Shinto
JF-Expert Member
- Dec 6, 2010
- 1,781
- 96
Wakuu,
Kwanza nianze kwa kutangaza "interests"! Mimi nimesoma shule za Kanumba mwanzo mwisho!.
Sasa jana nilibahatika kuona paper ya jiografia ya dogo moja anayesoma hizi shule zenu za kisasa 'english medium'.
Yeye anajiandaa kumaliza darasa la saba mwaka huu, sasa nikaona swali nikahisi alikosa kwa sababu ya 'mabomba' tu kwenye lile swali. Nikajitahidi kutafsiri, nikamuuliza kwa kiswahili swali lile lile akapatia!!!!!!!.
Kutoka hapo, nikaamini kuwa tutake tusitake kizungu ni kikwazo kwa hawa watoto. Yaani katika somo, 50% inapotezwa kwa sababu ya ugumu wa lugha, hasa ikiwa mtoto anarudi nyumbani anakoongea kiswahili au anakaa boarding za magumashi (wanazoongea kiswahili watoto wakiwa peke yao).
Swali hapa, tuifanye elimu ya iwe kiswahili tuu, au kiingereza tuu? Tukichagua hilo la pili, itabidi tuifanye kiingereza kuwa lugha ya kwanza kwa mawasiliano hata huku uswahilini!
Kwanini wale wanaozungumzia kiwango cha elimu kushuka, hawashupalii hili?
Nawasilisha!