradhuri... kwani kwa kufanya hivyo ndio itaonekana kutimiza haki za binadamu za kujichagulia vile anayo penda hawe.
   
 6. M

  MohamedSalum200 Member

  #6
  Feb 22, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii yote inatokana na utandawazi na nchi kukosa heshima anyway tunaomba Tanzania isitokee Mungu atuepushe
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mnaogopa nini. Asubuhi utaona kitoto cha kiume kinatoka nje kwenda kujisaidia uku kimesimika vitu. hivyo hata mtoto anazo hisia za ngono.
   
Loading...