Elimu Ya Mazingira Ni Muhimu

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
25
Uchafuzi wa mazingira unasababisha athari nyingi katika jamii. Uchafuzi huo wa mazingira unatokana na kutupa takataka ovyo katika sehemu zisizoruhusiwa kama barabarani, kwenye mazingira ya nyumba zetu na kadhalika. Wazalishaji wakubwa wa takataka ni viwanda, tasisi za elimu (shule na vyuo), hospitali, tasisi za dini n.k. Ili kuepuka athari hizo elimu ya mazingira ni muhimu sana.

Mabadiliko ya tabia ya hali ya hewa duniani ni miongoni mwa athari za uchafuzi wa mazingira. Hali ya joto imeongezeka duniani, barafu katika milima imepungua au imekwisha. Mlima Kilimanjaro kwenye miaka ya 1970 na 1980 ulikuwa umefunikwa na barafu kwa kiasi kikubwa, kwa sasa barafu imeisha. Hii imetokakana na athari za uharibifu wa mazingira. Maji katika bahari yameongezeka ina maana kina cha maji baharini kimepanda, visiwa vingine vimemezwa na bahari.

Athari nyingine ni kuibuka kwa magonjwa kama magonjwa ya ngozi na kansa. Haya yote yanatokana na maendeleo yasiyokuwa endelevu (non-sustainable development)

Tutunze mazingira kwa faida ya wote. Mazingira yatunzwe kwa kizazi hiki na kijacho. Kila mmoja akiwa mlinzi wa mwingine/mwenzake katika matumizi ya mazingira nadhani tutafanikiwa kupunguza athari za binadamu katika mazingira na kupunguza magonjwa ya mlipuko na kuyahifadhi mazingira yetu na kufurahia matunda ya mazingira mazuri kwa kizazi hiki na kijacho. Elimu ya mazingira ni muhimu kwa kila mtu.
 
Asante ndugu Mhache kwa kuhamasisha elimu ya mazingira. Kwa maoni yangu, serikali bado haitilii mkazo elimu hii kwa vitendo. Pale Mbagala Mission (kati ya Mtoni-Mtongani na Mbagala Rangi 3) kuna kiwanda cha nguo KTM. Kiwanda hiki kinatoa pollution: water, air and environmental pollution.

Kiwanda hiki kinatirisha maji yenye kemikali kwenye mto unaoelekea baharini. Zamani ulikuwa na samaki lakini siku hizi hamna. Hayo maji yanapita karibu na makazi ya watu. Kwa sasa kuna utengenezaji wa daraja unapopita huo mto.

Ukipita utaona kuwa mabomba ya maji yanayotumiwa na binadamu yamepita karibu na maji hayo yenye kemikali. Mabomba mawili pando zote mbili za barabara yamegusa hayo maji na kama mto utaongezeka ujazo, hayo maji yatafunika hayo mabomba kabisa.

Lakini pia, kuna bomba moja lililo juu kidogo maji ya kunywa yanadondoka chini. Hii inaonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa hata maji hayo ya kemikali kuweza kuchanganyikana na maji ya kunywa na hivyo kuhatarisha afya za wakazi wa Mbagala Mission/Mbagala. Ina maana serikali hailioni hili (yaani viongozi au mamlaka husika)?

Je, wakazi wa Mbagala Mission/Mbagala Rangi Tatu 3 watakapodhurika kutokana na athari za kemikali hizo za KTM nani atakuwa responsible? KTM au Mamlaka ya Maji Safi na Taka au vyote 2? Kweli inasikitisha kuona pesa zinapewa kipaumbele kuliko afya za watu!
 
Uchafuzi wa mazingira unasababisha athari nyingi katika jamii. Uchafuzi huo wa mazingira unatokana na kutupa takataka ovyo katika sehemu zisizoruhusiwa kama barabarani, kwenye mazingira ya nyumba zetu na kadhalika. Wazalishaji wakubwa wa takataka ni viwanda, tasisi za elimu (shule na vyuo), hospitali, tasisi za dini n.k. Ili kuepuka athari hizo elimu ya mazingira ni muhimu sana.
.

Mhache,

Mkuu Umenikumbusha kitu ambacho siku zote ninakiwaza.

Ni hii tabia ya magari yaendayo Safari za mikoani kutoka Dar au kuja Dar.

Nitaongelea Mabasi yatokayo Mbeya huku ambako ninatoka. Ukipanda basi lolote toka Mbeya ukivuka tu Mzani wa Makambako kwa mbele kidogo kuna Traffic na hapohapo watu hupatumia kama sehemu ya kuchimba dawa au kwa maneno mengine sehemu ya kujisadia. Lengo ni kujisaidia haja ndogo lakini abiria wengine huitumia kwa haja kubwa. Utasikia Kondakta anasema haya jamani tunasimama hapa kuchimba dawa.

Ni sehemu inajulikana sana hata wafanyabiashara ndogo ndogo wanajua kuwa mabasi yatasimama, kwanza kwa kukaguliwa na polisi na pili kwa kuchimba dawa (Abiria kujisaidia). Siku zote huwa ninajiuliza kwa nini Serikali iko kimya kwa huu uharibifu wa mazingira unaondelea sehemu kama hizi. Kwanza sio mazingira pekee yanayoharibiwa bali hata afya za abiria ziko mashakani.

Kwa mfano, wafanyabiashara ndogondogo wanauza maji, sambusa, biscuts, etc. Kwa kuwa abiria anakuwa ameamka asubuhi bila kupata chochote basi utakuta baada ya kujisaidia ananunua chochote kama kifungua kimya. Pale hakuna bomba la maji na hawa jamaa nao wanashika hela na wakati huo huo wanawahudumia abiria. Ukipita wakati wa mvua utaona ni jinsi gani ile sehemu ilivyo na hatari iliyopo kiafya na kwa mazingira.

Hali iko hivyo hivyo kwa basi linaloondoka Dar asubuhi kwenda Mbeya, mara baada ya kuvuka njia panda inayoenda Mzungu University kuna sehemu maarufu sana kwa kuuza miwa. Basi utasikia Kondakta anasema jamani tutasimama hapa kuchimba dawa. Same story kama pale Makambako, mchanganyiko wa biashara na kujisaidia bila bomba la maji.

Ukiangalia takataka sinavyotupwa maeneo haya utajiuliza kama kweli tuna Waziri wa mazingira. Ukiangalia jinsi vyakula vinavyouzwa sehemu ya chooni, utajiuliza kama kweli tuna waziri wa afya. Chakufurahisha hapa Waziri wa Afya anatokea Mbeya kwa hiyo kama anapita humu JF atakubaliana na mimi ninayosema. Yes, Prof Mwandosya alisha hama wizara ya Mazingira, lakini na yeye analijua hili.

Mwisho ninapenda kutoa mapendekezo yafuatayo.

a) Kwa kuwa sehemu za kuchimba dawa au sehemu za kujisaidia au ita sehemu za vyoo zinajulikan basi ninaomba wizara zinazohusika zifanye utaratibu wa kuziendeleza na kuweka vyoo ili kuepusha mlipuko wa magonjwa.

b) Kwa faida ya kizazi kijacho na mazingira kwa ujumla zitengwe sehemu maalumu za kujisaidia ili kudhibiti uchafu unatupwa maeneo haya yasiyofuatiliwa na mtu yeyote yule.

Sijagusia sehemu zingine kama barabara za Dar -Moshi, Dar - Mtwara, nk, kwa sababu, I have never been those places. If anyone could bring forward what is going on those routes would be grateful.

Nawakilisha

Njimba
 
mazingira ni uhai wa binadamu na viumbe vingine tukiyaalibu ndo mwish wa maisha yetu,lakini pamoja na hawa watu kuchimba dawa athari kwa mazingira sio kubwa sana kama za kiwanda na uchafu uliotapakaa kila sehemu hasa kwa dar.
Dar ina takiribani watu milioni nne na 90%wanaishi kwenye maeneo yasizopimwa na zaidi ya asilimia 80% wanatumia vyoo vya shimo na ambavyo sio rahis kuleta gari na kutoa huo uchafu wa binadamu.
Na dar ina zalisha takribani tani 2600 za uchafu kutoka majumbani na kwingineko kila siku na huu uchafu utupwa ovyoovyo katika maeneo yasiyo rasmi na pia dar pamoja na kubinafisha ukusanyaji wa taka ndo huduma imezidi kuwa duni magari yenyewe yanayozoa taka na yenyewe ni taka,hamna vifaa na hivyo kwa ujumla tanzania hatujaelewa dhana nzima yakubinafsisha(kwa tanzania tunabinafsisha ili kudumaza huduma na kuwa andalia watu wengine ulaji)
Elimu ya mazingira ni muhimu lakini utakapotoa elimu bila kutengeneza mazingira ya kutumia hiyo elimu basi hapo ndo pabaya zaidi kwa mfano vijana wanaosoma chuo kikuu kama cha dar("the cream"as many misbelieve) utakuta chuo kimejaa chupa za maji, karatasi,mifuko ya plasitiki ijapokuwa elimu inatolewa lakini vijana hawako tiyari kuitumia...kuna kipind niliandika proposal likiwa na kichwa"the role of the environmental education in higher learning intitutions to environmental conservation" ijapokuwa sikumalizia utafiti wangu lakini kwa kuangalia elimu ya mazingira bado haijawasaidia waliowengi kutunza mazingira bali kushinda mitihani.
Mwanafunzi tena wa "geography and environmental studies"siku moja nilimfuma anatupa uchafu pasipo takiwa ni kamuuliza"mazingira unayosoma yanakusaidiaje katika kutunza mazingira"si kupata jibu....wengine yuko kwenye daladala anatupa uchafu nje na nani hatauokota?
watu wanaoathirika na uchafu wa viwnda cheki na mahakama ili haki itendeke...orders are there waiting to be given.....the industry should be responsible unless if people were not permitted to be where they are.....

"ELIMU ZAIDI INATAKIWA"
 
Uchafuzi wa mazingira unasababisha athari nyingi katika jamii. Uchafuzi huo wa mazingira unatokana na kutupa takataka ovyo katika sehemu zisizoruhusiwa kama barabarani, kwenye mazingira ya nyumba zetu na kadhalika. Wazalishaji wakubwa wa takataka ni viwanda, tasisi za elimu (shule na vyuo), hospitali, tasisi za dini n.k. Ili kuepuka athari hizo elimu ya mazingira ni muhimu sana.

Mabadiliko ya tabia ya hali ya hewa duniani ni miongoni mwa athari za uchafuzi wa mazingira. Hali ya joto imeongezeka duniani, barafu katika milima imepungua au imekwisha. Mlima Kilimanjaro kwenye miaka ya 1970 na 1980 ulikuwa umefunikwa na barafu kwa kiasi kikubwa, kwa sasa barafu imeisha. Hii imetokakana na athari za uharibifu wa mazingira. Maji katika bahari yameongezeka ina maana kina cha maji baharini kimepanda, visiwa vingine vimemezwa na bahari.

Athari nyingine ni kuibuka kwa magonjwa kama magonjwa ya ngozi na kansa. Haya yote yanatokana na maendeleo yasiyokuwa endelevu (non-sustainable development)

Tutunze mazingira kwa faida ya wote. Mazingira yatunzwe kwa kizazi hiki na kijacho. Kila mmoja akiwa mlinzi wa mwingine/mwenzake katika matumizi ya mazingira nadhani tutafanikiwa kupunguza athari za binadamu katika mazingira na kupunguza magonjwa ya mlipuko na kuyahifadhi mazingira yetu na kufurahia matunda ya mazingira mazuri kwa kizazi hiki na kijacho. Elimu ya mazingira ni muhimu kwa kila mtu.

Elimu ya mazingira inafaa. Kitu ninachojiuliza ni hiki: Jijini Dar es Salaam kuna watu wanajishughulisha na kilimo cha mboga. Lakini maji wanayotumia yananuka kupindukia. Baadhi wanachota kwenye mitaro inayotiririsha maji machafu (na pengine yenye kemikali). Hivi kweli maji hayo ni salama kwa matumizi ya binadamu?

Naomba mchango wenu - nielimishwe zaidi.
 
elimu Ya Mazingira Inafaa. Kitu Ninachojiuliza Ni Hiki: Jijini Dar Es Salaam Kuna Watu Wanajishughulisha Na Kilimo Cha Mboga. Lakini Maji Wanayotumia Yananuka Kupindukia. Baadhi Wanachota Kwenye Mitaro Inayotiririsha Maji Machafu (na Pengine Yenye Kemikali). Hivi Kweli Maji Hayo Ni Salama Kwa Matumizi Ya Binadamu?

Naomba Mchango Wenu - Nielimishwe Zaidi.

Maji Yanayonuka Yanaweza Kuwa Salaama Kwa Matumizi Ya Binadamu?mbona Hivyo
 
Maji Yanayonuka Yanaweza Kuwa Salaama Kwa Matumizi Ya Binadamu?mbona Hivyo

Asante ndugu Balingilaki. Kwa taarifa yako, mboga nyingi tunazotumia Dar es Salaam zinamwagiliwa maji hayo yanayonuka kupindukia.

Nenda Chang'ombe pale karibu na Kanisa Katoliki (kando ya makaburi) along Mandera Road, pita barabara ya Uwanja wa Taifa kuanzia sehemu iitwayo Magorofani hadi karibu na baa fulani hapo (kama unatokea Keko kuelekea Uwanja wa Taifa), angalia upande wako wa kulia kuna eneo linalimwa mboga na pembeni kuna mtaro wa machi yanayonuka sana na ndiyo yanayotumiwa kumwagilia hizo mboga; pita Kawawa Road (kutokea Magomeni kuelekea Msimbazi Centre) na angalia upande wako wa kulia kuna bonde kubwa na pale panalimwa mboga za kila aina na angalia maji yanayotumiwa.

Nadhani kuna sehemu zingine kama hizo na mbaya zaidi wakazi wa Dar es Salaam wananunua hizo mboga wakiamini zinalimwa na kutunzwa katika mazingira ya kibinadamu bila kujua kuwa soko holela halijali ubinadamu bali pesa!

Hivi kwa nini serikali isihamasishe wakulima hao (na kuwasaidia) kuchimba visima vya maji salama yanayoweza kutumika kumwagilia mboga zao? Au hawanyi hivyo kwa vile viongozi wetu hawali mboga zinazotoka kwa wajasiliamali hao ingawa walipa kodi kwa namna moja au nyingine?
 
Back
Top Bottom